Ziara ya Mnyika yatiririsha maji jimboni Ubungo

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,414
Wanabodi,
Kwa muda mrefu tumeshuhudia mashambulizi ya wahafidhina dhidi ya mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John John Mnyika.

Thread nyingi zilikuwa za "kimkakati wa kipropaganda" kwani zilishindwa kutoa ushahidi kama tatizo la maji linahusu jimbo zima la Ubungo, au ni asilimia ngapi ya wakazi wa jimbo hilo wana matatizo ya maji. Uhalisia ni kuwa zaidi ya nusu ya maeneo ya jimbo hilo huwa yanapata maji walau mara tatu kwa juma.

Kiukweli yapo maeneo kadhaa katika jimbo hilo (sio yote) ambayo yamekuwa na matatizo ya uhaba wa maji kwa muda mrefu, hasa wakati jimbo hilo linaongozwa na mbunge kwa tiketi ya ccm. Hata baada ya "mradi wa wachina" bado kuna maeneo ambayo bado yalikuwa na tatizo hilo, safari hii sababu kubwa zikiwa ni za kiufundi, uharibifu na uhujumu wa miundombinu ya maji. Sababu nyingine zaweza kuwa ni kumhujumu kwa makusudi mbunge Mnyika kunakofanywa na wahusika na wadau wa maji.

Naelewa jitihada kubwa zilizofanywa na zinazofanywa na Mh. Mnyika katika kutatua kero za wapiga kura wake hasa tatizo la maji.
Mh. Mnyika amekuwa akichukua maoni ya wapiga kura wake kupitia makongamano, mikutano ya hadhara, mitandao ya kijamii n.k. Vilevile amekuwa akitoa mara kwa mara mrejesho wa kazi zake kupitia njia hizo tajwa. Kwa mtu ambaye amekuwa akimfuatilia vizuri hawezi kupinga kuwa Mh. Mnyika amepiga hatua kubwa sana katika kuhakikisha kero za wapiga kura wake zinatatuliwa.

Wiki iliyopita mbunge Mnyika alianza ziara jimboni kwake katika ule mwendelezo wa kuwasiliana na wananchi wake.
Tangu alipotangaza kuanza ziara, maeneo karibu yote ya jimbo lake yamekuwa yakipata maji kwa kiwango kikubwa.
Hata yale maeneo ambayo hayajawahi kuona tone la maji ya bomba yamepata maji kuanzia jumamosi mfululizo hadi leo hii. Na haya ndio matunda ya mbunge anayejua nini anapaswa kufanya kwa wale anaowawakilisha.

Hongera Mh. John Mnyika.
Wale waliokuwa wanakubeza nadhani sasa aibu imewakumba.
 
sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,538
9,433
Hujasoma kwenye Raia Mwema Mangula amewaambia wanachama wa ccm wayashambulie majimbo yanayoongozwa na wapinzani lakini yanayoongozwa na wabunge wa ccm wayaache ili wabunge waweze kuitekeleza ilani ya ccm..!
 
JituParaTupu

Member
Nov 20, 2008
89
9
Mimi si mwanachama wa chama chochote...ila namkubali sana Mh. Mnyika kwa jinsi anavyochapa kazi. Keep it up Mnyika...nakukubali sana kwa utendaji wako wa kazi pamoja na hoja zako bungeni....
 
Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,414
Mimi si mwanachama wa chama chochote...ila namkubali sana Mh. Mnyika kwa jinsi anavyochapa kazi. Keep it up Mnyika...nakukubali sana kwa utendaji wako wa kazi pamoja na hoja zako bungeni....
Kuna watu wanapiga propaganda za kipuuzi lakini kwenye ukweli uongo hujitenga, na macho pia yanaona. Mnyika hana muda wa blahblah zaidi ya kupiga kazi.
 
usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
331
Hujasoma kwenye Raia Mwema Mangula amewaambia wanachama wa ccm wayashambulie majimbo yanayoongozwa na wapinzani lakini yanayoongozwa na wabunge wa ccm wayaache ili wabunge waweze kuitekeleza ilani ya ccm..!

ko ni mkakati maalumu wa kuhujumu miundombinu ili ionekane mbunge hafanyi kazi! Kwa akili ya wanaccm wa leo wala sishangai mtu kukata bomba la maji yanayoelekea kwake. Wana akili ya ajabu ajabu. Ndo maana uwt wamebakia kuwa makahaba wa viongozi badala ya kuwa watoa wazo mbadala, uvccm wamebakia wapanga mbinu za kigaidi badala ya wachapa kazi, jumuia ya wazazi ndo kabisa hata shule wameshindwa kuziendesha.
 
Kiwera Mikaeli

Senior Member
Aug 11, 2012
121
39
ko ni mkakati maalumu wa kuhujumu miundombinu ili ionekane mbunge hafanyi kazi! Kwa akili ya wanaccm wa leo wala sishangai mtu kukata bomba la maji yanayoelekea kwake. Wana akili ya ajabu ajabu. Ndo maana uwt wamebakia kuwa makahaba wa viongozi badala ya kuwa watoa wazo mbadala, uvccm wamebakia wapanga mbinu za kigaidi badala ya wachapa kazi, jumuia ya wazazi ndo kabisa hata shule wameshindwa kuziendesha.

kama walivyofanya eneo la goba! Washenzi kabisa
 
Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,328
954
Tabu ccm hawataki kuona mwananchi wa hali ya chini akinufaka au akipata unafuu wa maisha
 
Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
2,730
491
majimbo ya ubungo yapo mawili hapa dar? maji ni tatizo kubwa ila kama mnyika ameleta maji hapa jf sawa,lakini ubungo hatuna maji
 
Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
539
Imekuwaje Mnyika kutembelea ubungo, maji kutoka mabomani? uhusiano uko wapi?
Kama kuna habari tuambie
Tunajua Mnyika ni mchapa kazi ila hili la maji, kwa hadidhi hii fupi sioni kama kuna uhusiano,
Kama unataka ueleweke, sema eneo, na alichofanya maji yakatoka. sio kutembea. Au ilimaanisha kuwa waliogopa wakafungua maji? Ni wapi hapo? inawezekana basi hapo mahali maji yalikuwa yamefungwa na jirani tu.
 
mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,448
630
Kwanini kulimulika jimbo la Mnyika, ilhali kuna Segerea, Temeke, Ilala, na Kigamboni mbona maji hayapatikani ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom