Ziara ya Slaa Kigoma na Tabora ina tija kipindi hiki?

chasuzy

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
595
207
Anachofanya DR slaa kwa sasa ni kitu kinachoacha maswali mengi zaidi ya majibu,kamati kuu imemvua nyadhifa Mh Zuberi Zitto Kabwe na imempa siku 14 za kujieleza kwa nini asifukuzwe uanachama,kabla ya yeye ajajieleza tayari kuna viashiria na maneno kutoka kwa Slaa na Lisu ya nini kitatokea,huu si ustaarabu inaonekana ya kwamba tayari majamaa yameshaandaa nini cha kufanya na kilichopo ni mchakato tu ili ionekane taratibu zimefuatwa lakini siku zote haki inapiganiwa.

Sasa kuna ili la ziara za Mh Slaa kigoma,ikumbukwe Mh Zitto tayari alikuwa na ziara za kuimarisha chama kwenye ngazi ya kanda akianzia na mkoa wa katavi, tabora, shinyanga, geita na kigoma. Alikatisha ziara akaja Dar kuhudhuria kikao cha PAC,baadae aliendelea na mkoa wa shinyanga akakatisha tena ili aende uswisi kufuatilia mabilioni na pia kuhudhuria kongamano baadae wakati anapanga ziara ya Kigoma mambo ya chama yakamkuta,ila ziara yake kigoma ilikuwepo palepale kwani pia yeye ni mbunge. Slaa yeye ameenda kigoma kuimarisha chama au kumbomoa zitto? Ziara yake aliipanga lini? Je na Zitto akiendelea na ratiba yake Slaa na Lissu watasemaje?

Pengine wana chadema mnaweza msilione hili,Uwezi kumjerui Zitto chama kikabaki salama,huyu anao watu wengi walio nyuma yake,siasa za kiafidhina ndizo zinazotaka kuumba tabaka la sisi ndio bora na wenye mawazo sahihi tu,wengine na walio tofauti na sisi ni wasaliti.Pengine inawazekana ikawa ni mambo binafsi ya viongozi wetu kama uzinzi kushindwa kuongoza familia na mengineyo ila na wao si safi,mara ngapi wmekisaliti chama?

Mimi nasema ziara ya Slaa kipindi hiki Kigoma aina maslai kwa chama,kama ilikuwa na dhamira nzuri angemshirikisha Zitto,Yeye ni mbunge na ametoka eneo hilo,Pia anao ushawishi mkubwa sana kwa wakazi wa Kigoma
 
samaki mkunje angali mbichi akikauka akunjiki. CHADEMA kwa sasa haiogopi kumfukuza ZITO tena baada ya vioja vyote hivyo na pumba kujitenga machere. Huwezi kuahurumia kubomoa sehemu yenye ufa ili upatengeneze pawe imara, ukiogopa kupabomoa utakuja kujenga nyumba.
 
Ziara yake aliipanga lini? Je na Zitto akiendelea na ratiba yake Slaa na Lissu watasemaje?

Tatizo lako kubwa unakurupuka bila kufuatilia kisawasawa mambo yanayotokea na yanayojadiliwa, hapo nilipoweka RED kumbuka Ziara hii ya Dr. Slaa kama ilivyofafanuliwa ilipangwa tangu July 2013 ikaahirishwa kwa sababu Dr. alipata safari ya Ziara nje ya nchi sasa unapokuja na Hoja za Kiroja tunashindwa kukuelewa.
 
Vipi mkuu, hii ajira yenu inalipa kweli? Maana naona mnataka kufia kwenye mitandao wewe na mkeo Simiyu na ZeMarcopolo!! Msalimieni mwajili wenu Mwanadiwani
 
Zitto anafukuzika vizuri tu na Chama kitabaki kuwa IMARA zaidi!
Asitishie watu nyau kwamba yeye ni zaidi ya Chama! Hata ANC ilimeguka na kikaundwa chama kingine cha PAC lakini ANC haikuteterek, ilizidi kuimarika!
 
1426246_204126326439006_277632284_n.jpg
 
Kuna tofauti kubwa kati ya ziara hii ya Dr.Slaa compare to Mikutano ya JK na wazee wa jiji la Dar. Anachofanya Dr.Slaa ne kwenda kuwaeleza ukweli wa jambo gani zitto alifanya ndani ya CDM. Dr.Slaa ameruhusu maswali na kuwaalika wanaccm waliokuja na mabango kukaa kwa utulivu. Hiyo yote ni ujasiri na inavunja nguvu za CCM/Zitto
 
CHADEMA wanakodi watu wakuja kwenye mikutano!tunakoeleka ni kugumu zaidi,tunakodi waandisha wa habari wa kuandika propaganda?Yote haya ni baadhi tu ya matumizi babaya ya pesa ya Dr slaa.Ole wake mtu aoji ,kila jina baya utaitwa
 
Kama Slaa angekuwa kweli ana lengo la kuimarisha chama Kigoma,kwanin asisubiri vuguvugu la Zitto na Chadema lifikiwe muafaka?There z somthing wrong n this proves us that they know what is going to happen.The truth can never perish when a lie comes from a fool.
 
Zitto si zaidi ya CHADEMA lakini anatisha....Arusha Chadema imelazimika kwafuata watu Siko kuu tofauti na zamani walikuwa wanafanya mkutano Soweto na watu wanajaa. Sasa hivi wanafuata watu sokoni na bado watu wapo busy...... Lema anakera lakini anapendwa na vibaka wachache wa Ungalimited maana ni marafiki zake wa zamani
 
Ni kweli.
Hata ccm kule mtwara wakati nyuma za mbunge zinachomwa, hawakuandaa mkutano, mpaka upepo lipopita.
CDM walipaswa kujifunza.
 
samaki mkunje angali mbichi akikauka akunjiki. CHADEMA kwa sasa haiogopi kumfukuza ZITO tena baada ya vioja vyote hivyo na pumba kujitenga machere. Huwezi kuahurumia kubomoa sehemu yenye ufa ili upatengeneze pawe imara, ukiogopa kupabomoa utakuja kujenga nyumba.

hamuwezi kuthubutu, Kigoma SLAA alipata 40% mwaka 2010 ikilinganishwa na Kilimanjaro 5%-alichokuwa akikifanya SLAA ilikuwa kutest zari akidhani Waha ni wajinga na Kahama ilikuwa danganya toto-walimtuma ilikujua REACTION ya watu wa Kigoma ili iwasidie kufanya maamuzi dhidi za ZZK, sasa ujumbe wetu kwa CC ya CDM ndio huo anapewaa SLAA kwa kipondo-mfukuzeni kama hamjipendi WA KANDA ninyi
 
Zitto anafukuzika vizuri tu na Chama kitabaki kuwa IMARA zaidi!
Asitishie watu nyau kwamba yeye ni zaidi ya Chama! Hata ANC ilimeguka na kikaundwa chama kingine cha PAC lakini ANC haikuteterek, ilizidi kuimarika![/QUOTET]

hapa unashindwa kuzingatia uhai wa siasa na vyama inategemea historia, jiografia na kiwango cha utambuzi(elimu)-hapa ulitakiwa uzungumzie NCCR ambayo MREMA alikuwa anazima gari watu wanalisukuma mafuta yasiishe lakin alipoleta ubwege sema walimfanyaje...........sio habar za Afrika kusini
 
unalia lia nini?
kama vile houni ni kwa jinsi gani huyo msaliti alivyo kisaliti chama mpaka tulipoteza majimbo mangapi uchaguzi 2010 hilo wewe hulioni

wewe endelea kumlilia zito sisi hatujali hata akiondoka na wanachama wapuuzi na wasaliti kama yeye watu makini na wazalendo bado tupo CDM hatuna cha kupoteza

mwambie zito aende CHAUMA ili wewe kibaraka wake mfuateni huko
 
Zitto anafukuzika vizuri tu na Chama kitabaki kuwa IMARA zaidi!
Asitishie watu nyau kwamba yeye ni zaidi ya Chama! Hata ANC ilimeguka na kikaundwa chama kingine cha PAC lakini ANC haikuteterek, ilizidi kuimarika!

hapa unashindwa kuzingatia uhai wa siasa na vyama inategemea historia, jiografia na kiwango cha utambuzi(elimu)-hapa ulitakiwa uzungumzie NCCR ambayo MREMA alikuwa anazima gari watu wanalisukuma mafuta yasiishe lakin alipoleta ubwege sema walimfanyaje...........sio habar za Afrika kusini
 
wewe ulikuwa wapi, maswalimu yako yote yameishajibiwa humu ndani, pitia threads zimo za kutosha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom