Ziara ya Rais Lazarus Chakwera wa Malawi itufunze mazuri ya Malawi

mwimbule

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
585
288
ZIARA YA RAISI LAZARUS Mc CARTHY CHAKWERA WA MALAWI ITUFUNZE MAZURI YA MALAWI

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kupitia Mkurugenzi wake Gerson Msigwa, ililipoti kuhusu ziara ya Kiserikali ya siku tatu kuanzia tarehe 7th Octoba 2020 ya Mheshimiwa Rais LAZARUS MC CARTHY CHAKWERA katika Nchi ya TANZANIA, kupitia Mwaliko wa Rais JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI.

Na tumejulishwa kwamba Rais CHAKWERA akiwa nchini atafanya ziara ya kitaifa ya siku tatu. Pia Mheshimiwa Magufuli atafanya mazungumzo na mgeni wake. Na Tunafahamu kwamba Rais CHAKWERA atahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na Rais MAGUFULI .

Hatujambiwa kama Rais CHAKWERA atafanya mazungumzo na Wamalawi wanaoishi na kufanya biashara nchini Tanzania hasa hasa katika mji wa Dar Es Salaam. Na mwisho hatujaambiwa pia kama mazungumzo yao yatahusu pia Mgogoro wa siku nyingi kati ya nchi hizi mbili kuhusu Mpaka katika Ziwa Nyasa au Ziwa Malawi kama wao Malawi wanavyoliita. Pia hatujaambiwa pia kama Viongozi hawa watajadili Mradi pendwa shiriki wanchi Mbili MTWARA CORRIDOR PROJECT.

Hata hivyo Makala hii haitajikita sana katika masuala hayo mtambuka. Ziara hii ya Rais CHAKWERA ni muhimu sana kwa sisi wadau wa Tanzania tunaofuatilia sana ziara za Viongozi wa nje nchini Tanzania.

CHAKWERA ni rais Mpya wa Sita nchini Malawi aliyeapishwa Tarehe 28 JUNI 2020 baada ya kumshinda Rais PROFESSA ARTHUR PETER MUTHARIKA baada ya marudio ya Uchaguzi Mkuu yaliyotokana na Amri ya Mahakama Kuu ya Malawi. Kwaiyo ni mtazamo wangu kwamba ziara hii pengine ina umuhimu mkubwa sana kwa Tanzania kwa mujibu wa wadau wa wizara ya mambo ya nje ndio maana CHAKWERA amefanya ziara ya kwanza nchini Tanzania.

Ni muhimu pia tukafahamu kwamba Tanzania imekuwa ikifaidika sana na Malawi , kwa sababu Malawi kama nchi isiyo na Bandari Bahari, imekuwa ikipitisha mizigo yake mingi kama siyo yote kupitia Bandari ya Dar Es Salaam. Kwaiyo kuna mchango wa Malawi kwa uchumi wa Tanzania. Pia ikumbukwe kamba watanzania wengi wamekuwa wakifanya biashara nchini Malawi.

Katika muktadha huu ni muhimu kufahamu kwamba Historia ya Malawi ni ndefu kama ilivyo ya Tanzania, nchi ya Malawi kama ilivyo Tanzania ilitawaliwa na Uingereza kuanzia Miaka ya 1883, kwa Miaka hiyo MALAWI ilijulikana kama BRITISH CENTRAL AFRICA PROTECTORATE na baadaye mwaka 1907 jina likabadilishwa na kuwa NYASALAND. Na mwaka 1953 NYASALAND Iliungana na NORTHERN RHODESIA (ZAMBIA) na SOUTHERN RHODESIA (ZIMBWABWE) Kuunda SHIRIKISHO LA RHODESIA NA NYASALAND. Shirikisho hilo lilifutwa Rasmi 31, Desemba 1963. Kama ilivyokuwa kwa Tanzania, Malawi ilipata Uhuru kutoka kwa Uingereza tarehe 6 Julai 1964 chini ya Uongozi wa JOHN HASTING KAMUZU BANDA. Na baada ya uhuru watawala wakabadili jina la nchi na kuwa MALAWI.

Na kuanzia mwaka 1966, Baadaye Malawi ilibadili katiba na kuwa JAMHURI YA MALAWI. MALAWI nayo ilifuta vyama vingi na kuwa nchi ya chama kimoja cha MALAWI CONGRESS PARTY (MCP) Kama ilivyofanya Tanzania Mwaka 1964.

Mambo muhimu ambayo tunaweza kujifunza kama taifa kupitia ziara ya Rais CHAKWERA nchini TANZANIA kwa kipindi hiki ambacho kwangu ni muafaka sana na muhimu sana hasa kwa sababu TANZANIA, ipo katika harakati za kampeni kali kuhusu UCHAGUZI Mkuu unaofanyika tarehe 28 October 2020.

MOJA YA MAMBO AMBAYO NCHI YETU INAWEZA KUJIFUNZA WAKATI HUU RAISI WA MALAWI ANAPOTEMBELEA TANZANIA,

Ni Upana wa demokrasia ya Malawi kwa mujibu wa katiba yao. Ikumbukwe kwamba Malawi Mwaka Jana 2019 ilifanya uchaguzi wa sita tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. Tanzania twaweza kujifunza upana wa demokrsia ya Malawi kwenye uchaguzi kwa namna unavyoshirikisha wagombea binafsi au huru kwa nafasi zote kwa mujibu wa katiba yao. Ikumbukwe kwamba Malawi mgombea anaweza kugombea cheo chochote bila kuwa na chama au kulazimishwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Yaani katiba ya Malawi hailazimishi mgombea kuwa na chama cha siasa. Hii ni tofauti na Tanzania yetu ambayo mgombea lazima apitie chama cha siasa. Hii sera ya Malawi imepanua wigo wa watu wengi kuweza kushiriki katika siasa za nchi yao ya Malawi. Kwa mwaka 2019 nchini Malawi MR REVEREND HADWICK KALIYA alikuwa MGOMBEA BINAFSI wa Uraisi, pia kulikuwa na wagombea huru/binafsi mamia katika nafasi za ubunge.

Jambo lingine ambalo linaonyesha namna wenzetu wa MALAWI walivyo na upana wa demokrasia na ambao kama taifa tunaweza kujifunza, ni kwamba katika uchaguzi wa Mwaka 2019, aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Malawi DR. SAULOS CLAUS CHILIMA naye aligombea URAIS akipambana na ARTHUR PETER MUTHARIKA wa DPP Kupitia chama cha UTM.

Pia ATUPELE MULUZI aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Arthur Peter Mutharika, katika Wizara ya Nishati na Madini naye aligombea Uraisi dhidi ya Boss wake Arthur Peter Mutharika kupitia chama cha UNITED DEMOCRATIC FRONT (UDF). Hii yote inaonyesha namna wenzetu wa Malawi walivyo na upana wa demokrasia ukilinganisha na kwetu. Lakini pia jambo zuri lingine ni kwamba MALAWI iliendelea kutekeleza demokrasia ya uhakika chini ya Raisi mwanademokrasia Arthur Peter Mutharika Professa Nguli wa Sheria ,na Wakili aliyehudumu na kuishi nchini Tanzania Miaka ya 1976 akiwa na namba 339, na pia kufanya kazi Marekani kwa zaidi ya Miaka 30.

Kwaiyo jambo la Msingi sana katika ziara hii ya nchini Tanzania ya Raisi wa Malawi hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu wa Tanzania ni umuhimu wa Wagombea binafsi (INDEPENDENT CANDIDATE) katika sheria zetu, katiba na sheria za uchaguzi,

Pia Malawi Vyama vinaruhusiwa kufanya shughuli zao wakati wowote, yaani mikutano na maandamano ya amani ,kwa ajili ya kutafuta wanachama wapya , na kupinga sera zisizofaa.

Pia jambo lingine ni kwamba Matokea ya uchaguzi wa Uraisi nchini Malawi yanapingwa mahakamani. Wakati kwetu Tanzania ni kinyume chake yaani hairuhusiwi kuyahoji matokeo ya Uraisi Mahakamani. Na kumekuwa na uhuru mkubwa sana wa Mahakama nchini Malawi hasa katika vipindi vya uchaguzi. Na Moja ya kesi zilizoamuliwa na Mahakama ya MALAWI kuhusu Uchaguzi ilikuwa ni KESI YA MAPITIO NAMBA 38 YA MWAKA 2014 KATI YA NCHI YA MALAWI NA TUME YA UCHAGUZI, FRIDAY ANDERSON JUMBE, AMOSI MAILOSI, DAVE KAZINJA, ambayo iliamua kwamba Tume ya uchaguzi haiwezi kuongeza siku za kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Raisi. Ni lazima matokeo yatangazwe ndani ya siku nane kama inavyotakiwa na sheria za uchaguzi za nchini Malawi.

Pia Katika kesi ya kikatiba No 1 ya 2019, Kati ya DR. SAULOS KLAUS CHILIMA, DR. LAZARUS MC CARTHY CHAKWERA AND PROFESSOR ARTHUR PETER MUTHARIKA, ELECTORAL COMMISSION, Mahakama Kuu chini ya Maaji watano ilifuta na kubatilisha matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Malawi na yaliyomweka Madarakani Rais Professor Arthur Peter Mutharika.

Jambo lingine tunaloweza kujifunza kutoka Malawi ni kwamba TUME YA UCHAGUZI ina uhuru na huru katika kusimamia uchaguzi kutokana na muundo wake. Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wa Malawi wanateuliwa kutokana na mapendekezo na ushirikishwaji wa Vyama vyote vya siasa vyenye wabunge bungeni. Na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi anatoka miongoni wa Majaji wa Mahakama ya juu ya Malawi ambaye anateuliwa na Tume ya Utumishi ya Mahakama.Hii ni kwa mujibu wa ibara ya 75 ya katiba ya Malawi ya Mwaka 1994. Wakati kwetu Hapa Tanzania ni tofauti,Tume inatokana na uteuzi wa Raisi ambaye pia ni mgombea wa Uraisi.

Kuweza kuona uhuru wa Tume ya Uchaguzi Malawi, Uchaguzi wa Mwaka 2014, Tangazo la Rais JOYCE HILDA MTILA BANDA la kufuta uchaguzi wote wa Urais kwa kigezo kwamba uchaguzi uliharibiwa na kwamba itabidi uchaguzi ufanyike Upya,lilipingwa vikali na TUME YA UCHAGUZI YA MALAWI chini ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa wakati huo hayati JAJI MAXON MBENDERA na wadau wengine,Pia Mahakama ya MALAWI baada ya kesi kupelekwa na wadau iliamua kwamba Raisi hana uwezo wa kufuta uchaguzi wa MALAWI.

MALAWI walipata Katiba mpya ya MALAWI ya Mwaka 1994 ambayo iliimarisha Demokrasia ya kweli, Utawala bora, Haki za binadamu, Tume huru ya uchaguzi, na kwa ukweli kabisa ilileta ushindani wa kweli kwa wananchi kwa kuruhusu wagombea binafsi katika nafasi zote za uongozi ndani ya MALAWI. CCM mjifunze pia hili la umuhimu wa katiba mpya,

Na Malawi imekuwa ya amani na demokrasia pamoja na kubadili vyama mara nne katika kuongoza serikali ya Malawi. Maisha yataendelea, Hata chama kingine kikishinda katika nchi.

Chama ca MCP chama kikongwe KIMERUDI madarakani tena nchini Malawi Mwaka huu tarehe 28 Juni 2020 baada ya kukaa benchi kwa miak 26 kuanzia mwaka 1994 ambapo Ndugu BAKILI MULUZI kiongozi wa chama cha UNITED DEMOCRATIC FRONT (UDF) alichaguliwa kuwa raisi baada ya kumwagusha NGWAZI DR.HASTING KAMUZU BANDA (OMUYAYA), Ambaye alikuwa ametawala MALAWI KWA MIKA 30, KUTOKA TAREHE 6 JULAI 1966 HADI 24 MEI 1994. Kwaiyo CCM wasiogope inawezekana,

Uchaguzi huu nchini Tanzania Mwaka 2020, tuhimize demokrasia ni muhimu mazuri ya MALAWI kuyachukua na kuyaweka kwenye sheria zetu ili kuimarisha demokrasia ya kweli nchini Tanzania.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki Watanzania. Tuchukue mazuri ya Malawi, Mabaya tuwaachie
 
Wapo vizuri kwenye demokrasia, mahakama, police,tume zao sio Mali binafsi ya mtawala. Thus huwezi kuta polisi wa Malawi wanaegemea chama tawala wakati wa uchaguzi.

Pili jeshi ni Mali ya wananchi na linaapa kulinda nchi na sio kulinda chama.
 
Mataga wanapitia huu uzi kimya kimya
Mimi ni Mataga, nilichojifunza ni kwamba wananchi wa Malawi wamegundua kwamba MCP chama kikongwe ndiyo bora huko kote walikuwa wanajaribu wamepoteza muda ndiyo maana wameamua kukirudisha chama cha awali madarakani.

Tanzania tusidhani kwamba wapinzani wana jipya au wanaweza kuleta maendeleo sana sana wanaweza kuturudisha nyuma tulikotoka. Maadamu CCM imeonyesha mwelekeo wa maendeleo tuendelee kukiamini. Tusije tukathubutu kupoteza muda eti kuwajaribu wapinzani.
 
ZIARA YA RAISI LAZARUS Mc CARTHY CHAKWERA WA MALAWI ITUFUNZE MAZURI YA MALAWI

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kupitia Mkurugenzi wake Gerson Msigwa, ililipoti kuhusu ziara ya Kiserikali ya siku tatu kuanzia tarehe 7th Octoba 2020 ya Mheshimiwa Rais LAZARUS MC CARTHY CHAKWERA katika Nchi ya TANZANIA, kupitia Mwaliko wa Rais JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI...
Umeandika vizuri ila umesahau kimoja mwanafunzi humfuata mwalimu.
Hivyo hapo Lazarus ndio alikuja jazwa ujinga na jiwe ,subiri arudi Malawi utaona wasiojulikana wanaanza kuingia hapo
 
Wapo vizuri kwenye demokrasia, mahakama, police,tume zao sio Mali binafsi ya mtawala. Thus huwezi kuta polisi wa Malawi wanaegemea chama tawala wakati wa uchaguzi.

Pili jeshi ni Mali ya wananchi na linaapa kulinda nchi na sio kulinda chama.
Asante , hayo ndiyo ya kijifunza na kuyafuata hapa kwetu
 
Mimi ni Mataga, nilichojifunza ni kwamba wananchi wa Malawi wamegundua kwamba MCP chama kikongwe ndiyo bora huko kote walikuwa wanajaribu wamepoteza muda ndiyo maana wameamua kukirudisha chama cha awali madarakani.

Tanzania tusidhani kwamba wapinzani wana jipya au wanaweza kuleta maendeleo sana sana wanaweza kuturudisha nyuma tulikotoka. Maadamu CCM imeonyesha mwelekeo wa maendeleo tuendelee kukiamini. Tusije tukathubutu kupoteza muda eti kuwajaribu wapinzani.
La msingi ni wananchi kuwa na Mamlaka ya mwisho ya kuamua,, Tuwape demokrasia , Tume huru, na Katiba bora,,
Na CCM wasiopgope kuondolewa madarakani,, kwani wananchi hao hao wanaweza kuwarudisha,, wasiseme tu Kanu na Unip kutorejeshwa ,
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom