Ziara ya pinda shinyanga aibu nyingine mpya hizi hapa

chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,941
900
Pamoja na kutumia magari zaidi ya 50 kwenye msafara wake hapa kero za ujio wa mkuu huyu hazikuishia kwa kuwasweka rumande watu walioktaa kutoa mbuzi kama zawadi kwake mengine ni haya :

1. Alipokea mkufu wa dhahabu 20gm kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya kahama. Mkufu huo ulikuwa ukabidhiwe kwa mke wake lakini hakuwepo kwani alienda na wake wa vingozi wengine kumtembelea Mama Nyerere. Mkufu huo ambao uliandaliwa kama kiziba macho ili asihoji watendaji wake ulipelekwa na wasindikizaji wake aliokuja nao

2. Hakupewa fursa ya kuhutubia jimbo la kahama kwa Mh.lembeli badala yake alihutubia Jimbo la Mh.Maige ambapo aliacha nyukano mkali na kuongezea mpasuko zaidi kwa wabunge hawa wanaotoka waliya moja

3. Fisi walitumiwa kwenye burudani zilizoandaliwa kwa ajili yake lakini waliotumia fisi hao hawakukamatwa bali watu wengine
wakikutwa na fisi hapa shinyanga hunyanyaswa na wakati mwengine huwawa kwa kuitwa wachawi


 
Hilo lipelekwa bungeni bi mdogo wa pinda ataizima hiyo hoja, hayo twayasikia na tusiyoyasikia yaelekea ni aibu tu. Je nje ya nchi wanakoenda kuombaomba? Hivi jamani kumkalimu mtu ni lazima?
 
Mzeee wa meeeeeeeeee ana penda kuzibwa mdomo sana.
 
Mzeee wa meeeeeeeeee ana penda zawadi sana.

Watu walio wengi wanadhani pinda ni mpole kumbe sivyo,ni kutokana na vizawadi anavyo pewa vinamfanya afyate mkia.

Kweli unafikiri pinda anashindwa kuwaadabisha wa chini yake kama ana vyofanya mwakyembe?

Vizawadi ndio chanzo cha ukimya wa pinda.
Pinda umesahau hili neno?
"Nikichukua rushwa nife"
 
Mzee wa nini? wa meeeeee??? hahahaaaaa ngoja nimalizie mnazi wangu niende zangu job mie
 
Hilo lipelekwa bungeni bi mdogo wa pinda ataizima hiyo hoja, hayo twayasikia na tusiyoyasikia yaelekea ni aibu tu. Je nje ya nchi wanakoenda kuombaomba? Hivi jamani kumkalimu mtu ni lazima?

Nadhani huko ya nchi ni aibu zaidi ,hoteli wanazolala zina siri kubwa
 
kwahiyo wanakijiji walilazmishwa kutoa mee(mbuzi) wao kama zawadi? Na waliokataa waliswekwa rumande!
 
Basi wangemmilikisha mgodi. Kuna migodi mingi Shinyanga! Mmh Mtoto wa Mkulima hapa umeumbuka, mbuzi? mbuzi? Na waliokosa mbuzi ndani? Aibu! Hebu muipate hii, hata JK aliwahi kupewa ng'ombe Ukara Kisiwani, Ukerewe, shughuli ilikuwa kumsafirisha hadi Dar! Hivi kwa nini viongozi wa Afrika wanateswa sana na kula????
 
wangempa zawadi ya fisi anaendeleze shughuli zake za jadi....... si kulazmisha wanakijiji maskini watoe vitowewo vyao(mbuz) kumzawadia
 
Back
Top Bottom