ZIARA: Mawaziri na manaibu wote..waenda mikoani kuisafisha serikali

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,517
8,582
Katika hali inayoonesha kutaharuki na kuyumba kwa serikali mawaziri na manaibu waziri wote wakiongozwa na waziri mkuu..kesho jumatatu tar 1/10 wanaaza ziara nchi nzima kujaribu kuzima nguvu ya umma iliyoanza kujengeka miongoni mwa wanachi na kurudisha heshima ya serikali inayoporomoka kwa kasi..

Juzi mawaziri na manaibu wote walikuwa katika kikao cha kuwekana sawa.. pamoja na kujengana kimorali tayari kwa ziara hiyo ya mikoani, ziara hii inatokana na yafuatayo.. na hizo zikiwa hadidu za rejea ambazo mawaziri wana kazi ya kuzisafisha.

1. Kuchafuliwa kwa serikali na vyama vya upinzani.

2. Kutoa ufafanuzi kwa kashfa mbalimbali zinazoikabili serikali..

3. Kuwaelewesha wananchi maana ya sera na kauli mbui za serikali "maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana" na "ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA".. hasa wakikazania mafanikio ya serikali ya awamu ya nne hadi leo.. hasa kwenye nyanja za kiuchumi , miundombinu na ilimu..

4. Mafanikio ya ziara za rais na za viongozi kwa ujumla..

5. Kuzima dalili za nguvu za umma [hasa kuzomewa kwa viongozi na kurushiwa mawe ..i.e pale mkuu wa wilaya Kinondoni alipovurumshwa kwa mawe].., au pale rais aliposimamishwa na wananchi kule Buzwagi.. na kufikia kuthubutu kumzodoa na kumgunia rais.. amabalo si jambo la kawaida.... ambazo ni dalili za kuashiria kuyumbisha usalama wa taifa.

Kufanyika kwa ziara hizi hasa katika kipindi hichi kwa uchambuzi wangu binafsi na kwa kuzingatia hadidu za rejea kunaweza kuisaidia serikali kujisafisha ila zaidi zitawasha moto mkubwa zaidi wa serikali kukataliwa.. kwani umahiri wa mawaziri wengi katika kujenga hoja unatia shaka.. uwezekano wa kutuliza hasira za wananchi ni mdogo sana....

Njia pekee ya serikali kujisafisha ni kwa kufanya maendeleo na kuchukua hatua dhidi ya ufisadi....

Baadhi ya watafiti wa kisiasa wanaamini kuwa umaarufu wa mheshimiwa UMESHUKA HADI KUFIKIA ASILIMIA 50% TOKA 80% WALIZORIPOTI REDET..MWAKA 2005..NA KWELI RAIS AKASHINDA KWA 80.2%...KATIKA SIKU ZA KARIBUNI WATU WALIO KARIBU NA PROF MKANDARA WANASEMA AMEKATAA KUFANYA UTAFITI KUTHIBITISHA UMAARUFU KUVUKA CHINI YA 50% KWA MADAI KUWA HALI YA KISIASA KWA SASA NI BIASED KUWEZA KUTOA MAJIBU MUAFAKA..
 
MVUMILIVU HAWA wanaenda kama viongozi wa serikali ingawa huko kufagia wanakotaka kwenda kufanya kutaisaidia serikali ya ccm...sasa huu ndio wakati makada wapinzani nao wangewafuata hao mawaziri huko huko ili huu moto wa uwana mapinduzi na kuzinduliwa kwa wadanganyika kusipoe..mawaziri wenyewe kina ghasia,batilda,chenge at al sioni mwenye uwezo wa kuwashawishi na kuwatuliza wananchi wenye hasira hapo..watavuna aibu asilani..

ni kupoteza pesa tu..magari ..wasaidizi ..posho hadi kwa viongozi wa mikoa na wilaya watakao shiriki hizi ziara...hapa hata miaka miwili bado ..hadi ifike mitano itakuwaje?? i hope wananchi watakuwa wamekata tamaa...
 
Katika hali inayoonesha kutaharuki na kuyumba kwa serikali mawaziri na manaibu waziri wote wakiongozwa na waziri mkuu..kesho kumatatu tar 31/9 wanaaza ziara nchi nzima kujaribu kuzima nguvu ya umma iliyoanza kujengeka miongoni mwa wanachi na kurudisha heshima ya serikali inayoporomoka kwa kasi..

..

Mwezi wa tisa una siku 30, na katika kalenda inayotambuliwa na SMT na SMZ hakuna siku ya kumatatu
 
mawaziri wenyewe kina ghasia,batilda,chenge at al sioni mwenye uwezo wa kuwashawishi na kuwatuliza wananchi wenye hasira hapo..watavuna aibu asilani..

ni kupoteza pesa tu..magari ..wasaidizi ..posho hadi kwa viongozi wa mikoa na wilaya watakao shiriki hizi ziara...hapa hata miaka miwili bado ..hadi ifike mitano itakuwaje?? i hope wananchi watakuwa wamekata tamaa...

Kazi ipo kama EL kashindwa swali la mtoto wa form one hao sijui itakuwaje???
 
ZIARA:mawaziri na manaibu wote..waenda mikoani kuisafisha serikali.

1.kuchafuliwa kwa serikali navyama vyama vya upinzani.

2.kutoa ufafanuzi kwa kashfa mbali mbali zinazoikabili serikali..

Heshima mbele mkuu PM,

I mean hawa viongozi wetu wanatakiwa kujiandaa na evidence za mahakamani, ushauri wa bure tu kwao wakuu wetu,

masikini ya Mungu!
 
He Jamani

Makubwa haya. Si CCM ikiongozwa na Makamba tayari walishaanza ziara ya kuwajibu wapinzani? Basi CCM watoe tamko kuwa wameshindwa sasa majibu yanatolewa na mawaziri.

Si Kingunge alisema wanawapuuza wapinzani kwa kuzunguka kutokana na kutokuwa na kazi? Vipi leo wanazunguka kuwajibu? Na kingunge naye atakendwa kinyume na maneno yake?

Hii ni ziara ya ngapi kwa mawaziri? Si lowasa aliwaagiza wazunguke kuhamasisha ujenzi wa shule wakatumia fedha nyingi kuliko walizokusanya? Hivi wajakoma tu!

Wanazunguka kueleza mafanikio ya serikali, je wataeleza pia mapungufu ya serikali?

Hivi kwa nini wasingewatumia wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu tarafa na watendaji wa kata kufanya kazi hiyo katika maeneo yao?

Au kwa nini basi waziri wa Habari, Waziri wa Utawala bora na Waziri wa uhusiano wa jamii ndio wasiende kufanya kazi hii?

Kuwatoa mawaziri wa Maji, Elimu, Madini, Kilimo, Miundombinu nk katika mstari wao wa kazi na kuwapeleka kuwa makada wa propaganda kama Hiza na Akwilombe ndio kwenda kuhamasisha uwajibikaji?

Sasa Warioba awakemee na hawa kwa kuacha kusimamia maendeleo na kuelekea kwenye kufanya siasa za majukwaani.

Mbona tuhuma zilizotolewa zinahitaji kwanza kuzijibu kiofisi kabla ya kwenda kupayuka barabarani?

Au ndio janja yao ya kukimbia kuzijibu kiofisi?

Au wanamkimbia Kikwete kwa kila mtu kujifanya yuko busy kuranda randa mitaani?

Mpaka lini tutaendelea kuwa na mawaziri wazururaji?

Nawaza mie Asha, nipeni majibu
 
kweli ofisini hapakaliki naona kila fisadi anajidai bize ili Jk awakute kwenye pilikapili tu. hizo hela siwangechangia shule kuliko kukata walala hoi?
 
CCM they run out the breath, and this is marathon we have a long way to go. Wameshaanza kupapalika, sasa Upinzani need strategic plan ambayo ni strong and creative. Dr Slaa need a political adviser(Guru) who will advice him not to cool things down, but to hit more facts issues.

Upinzani have to be careful, CCM are looking for the weakness, and if they will find it, they will press it hard and hard and turn the battle of Baghadad to Upinzani.

Dr slaa need to come down, and he need to make sure Mrema keep his mouth shut, its a time for only critical thinkers to open their mouth. If they will set a smart attack strategy, CCM will be out of breath and we will see the turning point soon.
 
Lipumba na Mrema wakagombee ubunge watuongezee ongezee viti upande wa upinzani maana urais kwao is a NO CHANCE hata CCM wakivurunda kiasi gani!
 
Vigogo wahaha

na Mwandishi Wetu


ULE mpango wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuwatuma viongozi wake waandamizi mikoani kwenda kukabili hali ya mambo baada ya ziara ya vyama vinne vya upinzani, unaanza rasmi leo.
Katika kukabili mapigo, CCM imeamua kuitumia bendi yake ya muziki wa dansi ya Tanzania One Theatre (TOT), ili kuvuta wananchi wengi mikoani kuhudhuria mikutano, ili waweze kupewa somo mbadala juu ya hoja zilizotolewa hivi karibuni na viongozi wa vyama vinne vya upinzani.

Kundi la makada waandamizi wa CCM, likiongozana na kundi la TOT, chini ya uongozi wa Muumini Mwinjuma, linatarajia kuondoka jijini kesho kuelekea Mbeya, kuanza kujibu hoja za wapinzani.

Makada wa CCM waliopewa jukumu la kujibu hoja za wapinzani ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM, Agrey Mwanri, Richard Tambwe Hizza, Salum Msabaha na Shaibu Akwilombe, ambao wanatarajia kuanza kuyeyusha sumu ya upinzani kuanzia kesho mkoani Mbeya, Songea na baadaye katika mikoa mingine ambayo muungano wa vyama vinne vya upinzani walipita kwa kutumia helkopta, wakimwaga sumu ambayo hadi leo inaisumbua CCM na serikali yake.

Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa, mbali ya kutumia TOT ili kukusanya watu, CCM imepanga kutumia vizuri vyombo vya habari ili kuujulisha umma kile ambacho makada wake watakizungumza na kukifanya katika ziara hizo.

“Kesho tunaondoka na TOT, tunaanzia Mbeya, kuna timu maalum kabisa iliyoteuliwa na CCM chini ya Makamba kuanza kujibu hoja ya Zitto (Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini - CHADEMA) na zingine, na tunaanzia Mbeya, Songea na katika mikoa yote ambayo wapinzani wamepita kumwaga sumu ya Zitto,” kilisema chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya CCM.

Makamba, Tambwe na Akwilombe, wamemaliza ziara ya wiki nzima mkoani Shinyanga kujaribu kujibu pamoja na mambo mengine hoja ya Zitto katika mikutano ya hadhara, ambayo inadaiwa kuwa na idadi ndogo ya wananchi, hivyo kulazimika kuitumia TOT ambayo inamilikiwa na CCM.

Wakati CCM ikijipanga kukabiliana na hoja hiyo, serikali kwa upande wake imebuni mpango kama huo, kama sehemu ya kuweka rekodi sawa, baada ya viongozi wa upinzani, kuzunguka katika mikoa kadhaa nchini kuelezea udhaifu wa serikali.

Chini ya mpango huo, mawaziri watapangwa katika mikoa kadhaa, wakizunguka na kuzungumza na wananchi na viongozi wa CCM, kuelezea kile ambacho serikali imeshakifanya hadi hivi sasa katika kutekeleza ilani ya uchaguzi iliyokiweka chama hicho madarakani kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa, katika utekelezaji wa mpango huo, timu ya mawaziri wawili na naibu waziri mmoja, leo inaanza ziara ya siku saba mkoani Arusha, kwa madhumuni hayo.

Habari zilizopatikana kutoka mkoani humo zinaeleza kuwa, timu hiyo itaongozwa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia.

Ghasia atawaongoza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe pamoja na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Habari za uhakika zinaeleza kuwa, pamoja na kuzungumza na wananchi na kuwaelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya nne, pia watasikiliza na kupokea hoja, maoni na ushauri kutoka kwa viongozi wa chama na watendaji wa serikali kuhusu utekelezaji wa bajeti ya 2007/08.

Ziara hiyo inakuja wakati nchi ikiwa imetawaliwa na hoja mbili kuu, zilizotolewa na wapinzani kuhusu undeshaji wa nchi.

Hoja zote mbili ziliibuliwa bungeni na kusambaa kwa wananchi baada ya wapinzani kutoridhishwa na yaliyotokea bungeni.

Hoja moja iliibuliwa na Zitto kupitisa hoja yake binafsi, akihoji hatua ya Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kusaini mkataba wa mradi wa mgodi wa Buzwagi akiwa nje ya nchi na kukiuka taratibu.

Zitto alihoji kwa nini waziri alifikia hatua hiyo licha ya kuwepo kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete, lililotaka kutosainiwa kwa mkataba wowote wa madini, hadi hapo serikali itakapokamilisha kazi ya kudurusu mikataba iliyopo pamoja na sheria na sera zinazotawala sekta hiyo.

Hata hivyo, mbunge huyo alisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Januari mwakani, kwa tuhuma za kusema uongo bungeni.

Hoja nyingine iliibuliwa na Dk. Willibrod Slaa (Karatu-CHADEMA), ambaye aliwasilisha kwa Spika, Samuel Sitta, nia yake ya kuleta hoja binafsi akihoji madai ya ubadhirifu Benki Kuu (BoT).

Hata hivyo, Dk. Slaa aliiondoa hoja hiyo na baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge la bajeti, vyama vinne vya upinzani; CHADEMA, TLP, NCCR-Mageruzi na CUF, vilifanya ziara katika mikoa kadhaa, kuwaelezea wananchi kuhusu masuala hayo.

Wakati wa kuhitimisha ziara hizo, katika viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam, Dk. Slaa alitaja orodha ya viongzoi kadhaa wa serikali, akiwatuhumu kwa ufisadi na kuzusha mjadala mzito ambao unaendelea hadi hii leo.

Hatua hii ya serikali inakuja wakati viongozi kadhaa, waliotajwa katika orodha ya Dk. Slaa, wakiwa wamekanusha, na wengi wao kuonyesha nia ya kwenda mahakamani kumshtaki mbunge huyo pamoja na wengine wanaomsaidia kusambaza taarifa hizo.

Inaaminika kuwa, katika ziara hizo za mawaziri, hayo ndiyo yatakayotawala ingawa ziara hizo pia zitatoa fursa kwa watendaji wa serikali katika ngazi za chini kufahamu kwa undani mipango ya serikali na utekelezaji wake.

Habari zilizopatikana toka Arusha zinaeleza kuwa, viongozi hao wataanzia ziara hiyo wilayani Longindo na watazungukia wilaya zote za mkoa huo.

Source: Tanzania Daima
 
mimi nitakuwa miongoni kufanya hivyo hapa watakaponikuta. sasa sisi wengine tusiwaachie maswali hawa watoto wa Form one na wakulima ambao hawakwenda shule tu kuuliza.

tunapaswa kujitoa kimasomaso ili tuulize na kama ikibidi , tupoint udhaifu wao ili wajue kuwa muda wa usingizi munono umeisha.
 
mimi nitakuwa miongoni kufanya hivyo hapa watakaponikuta. sasa sisi wengine tusiwaachie maswali hawa watoto wa Form one na wakulima ambao hawakwenda shule tu kuuliza.

tunapaswa kujitoa kimasomaso ili tuulize na kama ikibidi , tupoint udhaifu wao ili wajue kuwa muda wa usingizi munono umeisha.

Hilo ni wazo zuri kuwaliza maswali yanayo hitaji kufikiri siyo majibu ya kukurupuka, lakini pia moto wa kuzomewa inapo bidi pale wanapo kuja na bla bla nadhani una faa zaidi! na unapeleka ujumbe mkubwa kuliko hata maswali.

Si hilo tu, pia vyombo vya habari ambavyo viko huru! Nina maana vile ambavyo havija ingiliwa na virusi vya Rupia kuhakikisha vina ripoti uhalisi wa kinacho endelea.

Mfano kule Geita tuliambiwa Mbunge alizomewa kumbe mambo yalikuwa makubwa hadi kwa PM mwenyewe ikabidi akimbie mkutano!!

Habari kama hizo ni vyema zilipotiwe kihalisi siyo yale maigizo ya kutoa kadi kwa watu 10 vyombo vya habari vilivyo athirika vina andika kwamba wamevunja ngome ya upinzani na kurudisha wanachama 400!! Vitu kama hivi ni sumu! Inabidi kuvidhibiti katika ziara kama hizi!
 
Nashindwa kuwaelewa kabisa viongozi wa Sisiemu na 'Sirikali'. Kingunge anasema wapinzani ni wa kupuuzwa wakati Katibu mkuu Makamba na wanasisiemu waliokimbia kambi ya upinzani, mawaziri na manaibu wao wanaelekea mikoani kujisafisha, sasa tuwaeleweje hawa?
Wanaenda kusafisha nini mikoani kama kila kitu kiko sawasawa? Na sitashangaa nikisikia Makamba ama waziri kazomewa ama kurushiwa mawe jijini Mbeya ama Rukwa ama iringa. Siasa za maweneo haya wazione kama ilivyo. Wakumbuke kuwa ni huku huku ambako walianza tabia ya kuzomea wagombea wachovu mwaka 2005! Maana wabongo wa sasa shule ipo kidogo, wanaelewa nini maana ya siasa na nini maana ya usanii.
Yangu macho.
 
Ama kweli wameamua kudidimiza uchumi zaidi. Kwanza walilalamikiwa kwa kula pesa za umma kwa kupitia mlango wa nyuma (Ufisadi), sasa wanaona ni nafasi yao kula pesa hizohizo tunazopigia kelele kwa mlango wa mbele kwa kujipangia ma perDiem ya kutosha kwa ajili ya kuzunguka nchi nzima.

Ni jambo la kushangaza kusikia eti serikali nzima ( mawaziri na manaibu wao) kuongozana kwenye ziara wanayoita ya kujisafisha.
Mzunguko wa Lowassa mkoa wa mwanza umeleta matunda gani? Zaidi ya kushindwa kutoa majibu kwa maswali ya akina muarobaini na mtoto wa shule?

Si ndo huyo alishindwa kutoa majibu, amerudi jijini kukusanya majeshi ya kumsaidia kutoa majibu aliyoshindwa kutoa huko? Si alijikuta anakumbwa na fedheha ya kuzomewa na kutupiwa mawe? ingawa vyombo vya habari vilishindwa kutuhabarisha mazingira halisi ya mikutano zaidi ya kuambiwa na watu waliokuwepo kwenye mikutano.

Je, ziara hiyo yamaanisha kina karamagi wanaahirisha kwanza zoezi lao la kwenda mahakamani? au mahakama waliyosema watashitaki kwayo ndo hii wapinzani waliyoita ya umma?

Ngoja tumsikie Kingunge atakavyosema ya jinsi serikali isivyo na kazi kwa kuamua kuzunguka kama alivyowatuhumu wapinzani.

Kwa staili hii ya utenda kazi wa serikali, maisha bora tutayapata mbinguni.
 
Hoja ikiwa ya kipumbavu, halafu ikapigiwa debe na watu wenye akili, wakitarajia watu kuikubali bila kuuliza hata ukiimbia nyimbo hoja hiyo haiuziki!! (M. M. Original quote)
 
Hoja ikiwa ya kipumbavu, halafu ikapigiwa debe na watu wenye akili, wakitarajia watu kuikubali bila kuuliza hata ukiimbia nyimbo hoja hiyo haiuziki!!


Mzee MMJ,

Bravo for this quote mkuu, nafikiri ni quote inayojitosheleza kuhusiana na hii ishu kwa ujumla!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom