Ziara ya siku moja ya Kinana na Nchimbi mjini Songea, je ni kufuta ile ya Mbowe 26.5.2013?


Ngalikivembu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
1,920
Likes
364
Points
180
Ngalikivembu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
1,920 364 180
Ikiwa imepita wiki moja tu baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kufanya mkutano mkubwa pale viwanja vya shule ya msingi Matarawe 26.5.2013, naye katibu mkuu wa CCM Bwana A.Kinana na Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Emmanuel Nchimbi walifanya mkutano katika uwanja wa majimaji hapo jana 2.6.2013. Mambo waliyozungumzia hiyo jana ni pamoja na kuwaambia wananchi wa mji wa SOngea kuwa wasiwe na wasiwasi juu ya rasimali zetu kwani suala la gesi na makaa ya mawe ni kwa ajili ya watanzania na kuwa juu ya umeme hapa Songea utapatikana kwa uhakika katika siku zijazo.Hii ni ahadi ya CCM kwa wanachi wake.

Lakini kubwa nililoliona ni kuwa Bwana Nchimbi ni kama alikuja kufuta kile kilichozungumzwa na Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa Mkoa.Hii ziara haikupangwa rasmi na CCM ila ilibidi Nchimbi akimbie haraka na kumwalika Kinana kutoka Njombe alikokuwa anafanya ziara na kuja Songea. Nchimbi alikuja na helikopta ya polisi kitu ambacho aliwapa kazi polisi kuilinda toka siku ya Jumamosi na Jumapili ikimsubiri yeye pale uwanja wa ndege wa Songea.

Kubwa ambalo limenishangaza ni hili la kuwasomba wananchi kwa malori mawili makubwa toka sehemu mbalimbali ya Manispaa ya Songea na nje ya Manispaa.Ni kwa vile kamera yangu iliisha charge baada ya ziara binafsi katika vijiji vya jimbo la Mbinga Mashariki, ambako huko nimegundua jambo kubwa sana lenye faida kwa Chadema.Hili nimepanga nisiliweke hapa jamvini bali niwape yale niliyoyaona moja kwa moja kwenye ofisi yao ili watendee kazi kama kweli wana nia ya kushinda uchaguzi ujao na kunyakua viti vyote vya jimbo la Mbinga.Niwieni radhi.

Swali langu ni hili, hivi kwanini hawa CCM hawawezi kufanya mkutano bila kuwalipa watu toka sehemu mbali mbali?

Jioni hii nimerejea toka kijiji kimoja ambacho nilihudhuria mazishi ya ndugu yangu mmoja.Kule nimekutana na wazee wenye busara zao ambao walihudhuria mkutano wa jana.Hawa wazee waliniambia walienda kwa sababu Bwana Nchimbi aliwalipa shilingi 10,000 kwa kila aliyekubali kwenda uwanja wa majimaji ambae alikwenda kwa lori.NASISITIZA HILI SI LA KUTUNGA.NI JAMBO LILILOFANYIKA.Wazee hawa ambao ilibidi nijionyeshe sura yangu halisi kuwa mimi ni mfuasi wa kambi gani,waliniambia jambo ambalo kumbe hata wao wanalijua ni kuwa HUWEZI KUGOMBEA NAFASI YOYOTE KWENYE CCM KAMA HUNA FEDHA.Usijaribu.Wakasema, sisi wazee huwezi kututoa huku kijijini bila kuona una nini mkononi mwako.

Kwa kweli nchi hii mikononi mwa CCM ni janga kubwa.Tujadiliane tufanye nini? Kwa wale walioona taarifa ya TBC leo,ule umati uliouona kwenye picha si wakazi wa Manispaa hii bali walisombwa kwenye malori toka vijijini.

Naomba kuwasilisha na hii ndio hali halisi ya siasa ya CCM.
 
C

Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Messages
1,339
Likes
5
Points
0
C

Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
Joined May 16, 2013
1,339 5 0
Kamanda asante kwa analysis yako ya kina,
Ukweli utajulikana tu siku moja hata watudanganye namna gani sasa mwisho wao ndo huo ushafika. Kiukweli hata wangewapa kiasi gani cha fedha jambola msingi ni kwamba ELIMU kwa UMMA ndo hiyo inapita kwa kasi kubwa.

Tunashukuru kwamba wazee wa CHADEMA wazidi kupita pita kila kona ili wajue anguko lao limefika kabisa.

Hakuna hata mmoja awezaye kuficha moto unaofuka, ni sawa na kikohozi hakuna awezaye kukibada lazima kikifika wakati utakohoa tu hata kama uko kwenye dhifa ya Taifa na Obama.
 

Forum statistics

Threads 1,275,212
Members 490,932
Posts 30,535,930