Zenda awapongeza mashujaa wa Tanzania siku ya mashujaa

Omary Kipingu

Member
Feb 22, 2016
40
48
ALICHOZUNGUMZA KAIMU KATIBU IDARA YA VYUO NA VYUO VIKUU UVCCM KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA NCHINI TANZANIA KATIKA KITUO CHA TELEVISION TV1

Jana tarehe 25/07/2017 ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya kumbukizi ya mashujaa nchini.

Hiki ndicho alichokizungumza mchambuzi wa maswala ya kijamii ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Idara ya vyuo na vyuo vikuu UVCCM Ndg. Daniel Zenda alipoalikwa katika kituo cha Television TV1.

1. " Ushujaa ni hatua ya juu ya uzalendo" - Daniel Zenda.

2. " Ili uweze kuwa shujaa lazima uwe mzalendo" - Daniel Zenda.

3. " Kuna mashujaa wa aina mbili, walio hai na waliofariki" - Daniel Zenda.

4. " Hatuna budi kuwaenzi mashujaa kwa kufanya shughuli kubwa za kijamii kama kupanda miti , kufanya usafi nchi nzima n.k" - Daniel Zenda.

5. " Hatuna budi kuwaenzi mashujaa wetu kwa kuwatembelea walio hai na kuwaombea dua au kuwafanyia ibada waliofariki" - Daniel Zenda.

6. " Kila mtu anaweza kuwa shujaa katika eneo lake kutokana na mamlaka aliyonayo kwenye jamii inayomzunguka" - Daniel Zenda.

7. " Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Katibu Tarafa wakiwajibika ipasavyo kwenye majukumu yao watakuwa mashujaa kwa mfano Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ni SHUJAA " - Daniel Zenda.

8. " Katika nchi yetu tunaye shujaa ambaye ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli" - Daniel Zenda.

9. " Kuna mambo makubwa ameyafanya na anaendelea kuyafanya kwa ajili ya watanzania kama kuzuia mchanga wa madini usiende nje (makinikia), kupambana na ufisadi n. k" - Daniel Zenda.

10. " Hakika Rais wetu ni shujaa wa kweli, hatuna budi kumlinda na kumuombea kwa mungu ampe afya njema" - Daniel Zenda.

11. "Mwisho nawaasa watanzania na viongozi wetu tuige kutoka kwa shujaa wetu aliye hai Rais Dkt. John Pombe Magufuli" - Daniel Zenda.

IMG-20170726-WA0291.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom