Ziara ya Waziri Makamba nchi zinazozalisha mafuta haijaleta tija kama alivyotangaza

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,366
2,000
Ndugu zangu,

Miezi ya hivi karibuni Waziri Makamba alitembelea nchi za ghuba zinazoongoza kwa uzalishaji wa mafuta ulimwenguni.Baada ya kurejea alituhakikishia kuwa mwezi Disemba mwaka huu mafuta yatashuka bei kwani kafaniiiwa kuwashawishi wazalishaji ili Tanzania kupitia TPDC inunue mafuta moja kwa moja kwa wazalishaj na sio kwa watu wa kati.Utaratibu huu ungepunguza bei ya mafuta.

Je, nini kinaendelea?ni kweli kuna makubaliano ya TPDC kununua mafuta moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji?
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,019
2,000
Niliandika sehemu humu na nitautafuta huo uzi mwisho wa siku nikatukanwa kuwa mimi Camel Oil nikasema dua likubaliwe niwe Camel oil. nilisema bei haitashuka wala hakuna kitu kama hicho na leo maneno yangu yametimia.

Bei haipangwi tu hata nyanya sokoni bei hazifanani ni demand and supply. TPDC walijichanganya ku tender bei ndogo imekula kwao hakuna kushuka wala nini mafuta yanaamuliwa bei huko soko la dunia kwa mahitaji hayatolewi kisiasa tutakupa bei hii. Serikali badilishe mfumo wa kuagiza mafuta ilete ushindani.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,668
2,000
Niliandika sehemu humu na nitautafuta huo uzi mwisho wa siku nikatukanwa kuwa mimi Camel Oil nikasema dua likubaliwe niwe Camel oil. nilisema bei haitashuka wala hakuna kitu kama hicho na leo maneno yangu yametimia. Bei haipangwi tu hata nyanya sokoni bei hazifanani ni demand and supply. TPDC walijichanganya ku tender bei ndogo imekula kwao hakuna kushuka wala nini mafuta yanaamuliwa bei huko soko la dunia kwa mahitaji hayatolewi kisiasa tutakupa bei hii. Serikali badilishe mfumo wa kuagiza mafuta ilete ushindani.
Mbona bei kwenye soko la dunia inazidi kushuka lakini Tz inapanda?
 

Galileo_Gaucho

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,878
2,000
Ni kijana aliyewahishwa kujua makubwa kabla hajapevuka kwa hio anakosa natural intelligence na ndiomaana huoni akili zenye kuakisi Umakamba katika uongozi, Yule shemeji yake Mzungu alimaliza maelezo yote, vijana wengi waaminio ni wateule na wenye CCM akili zero, Makamba Urais ndio basi na Upm ndio basi, aendelee kuchuma kwa maisha mengine.

Kawekwa pale kama mwana wa mwanakikundi iko hivo tu. Ni mtazamo tu.
 

Kaka pembe

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
904
1,000
Makamba anasakamwa sana na kundi lililoondolewa hasa yule mbunge wa kule kwa jiwe
Ficha ujinga wako. Jibu hoja kwani makamba hakutangaza bei ya mafuta kushuka mwezi 12?
Hakusema ziara yake nchi za emirates na Algeria zitaondoa middlemen katika uagizaji mafuta?

Acha siasa kwenye maisha ya watu ya watanzania. This government is failing kama haitaregulate mfumuko huu wa bei za vitu.

Wanasiasa wao wanaogelea kwenye michongo yao huku wakiyafanya maisha ya watanzania kuwa magumu.
We are people on the ground and we are the same people who feels this heavy weight of bureaucracy.
 

FM WOLLE

Senior Member
May 4, 2016
142
250
Ninachoshukuru ni mama kumpa wizara ya Nishati, hii imetusaidia kuondoa tongotongo za wale waliokuwa wakimfagilia na kuona anafaa kuliongoza Taifa. Ukweli wa uwezo wake umedhihirika pasina chembe ya shaka. Thank you God! Kikubwa tujitahidi kutunza kumbukumbu.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,519
2,000
Mkuu Wakudadavuwa , kwanza asante kwa bandiko zuri lenye kutanguliza mbele maslahi ya taifa, kufuatia ujio wa online media, kila mtu anayejua kusoma na kuandika, anajiona ni mwandishi na anaweza kuandika chochote, kuripoti chochote au kuhoji chochote. Sasa kwa vile mimi ni mwandishi, na huu ndio umri wangu wa kustaafu, nimejitolea, kila ninapokutana na andiko lenye maslahi kwa taifa, hatua ya kwanza ni kumpongeza mwandishi kwa kuleta bandiko la maslahi ya taifa as an ecouragement azidi kuleta mabandiko yenye maslahi kwa taifa na hivi ndio kutumia mitandao ya kijamii kulisaidia taifa na huu ndio uzalendo wa kweli wa mtu kwa taifa lake. Sasa wewe Mkuu Wakudadavuwa, umekuja kiuzalendo zaidi, hii ni dalili njema ya maturity zaidi, keep it up.

Hatua ya pili ni kulifanyia scrutiny kidogo tuu ya kuonyesha strengs na weakness za bandiko husika, hivyo kukupiga darasa to be a better writer, hivyo sasa pokea darasa,

  1. Heading ni tofauti na contents "Ziara ya Waziri Makamba nchi zinazozalisha mafuta haijaleta tija kama alivyotangaza" -hII heading ni wrong heading kwasababu umeweka heading yenye critics ikiwa final and conclusive kuwa ziara ya JM haijaleta tija kama ilivyotangazwa. Tija za ziara haziji hapo hapo, it takes time, its a process, it needs time kabla ya mafanikio kuonekane, sio kama kunywa maji, kiu inakata, tija za ziara ni kama kudungwa ile kitu, baada tuu ya kudungwa leo ile kitu, kesho yake mtoto hazaliwi, it needs time kukaa miezi tisa tumboni, kuna gestation period, kuna first trimester, miezi mitatu ya mwanzo ya kichefuchefu na kutapika, kuna second trimester ya ya miezi 3 ya pili ya viungo kufanyika na a third trimister ya kiumbe kukomaa ndio azaliwe. Wewe anataka JM mara tuu baada ya ile ziara, awe amedunga hapo hapo na kesho yake mtoto zaliwe?. No, tumpe muda!
  2. Content ya para ya kwanza umeweka subject matter, that is good, msomaji anaelewa unazungumzia nini kwa kuweka background na the expected results ya ziara hiyo. Kikawaida kuna short time results, medium term na long term. Haya mafuta yaliyopanda bei yalikuwa procured kabla ya ziara hiyo. Augizaji wa ziara hiyo bado, hajaleta mzigo wake, mzigo ukija, bei lazima itashuka.
  3. JPM alipoingia, akaitaka serikali kufanya manunuzi ya magari ya serikali kutoka viwandani kwa bei ya kiwandani, bila kutumia ma agents ili kupunguza bei, kama UN inavyonunua magari yake. Na ndivyo tulivyonunua ndege. GIPSA wakaenda Japan Toyota, Toyota wakawakubalia watawapoozea bei, lakini kwa vile Tanzania wana Agent, mzigo huo lazima upitie kwa agent hivyo serikali it collect bills of land kwa agent na ni lazima ulipie chochote kitu. Hivyo inawezekana hata kwenye mafuta ni hivyo, kama serikali yetu ilikuwa na bulk supplies rights, halafu tuna freight company yetu, halafu tuna shipping company yetu, halafu tunamiliki oil tanker ships zetu, hilo lingewezekana. Lakini hata tukiagiza direct, kwa vile hatuna kampuni ya ununuzi, lazima tutapitishiwa kwa agent wa ununuzi, hata zile ndege, Watanzania tulielezwa zimenunuliwa kwa bei ya kiwandani, direct, kiukweli zilikuwa ni ndege za Kazakhstan, malipo yamelipwa kupitia agent, cha juu kimewekwa ndio maana hukuweza kusikia tumenunua kwa bei gani na fedha zimelipwa wapi ila sio kiwandani!
  4. Hoja yako ya closing ya bandiko lako, "Je nini kinaendelea?ni kweli kuna makubaliano ya TPDC kununua mafuta moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji?", hii ndiohoja ya msingi na hii ndio ilipaswa kuwa heading yako.
  5. Mwisho. Be very careful wakati wa kufanya critics kwa "people to watch" like JM, huwezi jua kesho atakuwa nani!, akitokea akiwa, utakuwa mgeni wa nani?
Paskali
(Mwalimu wa Uandishi)
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,541
2,000
Ficha ujinga wako. Jibu hoja kwani makamba hakutangaza bei ya mafuta kushuka mwezi 12? Hakusema ziara yake nchi za emirates na Algeria zitaondoa middlemen katika uagizaji mafuta?

Acha siasa kwenye maisha ya watu ya watanzania. This government is failing kama haitaregulate mfumuko huu wa bei za vitu. Wanasiasa wao wanaogelea kwenye michongo yao huku wakiyafanya maisha ya watanzania kuwa magumu.
Atleast now imeeleweka kwamba chuki dhidi ya Magufuli zilikuwa upumbavu if you ain’t in the power circle!

Marope ni failure na amedhihirisha hilo tayari regardless ya Mbeleko aliyopewa na ni swala la muda tu itafahamika kwamba yupo pale kimkakati. Yani dhamira sio kuwasaidia watu wapate nafuu ya maisha bali ni ku accumulate wealth kupitia michongo kwa mgongo wa wizara. Masafari na madili ndio lengo kuu kwa sasa.

Wanyonge mtachora chini 😅
 

DURACEF

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
1,256
2,000
Ni kijana aliyewahishwa kujua makubwa kabla hajapevuka kwa hio anakosa natural intelligence na ndiomaana huoni akili zenye kuakisi Umakamba katika uongozi, Yule shemeji yake Mzungu alimaliza maelezo yote, vijana wengi waaminio ni wateule na wenye ccm akili zero, Makamba Urais ndio basi na Upm ndio basi, aendelee kuchuma kwa maisha mengine.

Kawekwa pale kama mwana wa mwanakikundi iko hivo tu. Ni mtazamo tu.
You are right. Yule ni kasha tu.
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,541
2,000
Mbona bei kwenye soko la dunia inazidi kushuka lakini Tz inapanda?
Na wana mpango wa kuhold bei hivyo hivyo mpaka February 😅 ili kule ikipanda waendelee nayo 😂!

Cha ajabu bei ikipanda sokoni changes ni instant wala hawasubirii mzigo uishe unaanza kuuzwa bei juu hapo hapo😅 hata kama ulinunuliwa bei chini!

Ila bei ikishuka sokoni wana hold bei ya awali mpaka mzigo uishe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom