Ziara ya CHADEMA mikoa ya kusini yawatesa wabunge wa CCM

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
ziara iliyofanywa na CHADEMA katika mikoa ya lindi na mtwara imegeuka kuwa mwiba mkali kwa wabunge wa ccm ambao majimbo yao yalipitiwa na kimbunga cha ziara hiyo yenye lengo la kuleta mabadiliko katika mikoa ya kusini. Wabunge wawili wa mkoa wa mtwara Abdallah Mtutula na Jerome Dismas Bwanaausi wameshambulia vikali hatua ya chadema kutembelea kwenye majimbo yao na kuwashambulia. Aidha wabunge hao wamesema hatua ya wabunge wa chadema kwenda kwenye majimbo yao na "kueneza chuki" na kuwashambulia wao inaweza kuleta machafuko na kutoweka kwa amani.

kuna msemo unasema kwamba ukirusha jiwe gizani ukasikia mtu anasema aiiii ujuwe limempata. Hivyo chadema wanapaswa kukaza mwendo kwani wabunge wa ccm katika mikoa ya kusini wameshaingiwa na hofu ya kuondolewa madarakani mwaka 2015.
 
Very good Chadema majimbo si mali ya mtu hayo ni mawazo mgando .Kazeni buti wapeni Elimu ya Uraia
 
Lakini kiukweli sio fair kwenda hadi kusini
brother unaniangusha chadema imesajiliwa tanzania ina uhuru kufanya ziara popote ndani ya mipaka ya tz iki ni chama cha kitaifa mkuu ujui kuna offisi za chadema kule? kulalamika hakuwasaidii wawapelekee maendeleo kimbunga kitawaponya wamekaa kimya muda mrefu mjengoni uoni kuwa m4c imewasaidia walau imewashinikiza wasimame mjengoni na waongee?
 
Hawataki waliolala usingizi waamshwe! kama wamewaletea maendeleo ya kweli wapiga kura wao hawana sababu ya kuwa na wasiwasi!
 
Mbunge wangu Jerome Dismas Bwanaausi kafunguka alikuwa kashona mdomo sijui kaondolea nyuzi hospital gani wakati madaktari wamegoma
 
Hiyo hapo imekaa vyema sana watu wansema kama unaishi kwenye nyumba ya vioo usiandishe vita ya mawe, sasa watapoteana hadi kitakapoelewekaaa.
 
Yaani hii kweli ni silly season, magamba wanaenda kulia bungeni!

Ok ccm kila mara wanakuja na tafsiri potofu na mfu....kuwaeleza wananchi kuwa serikali yao imewatelekeza, imewanyonya sana na kuwadhulumu kimfumo na kimkakati, na wakati huo huo kuwafunza elimu ya urai ili wazijue haki zao na wajibu wao inaitwa "chuki"

So according to CCM SILLY ni tusi. DHAIFU ni tusi. ELIMU YA URAIA ni chuki.....gimme a break fella!
 
ziara iliyofanywa na CHADEMA katika mikoa ya lindi na mtwara imegeuka kuwa mwiba mkali kwa wabunge wa ccm ambao majimbo yao yalipitiwa na kimbunga cha ziara hiyo yenye lengo la kuleta mabadiliko katika mikoa ya kusini. Wabunge wawili wa mkoa wa mtwara Abdallah Mtutula na Jerome Dismas Bwanaausi wameshambulia vikali hatua ya chadema kutembelea kwenye majimbo yao na kuwashambulia. Aidha wabunge hao wamesema hatua ya wabunge wa chadema kwenda kwenye majimbo yao na "kueneza chuki" na kuwashambulia wao inaweza kuleta machafuko na kutoweka kwa amani.

kuna msemo unasema kwamba ukirusha jiwe gizani ukasikia mtu anasema aiiii ujuwe limempata. Hivyo chadema wanapaswa kukaza mwendo kwani wabunge wa ccm katika mikoa ya kusini wameshaingiwa na hofu ya kuondolewa madarakani mwaka 2015.

nimeisikia hiyo kitu. jamaa wanatafuta umaarufu kwenye TV wale. sisi ndo wapigakura wao. wanapashwa kujuwa kama tunataka mabadiliko, siyo kujibaraguza ili ugongewe meza bungeni.
 
Back
Top Bottom