Ziara ya Rais Samia nchini Misri ni kete muhimu kwenye Diplomasia ya Uchumi Tanzania

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108
MISRI NI KETE MUHIMU KWENYE DIPLOMASIA YA UCHUMI TANZANIA

Uhuru Na Umoja

Ukitaka kwenda upesi nenda peke yako, lakini ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako, msemo huu wa wahenga ndiyo unaoongoza falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan katika mahusiano na mataifa mengine duniani.

Ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Misri ni kielelezo kingine muhimu cha jinsi Rais alivyodhamiria kujenga mahusiano mazuri na mataifa muhimu duniani.

Misri moja ya mataifa makubwa barani Afrika na muhimu wake kwa siasa za dunia hasa kwa ushawishi kwa siasa za Mashariki ya Kati, limekuwa rafiki wa Tanzania kwa miaka mingi tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Gamal Abdel Nasser.

Japo si wengi wanaofahamu, moja kati ya barabara muhimu jijini Mwanza ni ile inayopita maeneo ya Capri point, kutoka stesheni na kuzunguka hadi Kamanga Ferry, Barabara ya Nasser ikipewa jina hilo kwa heshima ya uhusiano mzuri wa Tanzania na Misri.

Ziara ya Rais Samia kwa mwaliko wa mwenyeji wake Abdel Sisi, ni hatua nyingine muhimu kukuza na kuimarisha sura ya Tanzania katika diplomasia ya uchumi.

Ili diplomasia ya uchumi iwe na mafanikio ni lazima kwanza Taifa liwe na ushawishi kwa masuala mbali mbali duniani. Ushawishi huo hauwezi kuja bila kuwa na mahusiano mazuri na ya kuaminika kwa nchi zingine.

Kwamba kama Tanzania tuna jambo letu, tunataka liungwe mkono kimataifa, ni lazima kuwa na mataifa mengine yenye ushawishi unayoweza kuyaita rafiki. Haya kabla ya kupeleka jambo lako kwa uamuzi, mathalani wa kupigiwa kura, unakuwa tayari umeteta na marafiki zako ili wao wakikuunga mkono wanasadia kushawishi mataifa rafiki zao.

Katika juhudi za kukuza uhusiano kimataifa Misri ni kete muhimu sana kwenye draft letu la kidiplomasia. Baada ya kuwa ametembelea jirani zetu wa Afrika Mashariki na nchi za Jumuiya ya SADC, hii ilikuwa zamu ya ukanda mwingine wa Afrika.

Kuichagua Misri ni njia rahisi ya kuwafikia Afrika Kaskazini lakini pia mataifa ya kiarabu ambayo nchi hiyo ni mwanachama wa Arab League.

Aidha kampuni kutoka Misri ndiyo inajenga mradi wetu wa kimkakati wa Bwawa la Nyerere. Hili linawafanya kuwa wadau wetu muhimu kiuchum.

Ndiyo maana ziara ya Rais Samia nchini Misri ni hatua muhimu katika kuimarisha taswira ya Tanzania kimataifa.​

20211110_173314.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa picha ya pamoja na Wafanyabiashara wa Misri baada ya kuzungumza na Wafanyabiashara hao leo tarehe 11 Novemba 2021Jijini Cairo nchini Misri

20211111_231117.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia mabadilishano ya Hati za makubaliano katika Nyanja ya kukuza Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri.

20211111_231352.jpg
 
Huyu mama anaenda kubembeleza wafanyabiashara wa Misri wakati nchini kwake anamsulubu mfanyabiashara maarufu na mkubwa kwa mashtaka ya kubumba
 
Back
Top Bottom