Ziara ya Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania gereza la Arusha

Kama sijui kusoma nimewezaje kuandika haya hadi ukauliza hivyo? Wahenga wanasema swali la kipumbavu hujibiwa kipumbavu. Hivyo, usishangae mimi kukushangaa mwanangu.
Sasa kama unajua kusoma basi una tatizo la kuelewa, umeambiwa katibu wa shura ya maimamu wewe unauliza anatembelea magereza kama nani?
 
njaa na ujinga vinawasumbua. Hawa hawana tofauti na matapili kama Gwajima, Mazinge, Lusekelo, Mwakasenge na wezi wengine wanaotumia dini kuishi kutokana na kutokuwa na sifa elimu wala utundu wa kuishi kihalali.

Na mwisho wao huwa mbaya tu na kudhalilika sana
 
Shura ya Maimamu Tanzania

TAARIFA YA MASHEIKH WA GEREZA LA ARUSHA LEO 11.10.2021.

Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda amefanya ziara leo kuwajua hali Masheikh waliopo katika Gereza Kuu la Arusha Kisongo.

Masheikh hao na waumini wao wapatao 61, walikamatwa mwaka 2014, na kupewa kesi za Ugaidi.

Kati yao watatu (3), tayari wamefariki dunia wakiwa gerezani na kubaki 58.

Waliofariki wameacha mayatima 18, na wajane 5.

Wanashikiliwa kwa zaidi ya miaka minane huku Serikali ikidai bado inatafuta ushahidi.

Miezi kadhaa iliyopita Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambae pia ni Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hasaan aliagiza kesi zilizokosa ushahidi kama hizo zifutwe ili watu wapate haki yao ya huru.

Hata hivyo agizo hilo limekuwa kama halikubaliki kwa watendaji wake.

Miongoni mwa mahabusu wanaogusa hisia za watu ni Yasini Mohammed aliyekamatwa (2014), akiwa mtoto mwenye umri wa miaka 15, na kupewa Ugaidi. Yasini anakulia gerezani na kukosa haki ya Elimu na malezi ya Baba na Mama.

Mwingine ni muadhini wa Msikiti aliyekamatwa mwaka huo akiwa na umri wa miaka 62, ambaye sasa yuko taabani kwa afya na uzee gerezani.

Katika ziara hiyo Sheikh Ponda amewafikishia Mahabusu hao salamu za Mawakili kuwa kesi zao zatakapoanza kusikikizwa watakwenda Arusha kuwatetea.

Mawakili hao ni wale waliowatetea Masheikh wa Uamsho na kushinda kesi 14, za Ugaidi kati ya 25, walizofunguliwa.

Sheikh Ponda pia amekutana na Familia za Mahabusu hao na kufanya nao mazungumzo.

Tayari amekwishafanya ziara katika Magereza ya Dar, es Salaam, Tanga na sasa Arusha. Ziara zinazofuata ni za Morogoro, Mwanza na Mtwara ambako pia mamia ya Waislamu baado wanashikiliwa.

Sheikh Ponda aliondoka Jijini Dar es Salaam jana 15.10.2021, saa 1:45 na kupokewa na viongozi wa Arusha katika uwanja wa Kilimanjaro International Air Port, saa 03:05, asubuhi.

Ibrahim Z. Mkondo
Msemaji Shura ya Maimamu
0713118812.
Hawa Magaidi toka wamekamatwa Arusha hakuna tena Mabomu wala hatari ya Usalama. Tunaomba tu wahukumiwe ili wasipoteze muda Mahabusu
 
Ukisikia Kuna sheikh Yuko ndani kwa makosa ya kigaidi ujue huyo sio wa bakwata.
Viongozi wote wa serikali na mashirika yake lazima Ni wa mrengo wa ubwabwa yaani bakwata.
Ukitaka kuikwaza serikali jiondoe bakwata. (Kwa waislamu)
Bila Bakwata Waislamu ni vurugu, Bila Bakwata hapa itakuwa vurugu za kugombea misikiti kila siku
 
Hawana lao tena
Utawala huu hautaki wanafiki na watu wa ndio bwana
Kina hadi mpaka kanzu zitapauka
Huwa nikiona shekh au kiongozi wowote wa kidini anawapigia debe maccm bs najua huyo anamatatizo au ni jizi lililo jificha kwenye dini kutapeli watu
 
Huwa nikiona shekh au kiongozi wowote wa kidini anawapigia debe maccm bs najua huyo anamatatizo au ni jizi lililo jificha kwenye dini kutapeli watu

Mbona wizi wao wengi unajulikana tu
Watu wanagawana mpaka misaada ya nyama toka Saudia na vurugu unategemea nini hapo

Mpaka Tende wanaiba na kuiomba serikali eti iondoe kodi
Yaani baba zima linaomba kodi iondolewe ya Tende wakati wamepewa bure

Mpaka kanzu za mitumba za misaada wanauza hawa watu
Njaa zao wamejificha sehemu ya Ibada
 
njaa na ujinga vinawasumbua. Hawa hawana tofauti na matapili kama Gwajima, Mazinge, Lusekelo, Mwakasenge na wezi wengine wanaotumia dini kuishi kutokana na kutokuwa na sifa elimu wala utundu wa kuishi kihalali.
Yani mwakasege umemuweka kwenye hao wajinga
 
Sasa kama unajua kusoma basi una tatizo la kuelewa, umeambiwa katibu wa shura ya maimamu wewe unauliza anatembelea magereza kama nani?
wewe ndo tatizo lwani yeye ni mtumishi wa umma au huko ni msikitini watakwenda wangapi tusichanganye dini na siasa jamani tunaanza kufufua udini taratibu.
 
wewe ndo tatizo lwani yeye ni mtumishi wa umma au huko ni msikitini watakwenda wangapi tusichanganye dini na siasa jamani tunaanza kufufua udini taratibu.
Hapo siasa iko wapi mkuu? Wamefungwa maimamu na masheikh aliyewatembelea ni sheikh pia ni kiongozi tatizo liko wapi?
 
Hapo siasa iko wapi mkuu? Wamefungwa maimamu na masheikh aliyewatembelea ni sheikh pia ni kiongozi tatizo liko wapi?
Aende kama ndugu lakini siyo kama katibu. Kama tutaruhusu upuuzi huu ni wangapi watakwenda na kweli kutakuwa na magereza au vurugu? Kesho atataka kutembelea mahakama kwa sababu mashehe wanahukumiwa huko. Kesho kutwa atataka aende ikulu kwa vile majaji wanateuliwa huko.
 
Back
Top Bottom