Zeyana Seif wa BBC afariki

Huduma

Member
Jan 26, 2008
68
1
Habari nilizopokea karibuni ni kuwa mtangazaji wa zaidi ya miaka 40 na BBC aliyestaafu miaka michache iliyopita na ambaye ni mzaliwa wa hapa kwetu Zanzibar amefariki dunia akiwa usingizini.

Sitaji jina kwa sasa hivi ili kutowashtua jamaa zake ambao nadhani kwa sasa watakuwa ndio kwanza wanapata habari hizo. Hadi kufikia juzi alikuwa mzima wa afya na alionekana mitaani London akifanya Shopping kujiandaa kwa funga funga za maduka hapa London!


Vicky Mtetema, Abdul Majura na kaka Ngahtyoma nikijisahau, tafadhali, muwaarifu wana JF- ni nani aliyefariki. Nadhani wote watakuwa na dukuduku kumjua bibie. Ina lillahi wa inaillahi rajiuuun!!
 
BBC katika matangazo yao ya asubuhi wameshamtangaza jina lake.
 
BBC katika matangazo yao ya asubuhi wameshamtangaza jina lake.

BBC wametangaza this morning, It is really sad news... I will miss your sweet voice . Poleni wafiwa wote na wadau wa habari hasa BBC

RIP Zeyana Seif
 
Hayati Zeyana Seif in 1959 Photo.

RIP

200706221150553.jpg


Zeyana Seif mmoja wa watangazaji wa kwanza wa kike akiwa na wenzake mwaka 1959.





BBCSwahili.com
 
RIP Zeyana, kila nafsi itaonja mauti. Tangulia mama nasi zamu yetu ikifika tutakufuata.
 
Kwa kuwa hiyo ndio njia, nasi twaja, saa na siku tu ndio hatuijui. Pumziko jema Mama Zeyana Seif.
 
Tunainua mikono na kumuombea dua.Mola amwangazie na kumpa kila la kheri fii jannatu naim.Amin.
 
Zeyana Seif afariki dunia

Imeandikwa na Mwandishi wa BBC

Mtangazaji wa siku nyingi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Zeyana Seif amefariki dunia mjini London Uingereza. Kifo chake kimetokea ghafla siku ya Jumatatu.

Zeyana alikuwa mwanamke wa kwanza kabisa kusoma habari kwenye redio, katika BBC.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Solomon Mugera kwa niaba ya shirika la Utangazaji la Uingereza BBC ametoa pole kwa ndugu na jamaa za marehemu.

Akimzungumzia marehemu, Bw. Solomon amesema alikuwa mcheshi na mchangamfu, na daima alikuwa tarari kutoa msaada wowote katika fani ya utangazaji.

Alistaafu mwaka 2005.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema.

Source: BBCSwahili.com | Habari | Zeyana Seif afariki dunia
 
Marehemu amefundisha batch kubwa sana ya watangazaji wa RTD. Kila RTD ilipoajiri watangazaji wapya, iliendesha Radio Induction Course ambapo watangazaji wakongwe walipewa vipindi huku ikialika na watu wa BBC na Zeyana ni mmoja wao.
RIP Zeyana Seif.
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa; Kazi ya Mungu haina makosa. RIP Zeyana Seif.
 
Hayati Zeyana Seif in 1959 Photo.

RIP

200706221150553.jpg


Zeyana Seif mmoja wa watangazaji wa kwanza wa kike akiwa na wenzake mwaka 1959.





BBCSwahili.com

RIP Zeyana.

Sote tu wapangaji hapa duniani na nyumbani kwetu lazima turejee. Natumai kuwa japo tupo kwenye nyumba nzuri ya kupanga hatutasahau kuboresha na nyumbani kwetu pia, kila kifo cha mmoja wetu ni ukumbusho kwa sisi ambao mkataba wetu haujaisha kuboresha na kwetu pia. Tuache maovu na dhuluma.


Alianza kazi BBC 1965 na kustaafu 2005, hakika sauti ya Zeyana ilikuwa ni nembo ya BBC hasa katika kipindi chote nilipokuwa nikisikiliza BBC kule kijijini kwetu.
 
Back
Top Bottom