Ziara ya Lowassa Ikulu ni funzo kubwa kwa wanasiasa nchini

Benmpo

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
450
500
Jana tarehe 09/01/2017 taifa limeshuhudia kitendo ambacho naweza kukiita ni “Cha ajabu” lakini pia ni “Cha Ujasiri Mkubwa”, kwa Mh Eddo Lowassa kuamua kwenda kumtembelea Rais Magufuli Ikulu na kumpa pongezi zake kwa utendaji wake uliotukuka ikiwa ni pamoja na kufikisha ushauri wake. Nimekiita ni kitendo cha ajabu na ujasiri kwa sababu sote tu mashahidi wa kauli ambazo siku za hivi karibuni wapinzani, Lowassa akiwa mmoja wao wamekuwa wakizitoa juu ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Kuna usemi kwamba “Ukweli Humuweka Mtu Huru”. Kwa kweli kama hujazoeshwa kuongea uongo katika maisha yako, siku ukifanya hivyo dhamiri yako lazima itakusuta na utakosa amani kabisa muda wote. Hicho ndicho kilichomtokea Eddo. Hakuweza kuvumilia kitendo cha upinzani kusema uongo muda wote dhidi ya serikali na huku hali halisi ikionekana kuwa mambo yapo kinyume kabisa na jinsi wanavyotaka kuwaaminisha wananchi. Hatimaye ameamua kujitoa muhanga na kusema kweli ya iliyopo moyoni mwake bila kujali gharama ya uamuzi wake huo kisiasa.

Kitendo hicho ni funzo kwa wanasiasa wengine kwa maana kwamba, si vema kupotosha hata ukweli ili tu upate mtaji kisiasa. Penye ukweli lazima tusema kama ulivyo na si kuugeuza ili uonekane kuwa ni uongo. Lakini pia ni nafasi kwa wanasiasa na hasa wa upinzani kutambua kwamba Rais yupo tayari kukutana kwa mashauriano yanayowasilishwa katika namna ya kuheshimiana na si matusi na kejeli kibao kama ambazo tumekuwa tukizishuhudia toka kwa wanasiasa walio wengi. Tujipe muda wa kujadiliana kwa staha masuala muhimu kwa maslahi mapana ya nchi yetu badala ya kuishi kwa vijembe na kejeli.

Hongera sana Eddo ukweli umekuweka huru, na umeandika historia nyingine.

Benmpo
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
9,430
2,000

si mnasema lowasa ni fisadi mkamuundia na mahakama ya mafisadi, kwa hiyo tuhuma za ufisadi zimeyeyuka kwa kuwa kamsifia mfalme wenu.
 
Vumilika

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
1,254
2,000
Huenda hata mtu mzima amekwenda kuwaombea vijana msamaha kwa mtu mzima mwenzake, ili maisha yasonge mbele lazima kuwe na hali ya kuelewana hususan kunako maendeleo ya taifa.
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,165
2,000
si mnasema lowasa ni fisadi mkamuundia na mahakama ya mafisadi, kwa hiyo tuhuma za ufisadi zimeyeyuka kwa kuwa kamsifia mfalme wenu.
Hoja ya Ufisadi wa Lowassa ilianza kushikiwa bango na Chadema mpaka wakamuweka kwenye 'ubao wa matangazo' au unajisahaulisha?

Chadema ni public bath kwa Yeyote aliechafuka ni hela yako tu kulipia Bafu
 
Benmpo

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
450
500
Hoja ya Ufisadi wa Lowassa ilianza kushikiwa bango na Chadema mpaka wakamuweka kwenye 'ubao wa matangazo' au unajisahaulisha?

Chadema ni public bath kwa Yeyote aliechafuka ni hela yako tu kulipia Bafu

Hiki huwa naona wanajisahaulisha kabisa, maana hadi wakafikia hatua ya kubadili gia angani na kumpa fisadi nafasi ya kupeperusha bendera inasikitisha sana
 
MwanaPekee

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
382
500
Kuna watu wa upinzani wameanza kuitazama hii issue kama vile Eddo alienda CDM strategically ili kuuvuruga UKAWA. So long as mission imekuwa accomplished basi alikwenda kutoa report kwa mkuu ya uharibifu ndani ya UKAWA. Upinzani endeleeni tu kumpenda huyo malaika wenu, na ikiwezekana 2020 apeperushe bendera tena ili tushuhudie mafuriko yale ya 2015
 
Lowassa amewavuruga sana, wanashindwa tu kuanza tena kumwita fisadi kwa sababu wamemsafisha muda si mrefu baada ya kumchamfua kwa muda mrefu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom