Ziara ya Kagera, Magufuli usiende pekee tu Wasaidizi wako wanakokupangia kwenda

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,822
35,817
Ziara ya Kagera, Magufuli chagua pia mwenyewe ambako ungetaka kwenda, yaoonesha wasaidizi wako hawapendi uje huku makwetu Rusahunga - Ngara kwani bila shaka utawatumbua tu.

Mh. Rais ilikuwa faraja kuwa utakuwa na ziara ya siku 4 mkoani Kagera. Hata hivyo ikashangaza kuwa katika ziara hii hutafika kabisa Biharamulo wala Ngara. Mheshimiwa wanaotengeneza wapi uende na wapi upite labda kama wana ajenda zao za siri. Vinginevyo mheshimiwa hebu jiongeze mwenyewe uwatake sasa ufike pia Ngara kupitia hii barabara ya Rusahunga - Nyakahura - Nyabugombe - hadi Benaco: katika njia hii kuu itokayo Dar hadi kwenye mpaka wa Tanzania na Burundi na pia Rwanda.

Ni wazi kuwa kama ungeweza kufanya safari ya kushtukiza kama mambo yako ya siku zile za mwanzo yaliyvokuwa; ukapita mwenyewe na huku pasipo na kuwaandaa wasaidizi wako hawa, majipu yahusianayo na barabara hii wala yasingehitji kutumbuliwa na mtalaamu mtumbuaji kama wewe bali yangetumbuka yenyewe tu.

Kwa jinsi ilivyo, huku sasa siyo wla kuiva tu kwa majipu bali yamepitiliza mno mheshimiwa hadi yakatepeta kwa na kujipongeza kuwa bingwa mtumbua majipu kazi hiyo labda sasa kaachana nayo kabisa! Ni mwenye uhakika kuwa wewe huna tena haja ya utumbuaji anayeweza achia barabara ikaporomoka kiasi hiki na bado akawa na jeuri ya kukujenga kiwanja cha ndege cha sh. bilioni 39.5 tena jimboni kwako.

Hivi sasa mvua zina nyesha hali barabara ni as good as haipo. Haihitaji uchambuzi mkubwa kufahamu kuwa washauri na wasaidizi wako hawa wanaokuvisha vilemba vya ukoka kwa jenzi za viwanja vya ndege tena kwa kuanzia Chatto hawakutakii mema. Funga safari sasa uelekee huku Ngara Ngara ujionee mwenyewe. Yataka umakini mheshimiwa kwani vinginevyo usije fanyiwa kama yule spika waliyemvisha kilemba cha ukoka na kumjengea ofisi ya Spika jimboni kwake kana kwamba atakuwa spika wa kudumu au kama vile maspika watakuwa wakitokea jimbo hilo siku zote au kuwa hata Ndugai leo atahamia huko kufanyia kazi za uspika anapokuwa likizo badala ya Kongwa.

Jiongeze mheshimiwa vinginevyo hawa jamaa wanaokueleza kuwa kila kitu ni shwari watakuwa wanapalilia chuki kwa niaba yako toka kwa wapiga kura wako 2020 pasipo na wewe mwenyewe kujua.
 
Watu siku hizi wanaloga Mkulu asitembelee mikoa na wilaya zao.... maana hawajui lipi litajiri kwenye ziara yake.
 
Hawa wakurugenzi wa Bk manispaa na halmashauri ndo wamekuwa kikwazo cha maendeleo hapo Bukoba na haswa wanastahili kutumbuliwa hasa hasa huyu wa manispaa ni jipu. Mh. rais msamehe lakini muondoe huyo hakufai na ameshindwa kabisa kuisaidia manispaa, barabara zenyewe zinadhihirisha jamaa asivyo na uwezo wa kukusaidia
 
Kipindi cha nyuma kuna waziri aliwaambia wakitaka Lami waharishe njia nzima kisha watapata Lami.Alikuwa ni Waziri wa ujenzi enzi za kikwete.Nimemsahahu jina.
 
Maneno mengiiii shida yenyewe ni ubovu wa barabara na kumhitaji Rais afike Benako kulamba asali na Ngara kuchukua Maharage.
Kwann usii sumarize tu mkuu maana wengi wetu tu wavivu wa kusoma habari ndefu utazan makala.

Mkuu wewe ni wale waratibu wa safari zake? Au wewe ni mnufaika ikiwa mheshimiwa hata zungukia huku? Mbona povu jingi? Au unatambua hautanusurika akifika huku msikopenda afike?

Au wewe ni wale wanaompamba huyu mheshimiwa kuwa mnampenda sana kwa kumjengea airport Chatto hali ati wale wanamkosoa ati ni maadui zake?

Andiko halikuwa kwa ajili yako. Umeona refu? Unashadadia vipi andiko ambalo si lako? Si uandike lako lililofupi kwa ajili yako na wenzako mlio wavivu?

Endeleeni kumdanganya lakini wapiga kura wanaona wala 2020 si mbali kama mnavyodhani.
 
Acha kuleta utetezi usiohitajika. Wakati mwingine heshimu ukosoaji. Unaandika meeengi lakini point hazizidi mbili halafu unasubiria pongezi. Fanya kazi yako halafu acha wasomaji wengine ama wakupogeze au kukukosoa.
 
Mh. Rais ilikuwa faraja kuwa utakuwa na ziara ya siku 4 mkoani Kagera. Hata hivyo ikashangaza kuwa katika ziara hii hutafika kabisa Biharamulo wala Ngara. Mheshimiwa wanaotengeneza wapi uende na wapi upite labda kama wana ajenda zao za siri. Vinginevyo mheshimiwa hebu jiongeze mwenyewe uwatake sasa ufike pia Ngara kupitia hii barabara ya Rusahunga - Nyakahura - Nyabugombe - hadi Benaco: katika njia hii kuu itokayo Dar hadi kwenye mpaka wa Tanzania na Burundi na pia Rwanda.
Magufuli anajua hali ya barabara zote kuu,hata umuamshe saa 6 usiku.
Hiyo barabara aliizungumzia wakati alipokua Tabora na kigoma mwezi wa jana
 
Magufuli anajua hali ya barabara zote kuu,hata umuamshe saa 6 usiku.
Hiyo barabara aliizungumzia wakati alipokua Tabora na kigoma mwezi wa jana

Mkuu nitashukuru kujua aliizungumzia vipi barabara hii inayo nihusu sana kuelekea huku makwetu. Ukweli usiopingika -- barabara hii inaweza kuwa si kitu kwa mtu aliye kwenye flyovers kwani mwenye shibe katu hawezi juwa kuna wenye njaa pia.
 
Hawa wakurugenzi wa Bk manispaa na halmashauri ndo wamekuwa kikwazo cha maendeleo hapo Bukoba na haswa wanastahili kutumbuliwa hasa hasa huyu wa manispaa ni jipu. Mh. rais msamehe lakini muondoe huyo hakufai na ameshindwa kabisa kuisaidia manispaa, barabara zenyewe zinadhihirisha jamaa asivyo na uwezo wa kukusaidia
Inaonekana maneno aliyaona
 
Kipindi cha nyuma kuna waziri aliwaambia wakitaka Lami waharishe njia nzima kisha watapata Lami.Alikuwa ni Waziri wa ujenzi enzi za kikwete.Nimemsahahu jina.

Atakuwa huyu huyu.

Incredible!
 
Mkuu umeipigia kelele sana barabara hiyo, ipo siku kilio chako kitasikilizwa.Kuwa na subira
 
Back
Top Bottom