ZIARA: Mawaziri na manaibu wote..waenda mikoani kuisafisha serikali

..yafuatayo ni makisio ya bajeti ya ziara ya siku 14 ya mawaziri na manaibu kutangaza uzuri wa bajeti ,kujibu kashfa za wapinzani na kuelezea maisha bora..............


POSHO............................................344,000,000

Mawaziri/manaibu 60@200,000/day [14 days]

wasaidizai maalum 120@80,000[14 days]

madereva 60[14 days]


MALAZI [YA HAO HAPO JUU[AVERAGE @80,000/DAY].......300,000,000

MAFUTA

MAGARI 120[include ya wasaidizi]@100lts/day..........126,000,000

GHARAMA ZA WILAYANI..................................440,000,000

POSHO WAKUU WA WILAYA 288 [SIKU 14]@120,000

POSHO WABUNGE 288[SIKU 14]@120,000

WENYEVITI WA CCM WILAYA POSHO288@80,000

WAJUMBE WA KAMATI ZA SIASA WILAYA20/288@40,000

WATAALAMU WILAYANI KILA WILAYA 10/288@45,000


UHAMASISHAJI KILA WILAYA[NGOMA ,MC ETS]288 @1,000,000=288,000,000

VIBURUDISHO [SODA NA MAJI KWENYE MIKUTANO] KILA WILAYA @ 1,000,000............................................288,000,000

JUMLA..............................................2,070,000,000


GHARAMA ZA DHARURA...5%[DECREASE OR INCREASE]....103,500,0000


TOTAL GRAND....................................2,173,500,000/=
 
Pesa isiyo na mwenyewe jinsi inavyotumika. Lipi lilikuwa na nafuu kuunda tume ya Bunge kuchunguza mkataba wa Buzwagi au hayo mapesa wanayotapwanywa kwa kisingizio?
 
Hawa ccm sasa wanatapatapa sana huenda wameanza kusoma alama za nyakati.

Hivi isije ikawa kuwa huu ni mkakati nwa EL kuhakikisha kuwa JK akirudi hakuti mtu ofisini ili amkute yeye then ampe hopes na information ambazo hazina kichwa wala miguu.

Waende wajibu hoja na sio kupuuza mambo makubwa kama haya, ila najua kwamba hawana uwezo wa kujibu mapigo kwani hili ni pigo takatifu sana .

Sipendi ubadhirifu, haswa kutumia fedha kwenda kutetea wizi huu ni wizi mkubwa zaidi ya ule wa mwanzo.
 
hivi hao wenyeviti wa CCM na wajumbe wa wilaya siasa wanalipwa hizo pesa kutoka mfuko wa nani? ni CCM au Hazina?
 
..yafuatayo ni makisio ya bajeti ya ziara ya siku 14 ya mawaziri na manaibu kutangaza uzuri wa bajeti ,kujibu kashfa za wapinzani na kuelezea maisha bora..............


POSHO............................................344,000,000

Mawaziri/manaibu 60@200,000/day [14 days]

wasaidizai maalum 120@80,000[14 days]

madereva 60[14 days]


MALAZI [YA HAO HAPO JUU[AVERAGE @80,000/DAY].......300,000,000

MAFUTA

MAGARI 120[include ya wasaidizi]@100lts/day..........126,000,000

GHARAMA ZA WILAYANI..................................440,000,000

POSHO WAKUU WA WILAYA 288 [SIKU 14]@120,000

POSHO WABUNGE 288[SIKU 14]@120,000

WENYEVITI WA CCM WILAYA POSHO288@80,000

WAJUMBE WA KAMATI ZA SIASA WILAYA20/288@40,000

WATAALAMU WILAYANI KILA WILAYA 10/288@45,000


UHAMASISHAJI KILA WILAYA[NGOMA ,MC ETS]288 @1,000,000=288,000,000

VIBURUDISHO [SODA NA MAJI KWENYE MIKUTANO] KILA WILAYA @ 1,000,000............................................288,000,000

JUMLA..............................................2,070,000,000


GHARAMA ZA DHARURA...5%[DECREASE OR INCREASE]....103,500,0000


TOTAL GRAND....................................2,173,500,000/=


Samahani mkuu,
Hizi hesabu ni sahihi? ama za kufikiria tu kwamba huenda ndo hiyo bajeti??

Naona kiarabu arabu hapa!!
 
..rwabugiri ..hiyo ndio figure..au na wewe unataka original copy...my dear what do you expect mawaziri 60 walienda mahali hujui ni kivumbi wanahitaji wasaidizi ..magari..walinzi..malazi..ete..na wakifika mikoani unategemea wanazunguka na nani...na propaganda anafanya nani..

kwa taarifa hicho ndicho kiasi ambacho uchumi uta suffer kwa mawaziri kuwa mikoani kwa siku 14............hasara ni kubwa zaidi hapo hujaangalia miadi ya kikazi ya watu wooote wanaofutana na mawaziri na mambo yote yatakayokwama kwa wao kutokuwepo,,,upo hapo!!???
 
hivi Tanzania ni nchi maskini hilo "halina ubishi".. sasa hivo karibu bilioni mbili wanazitoa wapi?
 
Hizi bilioni mbili mbona ni kidogo sana jamani?

Kama wameweza kuiba pale BOT ,kwenye taasisis moja zaidi ya trilioni moja, je,?ukiamua kuangalia kwenye kila wizara na taasisis za serikali utajua wameiba ngapi na hivyo kutumia hizi sio nyingi.

Swali ni je?hizi pesa zilikuwa zimetengwa kwenye bajeti?

Na, je?zilitengwa kwa kazi hiyo?
 
hivi Tanzania ni nchi maskini hilo "halina ubishi".. sasa hivo karibu bilioni mbili wanazitoa wapi?


Majibu ni kuwa Tanzania sio masikini, ila wananchi wake ndio masikini kutokana na viongozi wao kutowajali.

Viongozi ni matajiri na haswa wale wa chama tawala.

Sitaki kuamini maneno haya ambayo tumelishwa eti kuwa nchi hii ni masikini, ila haya ni matokeo ya uongozi mbovu na wananchi kutokujua haki zao.
 
Hawana haja ya kuzunguka. Mwenye kashfa ajiuzulu, halafu aende mahakani kujisafisha.
Rais awe Rais kweli sio kiongozi wa genge la wezi. Ni lazima tuwe na Rais anayeheshimiwa na kuogopwa kiutendaji.

Nyerere aliwahi kusema, "kutuhumiwa tu ni doa kubwa sana, kwanini wakutuhumu wewe?"

Hakuna usafi zaidi ya kuwawajibisha wezi.
 
kwa hiyo hawa mawaziri kila baada ya kikao cha bajeti watakuwa wanatembea huko mikoani?ss hiyo bajeti wanayoipitisha huko dodoma si ndio watatumia kwenye hizi safari zao?watanzania tutakuwa masikini mpaka kiyama.
 
...2 billion kutetea ufisadi?wazee hiyo hailipi kabisa itabidi tuwang'oe tuu hawa hakuna msamaha,ila power ya media sanasana haya mablog na www kama hii ya jamboforums zimesaidia sana kuelimisha wananchi juu ya hawa mafisadi na kuweka mambo open,hope technology imefanya demokrasi iwe kubwa zaidi maana hawajui wamkamate nani maana marockets yanarushwa angle zote na anonymous...ila Msola ndio alikoma maana alichapwa bakola bila kujua zinatoka wapi.
 
Tunashindwa kudhibiti mfumuko wa bei - Dk. NaguMbona asiwaambie kuwa mfumuko wa bei unatokana na kufidia hasara , serekali ilizo pata kutona na wizi na maamuzi mabaya kama umeme wa kukodi, City Water/Bi Water, Net Group, Mashangingi, Kupeana Transfer bila kujali hali ya Uchumi, Kuweka mikataba isiyo na manufaa kama kwenye ATC, the list is long, labda Mchambuzi atanisaidia
na Stella Ibengwe, ShinyangaWAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Mary Nagu, amewataka wananchi kuelewa kuwa mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali unatokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Dk. Nagu alisema hayo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wake mkoani Shinyanga wenye lengo la kuwaeleza wakazi wa mkoa huo faida za bajeti ya serikali kwa mwaka huu.

Waziri huyo ambaye pia ni mtaalamu wa mambo ya uchumi, alifafanua kuwa, tangu Serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani, imekuwa ikitupiwa lawama kwa kushindwa kudhiti mfumuko wa bei.

Alizitaja sababu za mfumuko wa bei kuwa ni ukame ulioikumba nchi, hali iliyosababisha uzalishaji wa umeme kuwa mdogo baada ya kukauka kwa Bwawa la Mtara, jambo lililowalazimu wenye viwanda kupandisha bei ya bidhaa.

Aidha, kupanda kwa bei ya mafuta duniani ni moja ya sababu ambazo serikali haina uwezo wa kuingilia kati.

Akifafanua zaidi alisema pipa la mafuta katika soko la dunia liliuzwa dola 59 lakini kwa sasa linapatikana kwa 83.

Kwa upande mwingine, Dk. Nagu alisema serikali itatunga sheria ya kudhibiti ukiukwaji wa usafirishaji na wauzaji wa mafuta wanaopandisha bei kiholela.

Pamoja na Waziri Nagu, wengine walioongozana naye katika ziara hiyo yenye lengo la kutoa mwelekeo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2007/2008 ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Cyril Chami na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Profesa Mark Mwandosya.
 
taaarifa iliyopo ni kuwa baada ya siku mbili za kwanza za ziara kutawaliwa na kuzomewa na kukejeliwa ..mawaziri wameagizwa kutumia mbinu zifuatazo sehemu zenye upinzani mkali au sehemu ambazo uwezekano wakupata wasikilizaji ni mgumu....

1]VIKAO VYA NDANI...mawaziri wameanza kutumia utaratibu wa kuendesha vikao vya ndani na kuepuka mikutano ya hadhara.vikao hivi huwahusisha makada wa wilaya husika ...wakiamini kuwa wakiweza kuwakusanya mabalozi na viongozi wengine ujumbe utawafikia wananchi...na siunajua tena mabalozi watapewa na posho kama hamasa...

2]WAANDISHI WA HABARI..kwenye hizi ziara mawaziri wakiwa na maofisa habari wao na wale wa mikoa wamedhamini pia baadhi ya waandishi wa habari wa magazeti ya mtandao ,ili wasaidie kufunika aibu wanazokutana nazo...kwa hiyo tusitegemee sana kupata habari negative kwa waandishi waliiooongozana na mawaziri..itabidi vyombo huru vitumie njia nyingine ikiwemo za kuwahoji moja kwa moja wananchi wa eneo husika ili kuweza kuwa na uhakika wa habari .

moto huko ni mkali kuliko tunavyosikia...si unajua nchi hii ni kubwa..lakini kwa kuwa simu zipo ..wahariri ni bora wakahakiki habari wanazotumiwa kwa kufanya rondom calls kwenye maeneo mikutano inakofanyika...ili tupate ukweli"call spade a spade"
 
Chonde chonde Mwandosya, usipoangalia na wewe utaharibu kasifa kako. au unatekeleza amri ya mkuu? hata kama hutaki? si ujiuzulu? itakuongezea credit mara milions. kumbuka ujumbe wenu ukizomewa na wewe umo pia no matter how respected you are.

I know you, you are not one of them.
 
hivi ni kweli kwamba pamoja na nia ya kuzima hoja
zinazowakabili, ziara hizi ni pamoja na kampeni ya
kibosile mmoja kuchukua nafasi nyeti kwenye mkutano
mkuu wa sisi mmh(ccm)unaokuja? nauliza tuu
 
hotuba ya mkuu mwisho wa mwezi huu ilisogezwa mbele au imefutwa? naomba kujua hili na kama ipo tutegemee nini?
 
Back
Top Bottom