Ziara ya Rais Magufuli Zanzibar na mikwara aliyopiga, imeleta hali ya utulivu visiwani humo

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wanabodi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli alifanya ziara ya siku mbili visiwani Zanzibar kati ya Septemba 3 na 4, 2016. Septemba 3 alikuwa kwenye uwanja wa Gombani ya Kale Pemba na Septemba 4 alikuwa Unguja.

Katika Ziara hiyo, Rais Magufuli alikumbusha umuhimu wa Watanzania kudumisha amani ya nchi tuliyonayo ili nchi isonge mbele. Alikemea vikali vitendo vya baadhi ya watu kutumia mwanya wa uhuru wa kujieleza kuleta maneno ya uchochezi kwa lengo la kulifarakanisha taifa.

Kikubwa ambacho ndicho kiini cha mada hii ni ile mikwara aliyopiga. Alimwambia Dr Shein ampe majina yote ya wanaovuruga amani ya nchi ambao ameshindwa kuwashughulikia na yeye atachukua dakika tano tu kuwasambaratisha. Hakika maneno yale yalikuwa makali sana kutamkwa na Mkuu wa Nchi. Wengi walijitokeza na kupaza sauti eti Rais ni dikteta.

Hata hivyo, niwakumbushe ndugu zangu kuwa Rais Magufuli amejitolea kuwa mtumbua majipu. Jipu halitumbuliwi kwa kubembelezana. Jipu linahitaji sura ngumu na ujasiri wa hali ya juu. Katika hili Rais Magufuli amefanikiwa. Tangu achimbe mkwara ule, ni zaidi ya Mwezi sasa hatujasikia matukio ya kipuuzi yakifanyika kule Zanzibar. Utulivu umetamalaki.

Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wangu. Nakuomba uendelee kufanya hivyo katika maeneo mengine.
 
Huku bara nako wakaahirisha Ukuta mara mbili, kila wakikumbuka ile kauli, " Sijaribiwi"
 
Hebu ngoja..
Kijana unamaanisha mkuu wa nchi huwa anapiga mikwara tu??
 
Wanabodi.
Kikubwa ambacho ndicho kiini cha mada hii ni ile mikwara aliyopiga. Alimwambia Dr Shein ampe majina yote ya wanaovuruga amani ya nchi ambao ameshindwa kuwashughulikia na yeye atachukua dakika tano tu kuwasambaratisha. Hakika maneno yale yalikuwa makali sana kutamkwa na Mkuu wa Nchi. Wengi walijitokeza na kupaza sauti eti Rais ni dikteta.
Baada ya miaka miwili lugha yetu itakuwa moja watanzania, tutapiga hatua.
 
Ha ha ha ha Magu bana

Tutarajie mengi tu yatokayo kinywani kwa Mh.Magu
 
Wanabodi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli alifanya ziara ya siku mbili visiwani Zanzibar kati ya Septemba 3 na 4, 2016. Septemba 3 alikuwa kwenye uwanja wa Gombani ya Kale Pemba na Septemba 4 alikuwa Unguja.

Katika Ziara hiyo, Rais Magufuli alikumbusha umuhimu wa Watanzania kudumisha amani ya nchi tuliyonayo ili nchi isonge mbele. Alikemea vikali vitendo vya baadhi ya watu kutumia mwanya wa uhuru wa kujieleza kuleta maneno ya uchochezi kwa lengo la kulifarakanisha taifa.

Kikubwa ambacho ndicho kiini cha mada hii ni ile mikwara aliyopiga. Alimwambia Dr Shein ampe majina yote ya wanaovuruga amani ya nchi ambao ameshindwa kuwashughulikia na yeye atachukua dakika tano tu kuwasambaratisha. Hakika maneno yale yalikuwa makali sana kutamkwa na Mkuu wa Nchi. Wengi walijitokeza na kupaza sauti eti Rais ni dikteta.

Hata hivyo, niwakumbushe ndugu zangu kuwa Rais Magufuli amejitolea kuwa mtumbua majipu. Jipu halitumbuliwi kwa kubembelezana. Jipu linahitaji sura ngumu na ujasiri wa hali ya juu. Katika hili Rais Magufuli amefanikiwa. Tangu achimbe mkwara ule, ni zaidi ya Mwezi sasa hatujasikia matukio ya kipuuzi yakifanyika kule Zanzibar. Utulivu umetamalaki.

Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wangu. Nakuomba uendelee kufanya hivyo katika maeneo mengine.
Hongera pia ziwaendee wananchi wa znz kwa kumuelewa rais na kudumisha amani kwa maendeleo yao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom