Ziara na Mapokezi ya Mama Salma, anastahili?

Big Dady

Member
Nov 10, 2009
59
2
Mke wa Rais, mama Salma amekuwa akifanya ziara katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kupokelewa na viongozi wakiwemo wakuu wa mikoa. Je, ana cheo gani kitaifa hadi kupokelewa rasmi hivyo. Je, kuwa fisrt lady ni cheo kinachotambulika na katiba yetu. Au ni mradi wa kutangaza WAMA na wakati huo huo kumwandalia mzee njia ya oktoba mwaka huu. Lakini je ni halali yeye kufanya ziara kama kiongozi wa serikali.
 
Yeye ni mama mkuu wa taifa.
Hiko ni cheo tosha.
She is the second most powerfull personin tz.
Why not????????
 
Lakini The Boss hujanjibu kisawaswa, katiba inamruhusu, isije ikawa ni kutumia feza za walipakodi kwa maslahi binafsi na kifamilia. Mbona wake wa marais wengine hatuoni wakifanya hivyo?
 
lakini the boss hujanjibu kisawaswa, katiba inamruhusu, isije ikawa ni kutumia feza za walipakodi kwa maslahi binafsi na kifamilia. Mbona wake wa marais wengine hatuoni wakifanya hivyo?

yapo mambo huitaji katiba kuyafanya..
Katiba yenyewe ina loopholes kibao..

Kwa mfano vipo vifungu vya sheria zetu
vinasema kwa mujibu wa tamaduni na mila zetu....

Sasa mila na tamaduni zetu ni zipi?
Juzi jacob zuma kaoa mke wa tatu,
na sherehe za harusi na gharama za wake zake
zinalipiwa na kodi ya wananchi....

Na anachokifanya ni kuendeleza mila na
dessturi tu za kwao.
 
Mke wa Rais, mama Salma amekuwa akifanya ziara katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kupokelewa na viongozi wakiwemo wakuu wa mikoa. Je, ana cheo gani kitaifa hadi kupokelewa rasmi hivyo. Je, kuwa fisrt lady ni cheo kinachotambulika na katiba yetu. Au ni mradi wa kutangaza WAMA na wakati huo huo kumwandalia mzee njia ya oktoba mwaka huu. Lakini je ni halali yeye kufanya ziara kama kiongozi wa serikali.

Sio halali ni uvunjaji wa sheria. Mke wa rais hatambuliki kikatiba na hana cheo chochote serikalini.
 
Afadhali na huyu siyo fisadi kale anna fisadi kalipokelewa sana.
 
Yeye ni mama mkuu wa taifa.
Hiko ni cheo tosha.
She is the second most powerfull personin tz.
Why not????????
Kuna title ya Mama Mkuu wa Taifa????
Du..ndo naisikia leo hiyo,any way Cheo cha first lady hakitambuliki kikatiba,so hata zile Gharama za kubembea Jamaica nasikia Muungwana alitoa mfukoni mwake,kama hakutoa bai ana deni.
 
KAMA wewe hutaki kumpokea usiende kumpokea.......wanaohitaji kwenda kumpokea wacha waende....wana sababu zao za kwenda kama wewe ulivyo na sababu za kutokwenda.....!
by the way wewe unataka yeye atambuliwe na katiba? kwani mimi katiba inanitambua kwa cheo?
 
JK angefanya kama mwenzake Museveni. Akampa uwaziri huyu mke wake. Matatizo yaliyoko sehemu kama Tarime yanahitaji kuundiwa wizara sio mkoa wa kipolisi!! Mama Salma awe waziri wa Tarime kama mwenzake Janet alivyo waziri wa Karamoja.
 
Wanampokea kwa kuwa wana nidhamu ya woga na si vinginevyo. Katiba haiko wazi kuhusiana na First Lady hivyo viongozi ngazi mbali mbali wanafanya hivyo kutokana na mazoea na kuhofia kupokwa madaraka yao.
 
Lakini The Boss hujanjibu kisawaswa, katiba inamruhusu, isije ikawa ni kutumia feza za walipakodi kwa maslahi binafsi na kifamilia. Mbona wake wa marais wengine hatuoni wakifanya hivyo?
Yaani first Lady anapewa heshima zote, lazima apewe ulinzi mkali na mapokezi yote kama first lady.
 
This is hardly about ulinzi.

Lazima mkuu wa mkoa na wapambe wengine wote waache kazi zao? Mimi naona si first lady tu, hata rais mwenyewe akifika sehemu si lazima viongozi wote wamzonge wakati kazi zinalala.

So medieval!
 
Tatizo la hawa viongozi wetu sijui wakuu wa wilaya na mikoa wengi hawana kazi au hawajui wafanye nini ndo matokeo yake hayo.
 
JK angefanya kama mwenzake Museveni. Akampa uwaziri huyu mke wake. Matatizo yaliyoko sehemu kama Tarime yanahitaji kuundiwa wizara sio mkoa wa kipolisi!! Mama Salma awe waziri wa Tarime kama mwenzake Janet alivyo waziri wa Karamoja.

Ni kweli mkuu,tena awe waziri wa elimu,kwa sababu alikuwa mwalimu bila shaka matataizo ya walimu atayatatua kirahisi.
 
JK angefanya kama mwenzake Museveni. Akampa uwaziri huyu mke wake. Matatizo yaliyoko sehemu kama Tarime yanahitaji kuundiwa wizara sio mkoa wa kipolisi!! Mama Salma awe waziri wa Tarime kama mwenzake Janet alivyo waziri wa Karamoja.

haha uwaziri mkuu bila skuli inakuja kweli?
 
Back
Top Bottom