Ziara ya Waziri Mkuu nchini Brazil yaleta tumaini jipya ktk harakati za kupambana na tatizo la umeme

jozzb

Member
Jun 30, 2011
87
20
IMG_5328.JPG

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Madini na Nishati wa Brazil, Mhe. Eddison Lobao (kulia) October 5, 2011 kwenye Ofisi za wizara hiyo zilizoko Brasilia. Yuko katika ziara ya kikazi nchini humo.
BRAZIL YAAHIDI KUSAIDIA KUTATUA KABISA TATIZO LA UMEME

BRAZIL imeahidi kuisaidia Tanzania kondokana moja kwa moja na shida ya umeme kwa kutoa teknolojia na uwezo wake chini ya uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Ahadi hiyo ilitolewa jana Jumatano Okt. 5, 2011 na Waziri wa Madini na Nishati wa Brazil, Bw. Edson Lobao katika mazungumzo rasmi ofisini kwake mjini Brasilia, makao makuu ya Serikali ya Brazil, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye anaitembelea nchi hiyo.BARUA HII NI NDEFU JAMANI.NAPENDEKEZA UISOME NA TUICHAMBUE PAMOJA ILI TUJUE UHALISIA WAKE
INAPATIKANA HAPA << ZIARA YA PINDA>>

UKIISOMA,NJOO TUIJADILI PAMOJA
 
Patamu hapa, leo utasikia wameenda thailand kuleta mvua, keshokutwa utasikia wamekwenda japani kuchukua power tiler kwa ajili ya kilimo kwanza, keshokutwa utasikia wamekwenda sijui wapi kuchukua nini, lakini ukiangalia efficient ya kile walichokifuata utatamani uhame dunia
 
hajatoa chozi kweli huko? hii safari nasikia aliililia ile mbaya coz JK ndo alitaka kwenda mwenyewe.
 
pinda ni kiongozi niliyekuwa ninamuheshimu,kwa sasa hana credibility yoyote.anapigishwa kwata kama mtoto mdogo. kaenda brazili ili akutane na wawekezaji wanaotaka ardhi kwenye makambi ya zamani ya warundi ya katumba na mishamo???nakumbuka alibanwa kuhusu uwekezaji huu na Alima mdee kuhusu ardhi hiii akachomoa lakini sasa amekuja na mkutano wa uwekezaji mkoa wa rukwa na mkutano wenyewe ni 17/10/2011.CCmagamba kila mtu ni msanii tusidanganyane
 
sioni haja ya kubeba msalaba wa mwenzio. Ni kweli pinda alikuwa mtu mzuri saaana.sasa kama anaona anapelekeshwa kwa nini asijihudhuru? Kwani uwaziri kitu gani? ( sijathibitisha na siamini kama anapelekeshwa,ila kama ni kweli,sioni haja ya kuendelea) ningekuwa mimi,ningejitoa
 
Patamu hapa, leo utasikia wameenda thailand kuleta mvua, keshokutwa utasikia wamekwenda japani kuchukua power tiler kwa ajili ya kilimo kwanza, keshokutwa utasikia wamekwenda sijui wapi kuchukua nini, lakini ukiangalia efficient ya kile walichokifuata utatamani uhame dunia

Ni kweli ndg yangu viongozi wetu ukiwafuatilia sana "utamanani uhame dunia" chukulia majukwaani na wakienda zghaibuni wanapitisha bakuri kwa nia ya kile wanachodai kufuta kabisa tatizo la umeme TZ tena kwa kipindi kifupi(kama iyo trip ya Pinda Brazil).Lakini hapo hapo wanataka kuiongezea Symbion mkataba wa miaka 20 (refer Raia mwema, Raia Mwema). Ndio hapo wazalendo wanahoji miaka 20 ni ya dharura gani? Kwa kifupi ni kwamba viongozi wetu hawana utashi wa dhati wa kushughulikia tatizo la umeme TZ, zaidi ya kulitumia kujinufaisha wao. Usishangae hizi ziara zao zikaleta kampuni nyingine sytle ya RICHMOND/DOWANS na sasa SYMBION.
 
United Republic of Tanzania Company Limited.

Kwa wale tuliosoma Saint Kayumbas mtakuwa mnakumbuka, kengele ya break ikilia saa nne wote mnakusanyika sehemu vinapouzwa vyakula hapo ndo kila mtu anatumia vijisenti alivyopewa na mzazi asubuhi kununua chochote, kuna wale waliokuwa hawapewi kabisa ikifika muda huu anakuwa anazunguka kwa rafiki zake akiomba kidogo kidogo, kwa huyu ice cream, yule andazi, kwa mwingine sambusa hadi kengele ya kurudfi darasani inalia ameshiba kabisa tena kuliko wale walionunua.....sasa imekuwa serikali yetu, najiuliza hivi wale ombaomba wa shuleni ndio leo hii viongozi serikalini?
 
Hapo kwenye bold ndo nini tena. Hapo unatusema wengi naomba usirudie tena.
 
Back
Top Bottom