Ziara ya Waziri Mkuu yaahirishwa Mbeya

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,804
Mbeya. Mkuu Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kuwa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani humo imesitishwa kufutia kifo cha aliyekuwa Waziri wa ulinzi wa Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.

Homera amesema leo Jumanne Agosti 3, 2021, akiongeza kuwa Waziri Mkuu Majaliwa ameondoka kuelekea Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuungana na Watanzania na familia ya marehemu kuomboleza msiba huo.

"Ni kweli ziara ya Waziri Mkuu imehairishwa na mpaka hapo baadaye itakapotolewa taarifa nyingine na Serikali na kwamba wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo mkubwa kwa taifa,familia na watanzania kwa ujumla," amesema.

Amesema kuwa licha ya kuahirishwa kwa ziara hiyo, Waziri Mkuu ameagiza kuzinduliwa kwa kitabu cha fursa za uwekezaji ambapo mgeni Rasmi atakuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Mbunge wa Jimbo la Lupa, Masache Kasaka amesema kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo na kwamba kama wabunge wataungana na serikali kuomboleza na kuungana na familia ya marehemu.

"Ni msiba mkubwa kwa Taifa hivyo tunaipa pole sana familia ya marehemu kwani ni pigo katika vyombo vya ulinzi na usalama hivyo tumwombe Mwenyezi Mungu atusimamie katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo,” amesema Kasaka.
 
Huyu kassim ananikumbusha zama za Ghalib akiwa Makamu wa Rais, ceremonial zaidi
 
Back
Top Bottom