Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,400
Napenda kuandika kidogo tu kulingana na uwelewa wangu juu ya Ziara ya Mama nchi Kenya na mikataba mlio tiana sign.

1. Ujenzi wa bomba la gas kutoka Tanzania kwenda Mombasa kwa ajili ya matumizi ya viwanda nchini Kenya,hapa mama unefail pakubwa sana maana yake nikwamba bidhaa za Kenya zitakuwa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi na kuteka soko la Africa Mashariki kuliko Tanzania. Tutarudi miaka ya nyuma tena kila kitu Made in Kenya.

a. Hii sera yetu ya viwanda itakufa maana hatuweza kushindana tena na product kutoka Kenya na vijana wetu watazidi kuwa wachuuzi wa bidhaa kutoka nje.

b. Kenya itatumia mwanya huu kuvutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza Kenya kuliko kuja kuwekeza Tanzania.

c. Tunasafirisha gas kama kuna surplus ya viwanda vyetu na matumizi yetu kama Taifa.Viwanda vyetu bado vinahitaji nishati ya gas lakini bado upatikanaji wake umekuwa mgumu na kwa gharama kubwa

d. Kenyatta amecheza karata yake vizuri katika ujenzi wa gas kuliko Mama sijui washauri wake wamekwama wapi natarajia kuona Kenya ikinufaika zaidi katika utawala wa Mama kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Tanzania na Kenya.

2. Ushirikiano wa anga..hapa Kenyatta anatafuta namna ya kuisaidia Kenya airways..inakwenda ku dominate soko na anga tena kama huko nyuma.hapa kumbuka faidia kubwa ya Kenya Airways inatokana na safari za Tanzania. Dsm, Zanzibar na Kilimanjaro.

Hapa tutalajie Air Tanzania ikifa kifo cha mende kutokana kutoweza kumudu ushindani na Kenya airways. Otherwise kufanyike changes za haraka katika Management ya Air Tanzania.

3. Soko la utalii hapa Kenyatta amecheza vizuri kama pele.
Tutalajie kuona vijana wetu wakiwa watazamaji kama kipindi cha nyuma na soko la utalii nikirudi mikononi mwa wakenya tena.(hapa kwenye utalii wenye fan zao wanaweza kudadavua kwanini Kenyatta amecheza kama Pela)

4. Biashara sioni jipya ni yale yale, hapa Mama ametoka 0-0

Note: Mama washuri wake wamshauri vizuri kabla yakwenda kufanya mikataba kwa niaba ya Watanganyika. Otherwise akubali kutuachia Tanganyika yetu!
 
Uliposema viwanda na gesi, nimekumbuka, Dangote alinyimwa gesi akaamua kutumia Makaa, wakamkatalia pia.

Bakhresa, akanyimwa gesi pale Mwandege.

Gesi ya serikali iliyobaki imesambazwa majumbani kwa staffs wa TPDC na Kinyerezi Tanesco.

Ngoja tuone viwanda vyetu hivi vya mikocheni(TPDC) na Kinyerezi vitakavyoshindana na vile vya urithi vya Kenya vitakavyozalisha kwa urahisi wa gesi yetu wenyewe.
 
Sioni sababu ya kuzua gesi isiuzwe eti kwa ajili ya kulinda viwanda hii roho mbaya
Shida sio kuuza nje..Tunauza nje kwa faida ipi je sisi wenyewe imetutosheleza kwanza?

Kama uwekejazi wa gas ulitokana na kodi za watanzania basi watanzania hao hao kwanza ndio wafaidike na kodi zao.

Tuuze gas baada ya sisi kuwa imetutosheleza kile kinachozidi (surplus)ndio kiuuzwe.

Viwanda vyetu wenyewe vinahitaji gas lakini gas hiyo hiyo hawapewi..inakuwaje unakwenda kumpa jirani yako!
 
Shida sio kuuza nje..Tunauza nje kwa faida ipi je sisi wenyewe imetutosheleza kwanza?

Kama uwekejazi wa gas ulitokana na kodi za watanzania basi watanzania hao hao kwanza ndio wafaidike na kodi zao.

Tuuze gas baada ya sisi kuwa imetutosheleza kile kinachozidi (surplus)ndio kiuuzwe.

Viwanda vyetu wenyewe vinahitaji gas lakini gas hiyo hiyo hawapewi..inakuwaje unakwenda kumpa jirani yako!
Aliyekufundisha uchumi kwamba unauza kitu nje ya nchi tu iwapo una "surplus" mwambie amekudanganya. Comparative advantage na monopolistic competition ndio msingi wa biashara ya kimataifa unaotumika sasa. Na ingekuwa hivyo usemavyo, basi duniani asingeweza kuishi mtu.
 
Back
Top Bottom