Ziara ya Mhe Pinda atoa matumainu kwa wananchi wa Kiteto Manyara

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Ziara ya mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda, Mkoani Manyara, imeingia siku ya pili.

Mhe Pinda alipokelewa Kijiji cha Dosidosi Kiteto jana na kuongea na wananchi akiwataka kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Magufuli katika kuwatumikia wananchi.

Akiwa Kiteto alikutana na
viongozi wa CCM na kuongea nao huku akipokea kero na changamoto zinazowakabili.

Baadaye alifika shule ya Sekondari Engusero kuzindua bweni la wasichana lililojengwa na halmadhauri ya Wilaya

Bweni hilo linauwezo wa kuhifadhi wanafunzi 84 ambalo limegharimu shilingi mil 86.4

Mhe Pinda aliwataka wanafunzi hao kusoma Kwa bidii na kuheshimu walimu ambao kazi yao ni kuelimisha.

Baadaye Mhe Pinda alienda kata ya Matui ambapo hapo alikutana na viongozi wa CCM na kuongea na kuhusu changamoto zinazowakabili.

Akiwa Kibaya Mhe Pinda alielezwa mengi ikiwemo migogoro ya ardhi na namna ya kuitatua, kuwa na Mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Kwa ujumla wanachama hao walizungumza kwa ujumla juu ya sekta ya Afya, elimu na Barabara kuwa bado Serikali inatakiwa kumaliza kabisa

Katika hatua hiyo Mhe Pinda pamoja na kuelezwa changamoto hizo pia aliwataka wananchi kuwa makini katika maendeleo yako

Mwisho


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikua waziri mkuu alishindwa kuleta matumaini, leo hii akiwa mjumbe wa kamati za chama ndio analeta matumaini mapya? Watu wengine sijui nani kawaharibu vichwa vyao.
 
Back
Top Bottom