Ziara ya rais wa tanzania huko north korea

Mwalimu Nyerere alikwenda huko mwaka 1988 akiwa mwalikwa wkenye tamasha la Vijana la Dunia, ingawa wakati huo alikua amesha ng'atuka Urais(yeye alikua hapendi kusema amestaafu) na kwa wakati huo alikua ni Mwenyekiti wa CCM

Alikua ni rafiki mkubwa wa Kiongozi wa wakati huo nadhani alikua ni Kim Il Sung
 
Jamani wahenga naomba nifahamishwe kama kuna rais yeyote wa Tanzania aliwahi kufanya ziara huko north Korea na kama bado kwa nini hawakutaka kwenda huko

Kivutio kikubwa duniani ni miji iliyopangwa na kujengwa kwa ufasaha (na siyo wanyama na milima). Kuna jitihada mbalimbali zimefanyika na mipango jiji la DAR ES SALAAM/ZANZIBAR ili kuhakikisha inakuwa kama Dubai lakini tukaambulia kuwa na majengo ya ovyo na kujenga nyumba ndogo ili ipo siku tutabomoa na kujenga Gorofa ambapo kwa uhalisia/kiasi kikubwa tunapoteza sumenti nyingi/mchanga mwingi/Gypsum/mapati (steel), kutokuwa na mifumo ya majitaka/maji safi, kusababisha foleni/uchawi n.k.

Aidha, hali hii inajidhihilisha kwenye majiji yote ya Tanzania (ikiwemo mbeya, Iringa, Arusha) kwa kuwa na vyoo kibao kila nyumba, barabara zisizo tengenezeka wakati tunaweza kutumia zege na kuwa na balabala njema kabisa. Kwa hali inavyokwenda tutafika miaka 100 tukiwa na dreams za kwenda kuangalia miji mizuri na iliyopagwa tutakaposafiri kuelekea ulaya/dubai/china. Bila kujiuliza ilijengwaje?

Kama ukijiuliza hili swali ndipo utakapo jua kuna haja ya watanzania kutenga miezi miwili (happy month) kwa kila mwaka kwa ajili ya watu kufanya mazoezi ya kujenga miji ambayo itahakikisha ramani ya mipango inatekelezwa kikamilifu. Ambapo, Serikali inatenga fungu/fedha za kujenga miji (labda kama mafundi wanataka kuchezea tope milele maana nyumba hazina lifespan) na kila mtu anajua kuwa Serikali haifirisiki kwani ipo vizuri kuzungusha fedha kwa njia ya kodi na tozo na viwanja ni vya Serikali.

Maisha ni mipango miji.
 
Nchi unayo sema ww ina njaa imeweza kutengeneza zana hatari za kivita na wapo vizuri kwenye Technologia kukushinda nyie mlioshiba na bado mskini wa kupupwa
Labda wewe ndo maskini wa kutupwa, kwanza silaha zinaliwa? Raia wa huko wanakimbia kila siku halafu useme kuna cha maana. Pamoja na hayo na sisi ni nchi ya viwonder, kingine kimezinduliwa jana.
 
NK kumejaa njaa tu labda kama unataka nuclear ya bei rahisi
Mkuu, Acha kabisa kusema kitu usichofahamu, nimepata bahati ya kukaa North Korea mwezi mmoja, hiyo njaa unayosema inaanzia wapi kuingia huko ? Viongozi wa North Korea wote wana tabia moja, sheria na kanuni zinaheshiwa, mkiaambiwa leo kulala ni saa 2 kamili jioni, ni lazima muda huo raia wote mlale, yaani ni Udicteta wa Kimocasia. Mnafanyiwa ukatili, lakini maisha mazuri kwa hiyo inakuwa sehemu ya maisha yenu. Ni sawa na kumchemsha chura kwa kuanza kumweka kwenye maji ya baridi, halafu ukaanza kuchemsha taratibu.
 
Back
Top Bottom