Zermacopolo atangaza nia ya kugombea ubunge Morogoro Kusini Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zermacopolo atangaza nia ya kugombea ubunge Morogoro Kusini Mashariki

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mapinduzi, Jun 5, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  .............................. Dr. Imani Hamza Kondo ( kwenye dunia ya ku-blog wananifahamu kama zemarcopolo), ninatangaza nia ya kugombea ubunge wa Morogoro Kusini Mashariki kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

  ......................Yeyote atakayehitaji taarifa zaidi basi asisite
  kuwasiliana nami moja kwa moja kwa
  zemarcpolo@yahoo.co.uk
  Nashukuru Sana.

  Habari toka Michuzi Blog

  Hongera sana Zermacopolo na kila la heri. Wengine wenye nia hii pia msisite kutujulisha.
   
 2. M

  Mwanakwetu B New Member

  #2
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 18, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera mdau ..... hii ni changamoto kwa sie tunaongojea tustaafu ndio tuanze kugombea ubunge kama vile bunge ni Club Med ya wastaafu!
   
 3. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2010
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 405
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  mwenyezi mungu akujaalie uupate huo ubunge, kwa vyovyote vile utakuwa umewekeza mapesa mengi tu, maana bila millioni mia inasemekana huupati huo ubunge
   
 4. M

  Mkono JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ingependeza kama ungekuja na ajenda ni nini kinakusukuma kufanya hivyo,still unahitaji pongezi mkubwa kwa kuamua kuonyesha njia.
   
 5. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Magreth Sitta una nia ya kugombea jimbo gani?
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2013
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Aiseee......tatizo Chadema
   
 7. Tony Gwanco

  Tony Gwanco JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2013
  Joined: Jan 22, 2013
  Messages: 5,920
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  hongera mwana mapinduzi wembe ni uleule hadi magwada yavuliwe yote yachomwe moto
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2013
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  teh teh teh, watu wagomvi yani wamekuja kuufukunyua huu uzi! wajameni mnatonesha madonda ya 2010. Kweli CCM ina wenyewe, hata ujibaraguze vipi utaishia kunawa tu/
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2013
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Siamini kwamba huyu mtu ni Dr. ukilinganisha na post zake anazoziweka hapa katika juhudi zake za kugandamiza demokrasia. Huyu mtu amekuwa akipinga hoja nyingi hata kama zinaelekea kueleza mantiki (logic). Hata hivyo naweza kuelewa nia yake ya kufanya hivyo kutokana na dhamira yake hiyo ya kugombea ubunge kupitia ngazi ya ccm. Nimeelewa kuwa kumbe msimamo wake huo hauletwi na uzalendo wake , kitu ambacho ni dhahiri, bali kwa kujinufaisha yeye binafsi.

  Nilishawahi kuelezea habari moja kuhusu rafiki yangu marehemu Prof. Seth Chachage. Alipopata PhD yake nilimpongeza na kumwambia, "Hongera bwana, sasa tutakuita Dr."!

  Alinijibu kwa uchangamfu, kama kawaida yake ilivyokuwa, "Wewe vipi bwana, usijali maana tumewaona wengi kama Dr. Nyamwicho, Prof. Vulata na wengine wengi"! Mimi nilimwambia aache utani na apokee hongera.

  Hata hivyo, maneno ya Prof. Chachage, pamoja na kwamba aliyasema kwa mzaha, yalibeba maana kubwa kuliko mzaha. Maana yake ni kuwa unaweza ukajiita msomi, lakini usomi wako uwe na manufaa katika jamii. Wengine mnaweza kutafsiri maneno ya Prof. Chachage jinsi mtakavyoona.
   
 10. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2013
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyu si ndo huwa anashinda humu kutukana na kukashfu hoja zenye mantiki kama Lusinde? Anyway, nampongeza kwa kuamua kuitumia haki yake ya kidemokrasia lakini pia ningependa ufafanuzi wa udokta wake!
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2013
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ni huyu ZeMarcopolo wa hapa jamvini au ni mwingine?

  Kama ni huyu tunaomba wananchi wampe adabu yake maana post zake humu ndani zinamuumbua. Anatetea hata kile kitu chenye fact ili mradi ku-please chama chake. Sikuamini kama kweli wewe ZeMarcopolo ni daktari wa philosofia?

  After all kuna Dr. Tamba, Majimarevu, Dr. Kinyozi, nao ni madokta!! Haki ya nani hizi degree not necessarily zinatufungua macho bali wengine zinawafanya vipofu kabisa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2013
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,137
  Trophy Points: 280
  Sikukosea kumbe niliposema huyu jamaa ana uwezo mkubwa wa kutafakari mambo kwa kina ila ameamua kujivisha umazwezwe. Kila la heri Mkuu katika kuwania nafasi ya kuingia mjengoni.

  ~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

  DR. IMANI HAMZA KONDO MPONDA
  Amezaliwa tarehe 15. 10. 1979 katika mkoa wa Morogoro. Mama yake anaitwa Anna Anthony Mwaga,wa Matombo Morogoro na baba yake anaitwa Hamza Kondo ambaye ni mtoto wa mzee
  gwijege wa Lukonde darajani, Mikese.

  1988 - 1993: Alijiunga na shule ya msingi Mkoani, Kibaha - Pwani. Alianza darasa la pili moja kwa mojabila kupitia darasa la kwanza baada ya kuonekana kuyamudu masomo ya kusoma, kuandika na hesabu ipasavyo. Akiwa darasa la tano katika shule hiyo alichaguliwa kuwa kiranja mwaka 1991.

  Alichaguliwa kuiwakilisha shule hiyo katika mashindano ya taaluma ya kata, ambapo alifanya vizuri na kuchaguliwa kwenda kuiwakilisha kata katika mashindano ya kitaaluma ya wanafunzi wa shule za tarafa. Katika kipindi hiki, pia alijiunga na kikundi cha chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi. Hapo alishiriki katika kuupokea na kuukimbiza mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Kibaha. Pia alishiriki katika kukaribisha viongozi mbalimbali wa kichama katika wilaya ya Kibaha, ikiwa ni pamoja na kutumikia wakati washughuli mbalimbali za chama kama vile chaguzi mfano Katika Uchaguzi wa mwaka 1992 wa viongozi wachama uliofanyika katika ukumbi wa B Melin wa shirika la elimu Kibaha. Miongoni mwa waliouhuria mkutano huo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa sasa wa Chama Cha Mapinduzi Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati huo akiwa mbunge wa wilaya ya Bagamoyo.

  1994 - 1997: Alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya watoto wenye vipaji maalum ya Mzumbe iliyoko Mzumbe Morogoro. Akiwa kidato cha kwanza katika shule hii alichaguliwa kuwa kiongozi wabweni la Mkwawa namba mbili. Kama kiongozi wa bweni alikuwa na wajibu wa kusimamia ulinzi, usalama, nidhamu, usafi na afya za wanafunzi wote wanaoishi bwenini humo. Bweni hilo lilikuwana wanafunzi wa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita, hivyo kuchaguliwa kwake kuwaongoza wanafunzi wa kiato cha zita wenye vipaji maalum kunaashiria kuwa alidhihirisha umahiri katika uongozi. Wakati huohuo alichaguliwa kuwa kiranja wa darasa la kidato cha kwanza C. Alipoingia kidato cha pili tu, alichaguliwa na shule nzima kwa kishindo kuwa kiranja wa nidhamu. Kama kiranja wa nidhamu alikuwa mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ambayo ilikuwa na wajumbe kumi akiwemo mwalimu wa nidhamu wa shule. Taarifa za vikao vya nidhamu vilitolewa ripoti kwa mkuu wa shule (Thomas Msuka). Pia alishiriki ipasavyo katika michezo ya UMISETA ya mkoa wa Morogoro.

  1998 - 2000: Baada ya kufaulu vizuri sana kwa kupata daraja la kwanza

  division one alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya watoto wenye vipaji maalum ya Ilboru iliyoko Arusha kwa ajili ya masomo ya fizikia, kemia na baiolojia. Akiwa kidato cha tano, serikali ya wanafunzi iliyokuwa madarakani wakati huo ilimuomba awanie nafasi ya uwenyekiti wa serikali ya wanafunzi kwa awamu inayofuata, jambo ambalo aliafikiana nalo . Alishinda kwa kishindo cha asilimia 89 dhidi ya John Seka ambaye alipata asilimia 10 ya kura. Asilimia moja ya kura katika uchaguzi huo ziliharibika. Hapo basi akaapishwa kuwa mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya watoto wenye vipaji maalum ya Ilboru mpaka mwaka 1999. Wakati wa mahafali ya kidato cha sita alitunikiwa tunzo ya uongozi bora na tunzoya taaluma kama mwanafunzi bora wa mwaka 2000 shuleni hapo. Mgeni Rasmi katika sherehe hizoalikuwa mbunge wa Arumeru Mashariki (CCM) Mh. Elisa Mollel. Dr. Imani Hamza Kondo, alisoma risala.
   
 13. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2013
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa taarifa yako mtu huyu ni hatari sana Mkuu Dingswayo. Ni Mwandishi wa habari mzoefu sana, Ni Mhadhiri, anajua siri nyingi sana za nchi hii inayoitwa Tanzania.

  Tatizo pekee alilo nalo ni kule kuwa upande ambao ni losing side. Katika siri kubwa Mungu ameweka katika maisha ya binadamu, mojawapo ni ile ya mwanadamu kushindwa kutabiri future yake kwa usahihi wa asilimia 100, na kitu kinaitwa "ubinadamu," ambao naupa tafsiri ya kiingereza ya Flaw. Huyu jamaa yupo upande ambao ni losing side na haoni!
   
 14. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2013
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu nilishawaambia jifunzeni kuwavumilia wenzenu humu ndani tunatofautiana kwa kila kitu,sasa wewe unakurupuka tu angalia sasa umekula BAN ambayo hukuwa na sababu zozote za msingi tena kwa siku kama ya leo ya wikiend!
   
 15. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2013
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hongera sana Mkuu Zermacopolo unajua sisi vijana lazima tuonyeshe kwamba tunaweza,na wala sio kukaa kutumika kama ninavyoona humu ndani kuna vijana wanajiita kwamba wana eli za chuo kikuu halafu wanatumika na wanasiasa,wanasiasa wenyewe wanafanya kazi ya kuwalipa shilingi 10,000 halafu wanafurahiiiii!.

  Haya Bwana na mimi najiandaa kugombea Ubunge kwenye jimbo Flani nitakuja kulitaja siku nitakapoweka hadharani kila kitu.lakini kwa sasa wala sikutanii,tuwasiliane na andika na amini pia ukifika wakati wa kampeni kwenye hilo jimbo unalokwenda kugombea kama kijana mwenzangu kwa sababu naona umri wako tuko sawa ingawa nakuzidi miaka miwili,nitakuchangia shilingi milioni 10.za mafuta kabisa kabisa,andika na amini tuombe uzima tufike.kwa sababu naona sasa hivi Bunge linachezewa,inatakiwa tukaweke heshima humo ndani na tuwaoneshe wananchi kwamba vijana wanaweza.

  Hobgera tena kwa sababu penye nia pana njia. BIG UP SANA:WABHEJASANA Nyanda Wane!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...