Jana tarehe 09/01/2017 taifa limeshuhudia kitendo ambacho naweza kukiita ni “Cha ajabu” lakini pia ni “Cha Ujasiri Mkubwa”, kwa Mh Eddo Lowassa kuamua kwenda kumtembelea Rais Magufuli Ikulu na kumpa pongezi zake kwa utendaji wake uliotukuka ikiwa ni pamoja na kufikisha ushauri wake. Nimekiita ni kitendo cha ajabu na ujasiri kwa sababu sote tu mashahidi wa kauli ambazo siku za hivi karibuni wapinzani, Lowassa akiwa mmoja wao wamekuwa wakizitoa juu ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Kuna usemi kwamba “Ukweli Humuweka Mtu Huru”. Kwa kweli kama hujazoeshwa kuongea uongo katika maisha yako, siku ukifanya hivyo dhamiri yako lazima itakusuta na utakosa amani kabisa muda wote. Hicho ndicho kilichomtokea Eddo. Hakuweza kuvumilia kitendo cha upinzani kusema uongo muda wote dhidi ya serikali na huku hali halisi ikionekana kuwa mambo yapo kinyume kabisa na jinsi wanavyotaka kuwaaminisha wananchi. Hatimaye ameamua kujitoa muhanga na kusema kweli ya iliyopo moyoni mwake bila kujali gharama ya uamuzi wake huo kisiasa.
Kitendo hicho ni funzo kwa wanasiasa wengine kwa maana kwamba, si vema kupotosha hata ukweli ili tu upate mtaji kisiasa. Penye ukweli lazima tusema kama ulivyo na si kuugeuza ili uonekane kuwa ni uongo. Lakini pia ni nafasi kwa wanasiasa na hasa wa upinzani kutambua kwamba Rais yupo tayari kukutana kwa mashauriano yanayowasilishwa katika namna ya kuheshimiana na si matusi na kejeli kibao kama ambazo tumekuwa tukizishuhudia toka kwa wanasiasa walio wengi. Tujipe muda wa kujadiliana kwa staha masuala muhimu kwa maslahi mapana ya nchi yetu badala ya kuishi kwa vijembe na kejeli.
Hongera sana Eddo ukweli umekuweka huru, na umeandika historia nyingine.
Benmpo