Se-ronga
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 650
- 909
Wakubwa kwa wadogo hongereni kwa majukumu ya kulijenga Taifa letu yenye kauli mbiu ya "hapa kazi"
Kama mjuavyo Kiongozi wetu mkuu wa nchi Mh.JPM tangu aingie Ikulu mwishoni mwa mwaka jana bado hado hajafanya ziara rasmi nje ya nchi.
Na hii inawezekana ni kutokana na majukumu mazito ya Kitaifa yaliyomtinga,na hasa suala la uteuzi wa mawaziri,makatibu wakuu,makamishna na hata watumishi wengine wa umma ambao lazima wale kiapo mbele yake.
Kwa kiongozi Mkuu wa nchi kama JPM ziara za nje ni muhimu kwani zinatoa nafasi ya kujenga urafiki kati ya nchi na nchi lakini pia kujifunza mambo mbalimbali yanaweza kusaidia maendeleo ya Taifa lake.
Kwa mantiki hiyo naamini Mh.Rais akishapunguza majukumu yake ya kitaifa basi atapata nafasi ya kufanya ziara nje ya nchi.Swali kubwa ni kuwa ni nchi gani ambayo itapata bahati ya kwanza kutembelewa na Rais ambaye anaonrkana kukonga nyayo za walimwengu hasa wasiopenda rushwa na ufisadi
Binafsi naamini kuwa ziara ya kwanza ya Mh.Rais lazima itakuwa ndani ya bara la Afrika ili kuhamasisha na kuunga mkono juhudi za mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ndani ya bara hili changa linaloendelea kuchechemea
Kwa kuzongatia uzito wa hoja hapo juu moja kati ya nchi tatu zifuatazo zinaweza kupata bahati ya kwanza ya kutembelewa na Mh.Rais tangu ashike nchi.Hii ni kutokana na kuwa marais wa nchi hizi wana misimamo inayoshabihiana na JPM:
1: Ghana- chini ya Rais John Mahama
2: Nigeria-Rais Muhammadu Buhari
3: Rwanda-Rais Paul Kagame
"Hapa kazi tu"