Einstein
Senior Member
- Dec 5, 2009
- 121
- 26
Nimesikitishwa sana na matokeo ya kidato cha nne. Katika matokeo hayo zaidi ya 82% ya wanafunzi waliofanya mtihani, wamepata division zero au four!!!!!! Tunaenda wapi??? Ni lazima tujiulize credibility ya hawa wanaojiita mawaziri wanafanya nini ofisini??
Nilipata kusoma shule moja ya pale Kilimanjaro(Shule ya ufundi). Nilikuwa nasoma ufundi wa umeme (O'level). Kwa kweli nilikuwa nashangazwa sana na utaratibu wa shule hiyo, katika swala zima la ufundi na baadhi ya masomo mengine. Zamani mtu alikuwa akimaliza shule ya sekondari ya ufundi alikuwa anaweza kujiajiri mwenyewe.. Lakini katika kipindi hicho ufundi huo niliosoma mimi swala la masomo kwa vitendo lilikuwa halitiliwi maanani.. Walim walikuwa wakijisifu kwa matokeo mazuri(Theoretically) ambapo wanafunzi hawa katika real life hawana chochote. Wengi waliosoma shule hizo wanaweza kuwa mashahidi kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya wanafunzi wanaomaliza shule za ufundi ni empty kabisa, hawana chochote.
Baada ya hapo nilipata kusoma shule moja, wanayoiita ya vipaji. Kiukweli sielewi maana ya huu msemo. Ila huenda wanamanisha shule ni ya vipaji kwa maana zinachukua wanafunzi waliofaulu sana. Walimu wengi katika shule hizo hawana uwezo, mpango-mkakati wa kumjenga mwanafunzi kuwa CREATIVE. Hawana utaalamu wa kisaikolojia wa kumjenga mwanafunzi ili nae aweze ku-reason mambo.. HAKUNA!!
Wanafunzi wengi wanaofanya vizuri, wanaotoka shule za serikali, wengi wao hujihangaikia wenyewe na kwa kusoma vitabu vya kutosha na twisheni ili waweze kuelewa mambo mbalimbali.. Kuna wakati mpaka wanafunzi wanaelewa mambo mpaka wanamzidi hadi mwalimu anaewafundisha ( Maana walimu wengi hawana vipaji vya kufundisha).
Tanzania ni moja ya nchi isiyojali wasomi kwa kuwaacha wakijihangaikia wenyewe bila angalau ya kuwapa sapoti ya aina yoyote. Kwa mtoto wa maskini, hawezi hata kununua vitabu vizuri wala ya kulipa twisheni, ili aweze kujisomea ili afikie malengo yake.. Na wala haina taim nao, kwa maana, serikali inaona kuwa usomi ni swala lisilo na tija kwa taifa hili, bali siasa za kifisadi ndizo zenye tija..
Naomba mwongozo:Kuna haja gani ya kuwa na majengo kibao ya shule, baadhi yaliyojengwa kwa kunyang'anya kuku na mbuzi wa wananchi, wakati walimu wa kutosha hakuna?? Ni bora kuwe na mwalimu makini anaewafundisha wanafunzi chini ya mti, kuliko kuwa na majengo ambayo wanafunzi wake wanafundishwa na ubao mweusi.
Ndg. Majembe asimame sasa, atueleze kwamba mwaka huu katuzawadia zero 65,700. Anatupeleka wapi?? Mipango iko wapi?? Je, ndo kusema wanaongeza wajinga ili watutawale milele?? KWA NINI SERIKALI YA TANZANIA HAMJALI ELIMU??? Ingekuwa ni nchi zenye adabu, waziri huyu angejiuzulu mara moja, au Rais angempa adabu yake! Ila kwa sababu bongo ni TAMBARARE, anapeta tu na kodi za wananchi na wala hana shida.. Inasikitisha!!
Wenzetu wa amerika na ulaya wanawaza jinsi ya kugundua vitu vizito na vyenye technolojia ya hali ya juu, SISI TUNAKAA KUJADILI JINSI YA KUPUNGUZA ZERO, Mmmh!! Huu ni upuuzi.. Haya mambo ya ajabu kabisa.
Lazima watanzania tukae chini tujifikirie kuwa, Mfumo wetu huu wa elimu utatufikisha?? Wasomi wa Tanzania wanatapatapa tu huko duniani wanatafuta elimu, ingawa cha kusikitisha serikali yao haiwajali! Kama hatutakaa chini na kujipanga upya juu ya swala la elimu, basi hakuna sababu ya akina MKURABITA wala MKUKUTA, Maana yatupasa kuandika maumivu kuwa, sisi ni MASKINI MILELE..
SO SAD!!
Nawakilisha