Ziara ya kutembelea Taasisi ya Bodi ya mapato Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
735
476
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim amefanya Ziara ya Kutembelea Taasisi ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB). Mhe. Jamal ametembelea Taasisi yake ya ZRB ili kujionea hali halisi ya mfumo wa VFMS unavyofanya kazi ya kukusanya Mapato ya Serikali.

Aidha, Mheshimiwa Jamal ameelezwa kuwa mfumo huo wa VFMS tayari umeshafungwa kwa walipa kodi 600 kuanzia July hadi sasa na Mfumo umeweza kukusanya Mapato ya Serikali jumla ya shilingi Bilioni 31.

Mhe. Jamal alielezwa kuwa jumla ya hoteli 480 tayari zimeshafungiwa na wanatumia mfumo huo wa VFMS. Mfumo huo unapatikana kwa kupitia online kwa njia ya laptop, simu za mkononi na vifaa maalum ambavyo vya kufanyia mauzo( POS).

Mhe. Jamal aliwaagiza ZRB Kuweza kuwaunganisha wafanyabiashara ambao wanao mifumo yao kuwa Mifumo hiyo iwe inafanya kazi kwa kuunganishwa moja kwa moja na mifumo ya VFMS kwa walipa kodi wote mfano walipa kodi wa mahoteli.

Mheshimiwa Jamal katika Ziara yake hiyo alipata fursa ya kutembelea hoteli ya Madina til - al bahar ili kujionea Mfumo unavyofanya kazi. Mhe. Jamal alifika katika hoteli hiyo sehemu ya mapokezi na kuona mfumo wa VFMS unavyofanya kazi kwa kutumia laptop na alitembelea katika Mgahawa wa hoteli hiyo na kuona mgahawa huo unatumia mfumo wa (POS).

Mhe. Jamal aliwaagiza ZRB kufanya haraka kuwafungia wafanyabiashara wote ili waweze kutumia mfumo wa VFMS ili wafanyabiashara hao waweze kutoa risiti za kielektroniki na kuweza kuhifadhi taarifa za biashara zao kwa njia ya kielektroniki. Pia alisisitiza kuwa wapo wafanyabiashara bado hawalipi kodi hususan wafanyabiashara waliopo maeneo ya nje ya mji, lakini ukiona biashara wanazozifanya ni sawa na mfanyabiashara wa mjini.

Waziri Jamali amesema ZRB wanatakiwa wafanye bidii kubwa ya kuwafikia walipa kodi wote ili waweze kulipa kodi na Serikali iweze kupata Mapato yake.

Mheshimiwa katika Ziara yake hiyo alitembelea duka la Saleh decoration liliopo Miembeni.
 
Back
Top Bottom