Ndugu yangu, hii miradi mikubwa inaenda kwa stage. Unajenga kwanza mfumo mzima wa kiwanda, mitambo na miindombinu yote.Utaanzaje kuzalisha bila kuwa na pesa ya kulipa mishahara?
Au utawakopa wafanya kazi?
Waache mbwembwe.
Hatua ya pili; ni production, ambayo hapo sasa inagusa administrative cost. Vibarua, waajiriwa, management team nk. Binafsi, naamini sh. bilioni 460 kama zilivyoletwa hapa zinaweza kujenga viwanda 100. Tuombe mradi uje ili ndugu zako wewe, yule na mimi waajiriwe bila kujali itikadi za vyama! Na serikali ipate kodi. Najua wewe Chadema mimi CCM, ila maendeleo yetu hayapaswi kuwa based on vyama.