Ziara ya Mjukuu wa Malkia wa Uingereza nchini, (Prince William)

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
Mjukuu wa Malkia wa Uingereza “Prince” William anatarajiwa kufanya ziara nchini kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2018.

Ziara hiyo inakuja kufuatia maombi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipofanya naye mazungumzo wakati wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Uingereza mwezi Aprili 2018.

“Prince” William atakapowasili nchini pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Aidha, atatembelea kikosi cha Maji cha Jeshi la Polisi; Bandari ya Dar es Salaam; Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House); Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.

“Prince” William ni mmoja wa wanaharakati duniani wanaopinga biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori na Uingereza imekuwa ikisifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na vitendo vya ujangili.

“Prince” William ataondoka nchini tarehe 29 Septemba 2018 kuelekea nchini Kenya.

-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
 
Prince” William ataondoka nchini tarehe 29 Septemba 2018 kuelekea nchini Kenya.

Tuwe precise kwenye mazungumzo naye, ndimi zikiteleza tu ndivyo reflexion atakayo waambia majirani
 
Hizi ndio habari anbazo chadema hawataki kusikia
Mfalme mtarajiwa anakuja kwenye nchi adhim ya Tanzania,kama kungekua na ukikwaji wa haki za binadamu na uminyaji wa demokrasia huyo mfalme asingekanyaga
 
Mr :Ebo Alisha wahi imba kuwa alisimamisha Bus ili aulize ni Saa ngapi?
Hakika alikuwa anafikisha ujumbe wa watu kama nyie
Si ajabu na shule ulienda ?
Si ajabu unamiliki na familia?
Si ajabu ni mshauri wa familia?
Si ajabu kuna watu wanakutegemea?

Jiulize Anaye kutegemea yupoje?
Alafu mwisho wa siku tutegemee nchi ya viwanda?
 
Wacha ngonjera wewe,si hua mna kipengele mnakiita 'for the english audience' si ni maalum watu kama hao waupate upupu wenu ili watuwekee vikwazo?
 
Wacha ngonjera wewe,si hua mna kipengele mnakiita 'for the english audience' si ni maalum watu kama hao waupate upupu wenu ili watuwekee vikwazo?
Mpo wengi mkilala alafu ukiwa fukara unasema Jirani yangu Ndiye anayeniloga ananionea Wivu,Soma Uzi vizuri unahusu nini? Alafu umecomment nini?
 
Mkuki kwa nguruwe!
Hizi ndio habari anbazo chadema hawataki kusikia
Mfalme mtarajiwa anakuja kwenye nchi adhim ya Tanzania,kama kungekua na ukikwaji wa haki za binadamu na uminyaji wa demokrasia huyo mfalme asingekanyaga
 
Ujio huu uatatusaidia kuitangaza Tanzania 🇹🇿. Vyombo vyote vya habari vitataka coverage
 
Ali Kiba bado ni balozi na wenzake ule ubalozi ambao humu nakumbuka kusoma michuano ya utimu.. kama bado natumaini watampa nafasi awemo katika haya pia.
 
Back
Top Bottom