Ziada Seukindo (Meneja Programu JF): Uelewa wa Sheria za Mtandao kwa watu bado ni mdogo

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,623
Madam.jpg

Picha: Ziada Seukindo Meneja Programu JamiiForums

Ziada Seukindo, Mtetezi/mchechemuzi wa haki za kidigitali na mtaalamu wa ushiriki wa wananchi mtandani na program meneja jamiiForums ashiriki mahojiano na Redio ya Kiss FM katika mjadala unaosema, Sheria za mitandao kutofahamika vizuri miongoni mwa wanajamii, inachangia vipi ukatili wa kijinsia? Na hivi ndivyo jinsi mahojiano yalivyokuwa;

Swali: Simu yakwangu bando lakwangu kwanini Sheria ya Mitandao inanikataza kupost kitu chochote kile ninachotaka kuweka mtandaoni?

Jibu: Mtandao umefanya dunia kuwa kijiji hivyo mtu unaweza kufahamiana na watu wengi tofatuti na anna kwa anna ambapo unaweza kufikia watu wachache. Sheria inaangazia kutengeneza usawa na usalama. Sheria inapokwambia usifanye kitu fulani sio tu kwa ajili ya wengine, bali pia ni kukulinda wewe sababu unaweza kujihatarisha wewe na maisha ya watu wengine, na hii ni sababu wewe kama raia serikali ina jukumu la kukulinda.

Mfano kanuni ya Sheria ya makosa ya mtandao inakuta kuwa na password kwenye kifaa chako, sababu mtu anaweza kuchukua kifaa chako akafanya uhalifu ukaingia matatizoni, kwa hapa sheria inakulinda wewe na sio kukupangia jinsi ya kutumia kifaa chako.

***​
Swali: Sheria za Mtandao zikoje, zimegawanyika kwa namna gani?

Jibu
: Sheria zinazogusa mitandano ziko kadhaa kama vile; (ICT Policy 2016) Sera ya TEHAMA 2016 ambayo inatoa muongozo wa namna masuala mazima ya TEHAMA yatakavyoendeshwa nchini

Sheria ya Makosa ya Mtandaoni - imeangazia masuala mazima ya makosa ambayo yanaweza yakatendeka mtandaoni na kutoa makatazo na adhabu mbalimbali zitakazoandamana nayo.

Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Electronic and Postal Communications Act - EPOCA), sheria hii inajumuisha kuna kanuni za masuala ya redio na TV, kanuni za maudhui mtandaoni nk.

Sheria inayoangazia upatikanaji wa Habari (Access to Information Act) - sheria hii inagusia upatikani wa habari nje ya mtandao

Statistics Act - Inatoa miongozo katika suala zima la kutoa takwimu mtandaoni, mfano kutoa taarifa ya idadi ya vifo kwenye ajali, mamlaka husika ndio inatakiwa kutoa taarifa hii. Pia inaongoza masuala mazima ya utafiti nk.

Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi 2022 (Personal Data Protection Act 2022) - inaangazia kulinda taarifa binafsi za watu ndani na nje ya mtandao. Mfano ukijasili Facebook, unaacha jina, email nk hizo zote ni taafifa binafsi. Taarifa binafsi ni taarifa inayokutambulisha wewe moja kwa moja.

***​
Swali: Sheria ipi ni kubwa kabisa katika Makosa ya Mtandao?

Jibu
: Sheria kubwa ni sheria ya makosa ya mtandao, sababu ndio inagusa makosa yote kwa ujumla wake, wakati hizi sheria nyingine zinagusa maeneo husika.

***​
Swali: Hali halisi ya Uelewa wa Sheria za Mtandao kwa ujumla ikoje?

Jibu: Watu wengi hawazifahamu sheria hizi, na hata watu wengi wanaofanya kazi ndani ya mazingira ya sheria hizi unaotarajia wanajua sheria hizi hawazijui. Na hii inachangiwa na ukweli kwamba mambo ya digitali yamechelewa kufika nchini, hatujaanza na teknolojia katika hatua ya chini na kukua nayo na teknolojia inakuwa kila kukicha hivyo tunaparamia pale teknolojia ilipofikia na kuendelea nayo. Hii inafanya mambo mengi inabidi twende nayo hivyo hivyo.
***
Swali: Unaposema Mitandao ya Kijamii unamaanisha mitandao ya aina gani?

Jibu
: Ni mitandao ambayo imetengenezwa kwa ajili ya watu kuwasiliana (socialize) mfano facebook unakuwa na uhuru kufanya utakacho, kuna wanaotumia kibiashara, kutafuta kiki, kufahamika, kuwasiliana na ndugu na jamaa nk. Halafu kuna majukwaa ya majadiliano mfano JamiiForums.Com, huku kuna mambo mengi zaidi kuliko mitandao ya kijamii kama facebook nk, majadiliano kwenye majukwaa yamepangiliwa vizuri, watu wanaosimamia majiliano yaende vizuri kabla hata watu hawajatoa malalamiko (kuripoti), hii ni tofauti na mitandao ya kijamii kama facebook nk ambapo ni mpaka mtu aripoti ndio malalamiko yake yashughulikiwe). Mfano wa majukwaa ni kama JamiiForums, Reddit, Quora nk.

***
Swali: Sheria ambazo tumezitaja zinatumikaje kuchangia Ukatili wa Kijinsia?

Jibu
: Sheria zetu zipo kimya kwenye mambo yanayohusu jinsia, Mfano makosa na mtandaoni yametajwa kwa ujumla, mfano huruhusiwi kumkera, kumuudhi, au kumtukana mtu kwa ujumla lakini haijawekwa kijinsia

Sheria imewekwa kwa ujumla na sio kijinsia. Mfano sheria inakukataza kumkera, kumuudhi na kumtukana mtu lakini haijaelezea hili kijinsia. Kwaiyo mambo ya kijinsia yanashughulikiwa yanashughuliwa kwa jinsi mwenye mamamlaka atavyoona sababu sheria haijaelezea kijinsia.

Pia kutokujulikana kwa hizi sheria kunachangia kuongeza masuala haya ya ukatili kuendelea kwa namna zifuatazo;

~ Mtu anapokuwa hajui haki zake ni ngumu yeye kwenda kushtaki.

~ wanaopokea malalamiko mfano polisi au mamlaka nyingine wanapokuwa hawajui sheria hizi inakuwa ngumu kutenda haki.
Kutokana na mfumo dume kwa mfano, ikiwa mwanamke ametendewa ukatili na kwenda kushtaki halafu amekutana na askari amefungwa na tamaduni hizo mwanamke huyo hatopata haki yake, badala yake atazidi kumdhalilisha; amepeta picha zako za utupu, alizipataje? Ulimtumia, kwanini ulimtumia? Badala ya kumsaidia anazidi kumkandamiza na hapo haki inakuwa imepotea

~ Mawakili kutoendana na kasi ya digitali kwenye masuala ya jinsia.
Mawakili wanafundishwa kuhusu utetezi haki na kupinga ukatili wa kijinsia lakini hawajajikita sana kwenye upande wa digitali sababu mambo ni mapya, sheria ndio zinaendelea kutungwa na wanadelea kujifunza, hivyo mawakili wanatakiwa kujiongeza.

Kukusanya ushahidi wa kidigitali/Mtandao ni tofauti na kukusanya ushahidi wa kawaida na hapa ndipo kesi nyingi sana zinazohusu makosa ya mtandao zinakuwa zinashindwa kutokana na utofauti wa mchakato wa ukusanyaji wa ushahidi mtandaoni. Mtu anaweza kufuta kitu kilichomtia hatiani, unafanyaje kupata ushahidi huo kwa kuzingatia muda na mambo mengine ili ushahidi huo uweze kutumika mahakamani?

~ Watoa maamuzi baadhi wanachangia haki kutotendeka.
Baadhi wamefungwa na tamaduni zinazofanya jinsia moja ionewe, wengi umri umeenda wamepitwa na mambo ya mtandao ambapo wanalazimika kuweka nguvu zaidi kuendana na kasi hiyo wakati yeye si mtu wa mtandao pengine hatumii kabisa, hivyo inakuwa rahisi sana kwa yeye kutenda haki sababu hajui masuala hayo ya mtandao.
***​

Swali: Ni kitendo gani ukikifanya Mtandaoni inakuwa umetenda Ukatili wa Kijinsia?

Jibu
: Ukatili wa kijinsia ni kumnyanyasa au kumdhalilisha mtu kutokana na jinsia yake. Kwa mtandani inaweza kuwa kwa aina mbalimbali kama vile;

Ufatiliaji wa mawaliano ya mtu (Kudukua/hacking) - Hili ni kosa kisheria na pia ni ukatili wa kijinsia, mtu anaweza kuweka kifaa cha kukurekodi kwa sauti au video kukufatilia ndani kwako ambapo anaweza kuweka/kuachilia maudhui hayo mtandaoni

Ukatili wa wazi - Ambapo mtu anakutukana, au ameweka picha za utupu zinazodhamilia kudhalilisha utu wako, kuweka picha ya mwanaume au mwanamke na kuwahusanisha kwa nia ovu

NB: Masuala hayo hayapo bayana moja kwa moja, inategemea na hali ilivyo na kwa jinsi kitendo/kosa limefanyika kwa wakati huo, na hata sheria haitajata bayana kwamba ukifanya kitendo hiki ni udhalilishaji, ila imesema ukiweka kitu chochote kinachoenda kumdhalilisha, kumkera au kumharibia mtu taswira yake kwenye jamii hayo yote ni ukatili wa kijinsia.
***​

Swali: Je, ni Ukatili wa Kijinsia kwa mtu anayeamua kupiga picha au video ya utupu kwa matumizi yake na kuhifadhi kwenye simu, mpaka kufikia hatua ya picha/video hizo kuvuja?

Jibu: Kwa huyu hatuwezi kusema amefanyiwa ukatili wa kijinsia lakini amefanya kosa la kimtandao kwa mujibu wa Sheria ya Mkosa ya Mtandao, sababu hairuhusiwi kuweka picha zenye maudhui ya ngono mtandaoni.
***​

Swali: Sheria inasema tusiweke picha za watoto mtandaoni, vipi kuweka video za mtu akimchapa mtoto au mwanamke mtandaoni kwa lengo la kuripoti tukio hilo?

Jibu
: Si sahihi kufanya hivi na ndio maana hata kwenye mitandao mingine matukio kama haya yanakuwa yanaondolewa na mitandao hiyo. Tukumbuke ukishewaka kitu mtandaoni hakisahauliki, ukiweka kitu mtandaoni si chako tena, kurekodi matukio hayo ya kikatili na kusambaza unaweza kutengeneza jeraha la kudumu (trauma) kwa yule aliyetendewa ukatili.

Tuendelee kupeana elimu na kuacha kutumia mitandao kama sehemu ya kuripoti masuala ya ukatili sababu tunakuwa sehemu ya kuendeleza ukatili huo na kudhalilisha na kushusha utu wa mwathirika bali twende kuripoti kwenye mamlaka zinazohusika kushughulikia masuala hayo ya ukatili wa kijinsia.

Wakati mwingine mtu anakuwa anaweka mtandaoni tukio la ukatili ili lifikie watu wengi ikiwemo wale wanaotakiwa kuchukua hatua lakini, kuweka kwenye mtando haifai, na ikitokea umeweka basi iwe chaguo la mwisho kabisa kufanya ikitokea umemaliza mamlaka zote na hakuna hatua iliyochukuliwa hususani kwa maudhui yanayohusisha watoto sababu watoto wahana usemi kuhusu yanayofanyika dhidi yao alini baadaye inaweza kumuathiri kwenye maisha yake na uhusiano wake na jamii.

***​

Swali: Katika warsha mbalimbali na juhudi za kuelimisha watu juu ya Masuala ya Mtandaoni, yapi mnayafanya ili kuongeza kuongeza nguvu kwenye Sheria za Mitandao?

Jibu
:
Kutoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia, makosa ya mtandao pamoja na sheria zake
Jambo la muhimu ni uelewa wa wanachi linapokuja kwenye masuala ya ukatili wa kijinsia sababu kuna watu wanafanya kwa kujua na wengine ni kwa kutokujua na ukimpa elimu anaacha. Kupitia majukwaa mbalimbali tumekuwa tunawapa watu elimu kujua sheria zinasema nini, jinsi ya kujilinda na unapopata matatizo uende ukaripoti wapi

Kufanya uragabishi (advocacy) ya kuboreshwa kwa sheria hizo
Mbali na sheria hizi kusaidi kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia , sheria hizi zinamapungufu kadhaa, hivyo tunafanya mazungumzo na wanaohusika na kutunga na kusimamia sheria hizo kuhakikisha kwamba sheria inatoa haki na sio kuchukua haki za watu.
***​

Swali: Elimu ikoje kwa watumiaji wa Mitandao ya Kijamii mpaka sasa?

Jibu
: Watu wanaendelea kuelimika japokuwa bado juhudi zaidi zinahitajika sababu hatujafika pale tunapotamani kufika. Hata tukiweka machapisho kwenye mitandao mbalimbali mfano ulazima wa kuwa na password kwenye kifaa chako watu wanauliza na kuchangia mijadala, watu wanabadilika taratibu kadri muda unavyoenda.
***
Swali: Kwa kupima uelewa wa wananchi kutokana na maoni yao juu ya uelewa wao kuhusu ya Sheria za Mtandao na jinsi inavyoweza kuchangia ukatili wa kujinsia, yanatoa picha gani kwenye matumizi ya mitandao ukihusisha na Ukatili wa Kijinsia?

Jibu:
~ Kuna vitu vinafanyika ambayo ni muhimu kuvisema na kupiga kelele, mfano suala la watu kufanyiwa blackmail (kumlipa mtu pesa ili asiseme jambo la fedheha kuhusu wewe) kwa hasa mabinti wadogo.
Kuna tukio ambalo lilitokea Zanzibar kuhusu binti kufanyiwa blackmail takribani miaka 5 toka akiwa kidato cha 4 mpaka kufikia Diploma, anamlipa kijana pesa kwa muda wote huo lakini binti huyo hakusema na kuendelea kufanyiwa hivyo mpaka ilipotokea kuna warsha ndipo rafiki wa binti huyo akaripoti tukio hilo. Binti huyo alipata msaada kutoka kwetu, kijana alitafutwa na kuambiwa kufuta picha hizo na kuwekwa kwenye rada kwa ya polisi kwa miaka 10.

~ Wanaopitia ukatili wa kijinsia mtandaoni wasikae na vitu bali waripoti kwenye mamlaka husika, sheria na mamlaka zipo na zinajali.

~ Haki yoyote inakuja na wajibu, hivyo tuna wajibu wa kujillinda sisi wenyewe kabla hatujalindwa na mamlaka/vyombo vyenye jukumu la kutulinda

~ Tuache kurekodi picha na video za utupu kuwatumia wapenzi husuani kwa mambinti ambao ndio waathirika wakubwa.

~ Angalizo kwa wazazi kujua mitandao inavyofanya kazi na kutumia mitandao hiyo ili uweze kumlinda mtoto wako.
Hata kama unasema wewe sio mtumiaji sana wa mitandao ya kijamii, mwisho wa siku huwezi kuiepuka, kama wazazi/walezi ni muhimu kujua mitandao inafanyaje kazi sababu watoto wanaanza kutumia mitandao mapema sana. Mtoto akikushinda ujuzi inamaana huwezi kumlinda, anaweza kufanya vitu vya aibu ambavyo usingependa vitokee kwake, anaweza kurubuniwa na watu, nk.

***
Swali: Adhabu za Makosa ya Kimtandao zimepangiliwa vipi?

Jibu
: Adhabu zinaanzia kwenye kutoa maudhui/kufuta, kuna faini ambazo zinaanzia milioni 5 na kuendelea sababu makosa haya yanaweza kufanywa na makumpuni makubwa kama Facebook kwa mfano ambapo baadhi ya faini kwenye makosa haya zinafika mpaka bilioni kadhaa au kifungo jela.


Hitimisho
Swali
: Kipi unawashauri watu juu ya Sheria za Mtandao, watu ambao pengine wamekuwa wakichangia Ukatili wa Kijinsia kufanyika?

Jibu
: Hatuitaji sheria ili kutotendeana uovu, hata ukija kubanwa na sheria unaweza kuwa umesababisha madhara makubwa kwa mwathirika, hivyo tujitahidi kupima maudhui kabla hatujayapeleka mtandaoni, sababu unachoweka mtandaoni kinawafikia watu wengi wengi kwa muda mfupi na hivyo kusababisha madhara makubwa sana.

Sheria zipo lakini tutumie utashi wetu katika kuhakikisha mitandao inakuwa sehemu salama wa wote.
 
Uzi mrefu sana upelekwe maktaba.

Comment yangu isiguswe
Naimani utapata cha kujifunza Mkuu sababu yaliyoongelewa yanagusa maisha yetu moja kwa moja.... inaweza isikuathiri wewe lakini ikatokea kwa mtu wako wa karibu wakati ungeweza hata kuwaelimisha.
 
Uzi mrefu sana upelekwe maktaba.

Comment yangu isiguswe

Maarifa mengi yanafichwa kwenye maandishi hakikisha unatenga muda kujifunza zaidi na zaidi usichoke kujisomea kwani ni faida ya ubongo na akili yako na kwa kupanua uelewa wa mambo anuwai
 
Back
Top Bottom