Ziara ya Viongozi wa Kitaifa Katika Majimbo ya Pemba

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
605
1,536
Leo tarehe 09 Agosti 2021, Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Ndugu Juma Duni Haji, Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu na Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Ndugu Othman Masoud Othman wameanza ziara ya siku mbili kwenye Mikoa yote ya Kichama Pemba.

Akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha ziara hiyo kilichofanyika katika Jimbo la Konde na kuhudhuriwa na viongozi wa Mkoa, Majimbo na Matawi yote ya Mkoa wa Kichama wa Micheweni, Katibu Mkuu wa Chama Ndugu Ado Shaibu ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwaeleza viongozi na wanachama wa ACT Wazalendo maazimio ya kikao cha dharura cha Kamati Kuu kilichofanyika Unguja jana tarehe 08 Agosti 2021 kilichoitishwa kufuatia hujuma iliyofanyika kwenye uchaguzi wa marudio kwenye Jimbo la Konde.

Kwenye Kikao hicho, Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Ndugu Othman Masoud, Makamu Mwenyekiti Ndugu Juma Duni Haji na Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe waliwasilisha maazimio ya Kamati Kuu kama ifuatavyo;

1. Kusisitiza umuhimu wa mazungumzo katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamo wa Kwanza wa Rais Ndugu Othman Masoud ameeleza kuwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa marudio katika jimbo la Konde, yeye na viongozi wengine wa Chama walifanya jitihada na kuchukua hatua mbalimbali kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Ndugu Hussein Mwinyi kutatua kadhia ya Jimbo la Konde.

Aliendelea kufafanua kuwa kutokana na jitihada hizo za pande zote mbili, ndio maana Mgombea wa CCM aliyetangazwa kuwa mshindi kinyume na matokeo halisi ya uchaguzi huo alijiuzulu.

Ndg. Othman Masoud aliwaeleza viongozi wa Mkoa wa Kichama wa Micheweni kuwa Kamati Kuu imepongeza hatua hiyo ya mazungumzo na kwamba Kamati Kuu inatoa rai kuwa moyo wa mazungumzo uliooneshwa kutokana na kadhia ya Konde, utumike pia katika kushughulikia masuala mengine makubwa yanayoikabili Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wake.

2. Waliohujumu Uchaguzi wa Konde wawajibishwe.

Makamo Mwenyekiti Zanzibar Ndugu Juma Duni Haji aliweka bayana kuwa ingawa Chama kimeridhia kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio kwenye Jimbo la Konde, ni lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe. Alisema ni lazima wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi waliosimamia katika Jimbo la Konde wasirejeshwe tena kusimamia uchaguzi. Pili, ni lazima wale wote walioshiriki kuhujumu Uchaguzi wa Konde kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ndani ya Serikali wawajibishwe.

3. Makubaliano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Yatekelezwe.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Chama ameweka bayana kuwa mbali na kuwa ni takwa la kikatiba, Chama cha ACT Wazalendo kiliingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kutokana na makubaliano yaliyotokana na mazungumzo baina ya Mwenyekiti wa Chama Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar Ndugu Hussein Mwinyi.

Akiyataja makubaliano hayo matatu Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe alisema Maalim Seif na Rais Mwinyi walikubaliana yafuatayo;

i. Kuachiwa huru kwa viongozi na wanachama wote wa upinzani wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na kesi za kisiasa zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020

ii. Kufanyika kwa uchunguzi huru wa kimahakama (Independent Judicial Inquiry) wa uvunjifu wa haki za binadamu kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020

iii. mapitio (review) na mabadiliko (reforms) kwenye mfumo wa Uchaguzi Zanzibar na Taasisi zake.

Kiongozi wa Chama aliongeza kuwa Kamati Kuu imeazimia kuwa Wawakilishi wetu ndani ya Serikali wakiongozwa na Makamo wa Kwanza wa Rais Ndugu Othman Masoud kwa kushirikiana na viongozi wa Chama wafuatilie utekelezaji wa makubaliano hayo.

Leo, ziara hiyo inaendelea katika Mkoa wa Kichama wa Chakechake. Ziara itahitimishwa kesho kwenye Mikoa ya Kichama ya Wete na Mkoani.

Salim A. Bimani, Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.
09 Agosti 2021
IMG-20210809-WA0030.jpg
9q08dj.jpg
IMG-20210809-WA0034.jpg
IMG-20210809-WA0036.jpg


Screenshot_20210809-173309_1.jpg


Screenshot_20210809-173329_1.jpg
 
Haaaa Alijiuzuru kwa sababu za kifamilia.
Nani atahusika kugharamia uchaguzi wa marudio huku waliochempusha matokeo halali wapo
 
Back
Top Bottom