Ziara Iringa mpya yawapa kibarua kizito TAKUKURU

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
ZIARA IRINGA MPYA YAWAPA KIBARUA KIZITO TAKUKURU

Mkuu wa mkoa Iringa Ally Hapi ameendelea na ziara yake ya tarafa kwa tarafa ikiwa ni siku ya tatu ametembelea tarafa ya Kibengu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kusikiliza wananchi.

Katika ziara hiyo Hapi amezindua jengo la nyumba za walimu katika shule ya sekondari Ilogombe mradi ambao umetekelezwa na fedha za serikali shilingi milioni 141 hadi kukamilika.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa amehoji kiasi cha fedha kutolingana na thamani ya nyumba.
*“kiasi kilichotumika kwenye ujenzi ni kikubwa sana na hakiendani na dhana ya ‘force account’ ambayo msingi wake ni kupunguza gharama.Hatuwezi kugeuza serikali kama shamba la bibi. Bora ukumbatie mzinga wa nyuki kuliko kuchezea pesa za serikali.*
Alisema RC Hapi.

Hapi ameagiza TAKUKURU kuchunguza mradi huo haraka.

Mradi mwingine uliokabidhiwa kwa TAKUKURU ni mradi wa maji UKAMI ambao Mkandarasi alilipwa jumla ya shilingi milioni 285 na mradi kushindwa kufanya kazi kwa chanzo cha maji kukauka kabla ya mradi kukamilika. Sababu kubwa inatajwa ni kutofanyika upembuzi wa kitaalamu juu ya mradi huo. Serikali imelazimika kuingia mkataba Na Mkandarasi mwingine kwa ajili ya mradi mwingine wa maji katika kijiji hicho hicho wenye thamani ya milioni 370.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza ziara yake katika tarafa za Mkoa wa Iringa, Mkuu wa Mkoa Hapi amefurahishwa na utendaji kazi wa afisa kilimo na mifugo wa Kata ya Mapanda ndugu Maurusi Kisinga na kumpa shilingi laki moja na kumuahidi kumpatia pikipiki ili aweze kuendelea kuwahudumia wananchi vizuri.

Mkuu wa Mkoa alihitimisha mkutano wake kwa kusikiliza kero za wananchi.
QWEEEEEEEE.jpg
IMG-20180911-WA0039.jpg
IMG-20180911-WA0036.jpg
 
What is the return on investment kwa hizo ziara zako? unatumia resources zetu walipakodi, right??, isijekuwa unapotezea wananchi muda wao wa kufanya kazi for your political interests.
 
Mbona picha ya jengo la walimu hakuna? Ungepiga picha hilo jengo na sisi tujirizishe, sasa wewe umetuma picha nyingi halafu ukaacha picha muhimu.
 
Tanzania Nayo Inakuja Kuwa Taifa Kubwa
Zero Tolerance Kwenye Corruption
 
Back
Top Bottom