Zenawi katika ubora wake: Magufuli aige mbinu na mikakati ya mwana huyu wa Afrika

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
32,985
60,480
Sikuwa namfuatilia Meles Zenawi mpaka pale Zitto Kabwe alipoandika makala ya kuomboleza kifo chake.

Baada ya kumfuatilia kwa kweli nimemkubali kwamba alikuwa ni kiongozi mwenye maono na misimamo ya kuisaidia nchi yake.

Particularly nakubaliana naye kuhusu mtizamo wake ktk jinsi ya ku-finance miradi mikubwa ya maendeleo ya miundombinu.

Lingine ni kwamba alikuwa kiongozi imara ktk mambo anayoyaamini, na alikuwa na uwezo wa kuyatetea popote pale. kwa lugha nyingine alikuwa na USHAWISHI.

Pamoja na hayo, alikuwa na mapungufu ya hapa na pale. kwa mfano, analaumiwa kwa kugawa ardhi kubwa kwa wawekezaji huku wananchi wake wakifukuzwa ktk maeneo yao.

Nawaomba mfuatilie mahojiano aliyoyafanya ktk mkutano wa Africa Economic Forum uliofanyika nchini kwake. ili usipoteze muda msikilize kuanzia dakika ya 14.35

cc chige, The Boss, Kimweri, Bukyanagandi, Tetty, Geza Ulole, bagamoyo
 
JokaKuu,

Kumbuka usemi unaosema kwamba 'every politics is local'

Zenawi ameifanyia mambo mazuri Ethiopia, lakini kama ilivyo kwa shilingi upande wa pili wa Zenawi nao una mambo tofauti. Ndani ya Ethiopia kuna wanaomuona kama 'brutal ruler, wengine dikteta na wengine wanamuongelea kama muuaji'. Tanzania ina wakimbizi toka Ethiopia na hadi leo bado tunapokea vijana wanaokimbia hiyo nchi.

Jambo ambalo nadhani Magufuli anaweza kujifunza kutoka kwa huyo kiongozi wa Ethiopia ni kutambua afrika haiwezi kupiga hatua kwa kutumia definitio ya demokrasia toka nchi za Magharibi. Lazima demokrasia ya Afrika iendane na mazingira halisi ya Afrika ambayo watu wake wengi bado hawana elimu, na maskini.
 
Suala la kuwabana wapinzani wake wa kisiasa naliona kama moja ya mapungufu ya Meles Zenawi.

Kwa upande wa Tz nadhani demokrasia yetu imeshafika mbali, kufuata mitizamo ya Meles itakuwa kuturudisha nyuma.

Mimi anaponikosha ni kuhusu msimamo wake kuhusu uwekezaji mkubwa ktk miundombinu. wenzetu wako very BOLD kwenye uwekezaji wanaofanya.

Wakati JK na Magufuli wanafikiria megawatt 100 mpaka 300 ya umeme wa gesi, Ethiopia wamewekeza ktk megawatt 3000+ za umeme wa maji. sisi tunasuasua ktk ujenzi wa reli ya standard gauge, wenzetu wameshamaliza reli ya addis to Djibout[bandarini] na sasa hivi wanataka kuunganisha Addis to Juba, South Sudan.

Hivi viwanda vya NGOZI ambavyo Magufuli bado anaota njozi kuvianzisha, Ethiopia tayari wameshaanzisha na wana-export bidhaa za ngozi vikiwemo viatu.

Tatizo lao ni kwamba UMASIKINI wa Ethiopia ni mkali kuliko wa hapa Tz ndiyo maana unaona wananchi wao wengi wanakimbia nchi pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali yao kuinua hali ya uchumi.
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Tatizo nchi za Kiafrika tunaziweka katika kapu moja na nchi za Magharibi kwenye sera za kiuchumi na kisiasa wakati taasisi zetu za kutunga sheria, kusimamia sheria na kutafsiri sheria ni dhaifu huku mazingira kwa maana ya wananchi wakiwa sio rafiki wa sera hizo.

Tunakata tukifanye kinachofanyika kwa sasa, let say, Marekani au Uingereza wakati wenzetu hali kama zetu kwenye masuala ya kiuchumi na kisiasa walihangaika nazo mwishoni mwa karne ya 19.

Kinachofanyika katika nchi za Kiafrika ni sawa na kumlazimisha mtoto anayetambaa kuanza kukimbia!
 
Hayo uliyoyaeleza ni moja ya mambo ambayo Meles ameyatolea ufafanuzi.

Kwa mfano, ameeleza kwanini si busara kusubiri private sector kuwekeza ktk miradi mikubwa ya miundo mbinu.

Vilevile amezungumzia mahusiano ya demokrasia na maendeleo. pamoja na masuala mengine mengi.
 
..hayo uliyoyaeleza ni moja ya mambo ambayo Meles ameyatolea ufafanuzi.

..kwa mfano, ameeleza kwanini si busara kusubiri private sector kuwekeza ktk miradi mikubwa ya miundo mbinu.

..vilevile amezungumzia mahusiano ya demokrasia na maendeleo. pamoja na masuala mengine mengi.
Tanzania tulilazimishwa kuingia kwenye kapu la kiuchumi na kisiasa bila hata kupewa muda wa transition na mbaya zaidi watu waliotusaidia kuingia kwenye kapu ni aina ya Mzee Chenge ambao ushauri wao kisheria kuhusu maslahi ya taifa ulikuwa umejaa ubinafsi na ulafi.
 
Nadhani UBINAFSI ndiyo tatizo letu kubwa.

Pia tumewekeza "mayai" yote kwa mtu mmoja--Raisi.

Tungekuwa na taasisi huru na imara, particularly bunge letu, tungeweza kuwa-mitigate wahuni kama Chenge.
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Ubinafsi wa viongozi waliopita ndio umemaliza nchi yetu. Leo hii tuna waona wamaana na walikua wanachofanya lakini walijali familia zao zaidi kuliko watanzania. JPM anajaribisha kurekesha uchumi kama Tanesco kumiliki mitambo yao wenyewe na kuachan na wawekezaji ambao wanataka kupata return kubwa ya investment.
 
..nadhani UBINAFSI ndiyo tatizo letu kubwa.

..pia tumewekeza "mayai" yote kwa mtu mmoja--Raisi.

..tungekuwa na taasisi huru na imara, particularly bunge letu, tungeweza kuwa-mitigate wahuni kama Chenge.

Kweli kabisa Mkuu! Hii ni nchi iliyoongozwa na CCM kwa miaka zaidi ya 50 ila kila Rais aliyeingia madarakan alikuja na mtazamo wake utafikiri ni mpinzani, hili ni tatizo kubwa sana kwan hakuna anayejua nchi kama nchi inataka kuelekea wapi ki-maendeleo.

Ukiangalia mfano Kenya wao wako kwenye ubepari miaka yote wamebadili marais ila mtazamo wa nchi uko palepale, Utakuwa na wapinzani ambao mnapingana ndani ya mfumo mmoja.

Kwa mfano hivi kwa nia nzuri ya Rais Magu je? kuna mtu yeyote anaeelewa anatupeleka wapi na kwa mtazamo upi? Leo wanakuja wa vietinam hapa tunataka tufanane nao bila kujua wanafuata mrengo upi.

Kwa Mtazamo wangu lazma nchi i-identify mfumo wake na watu wauelewe then wapinzani na wenye mawazo tofauti tutapingana kutoka hapo!

Vinginevyo tutaendelea kupiga kelele na kuwasifia wenzetu huku tukiendelea kudidimiza maendeleo
 
..nadhani UBINAFSI ndiyo tatizo letu kubwa.

..pia tumewekeza "mayai" yote kwa mtu mmoja--Raisi.

..tungekuwa na taasisi huru na imara, particularly bunge letu, tungeweza kuwa-mitigate wahuni kama Chenge.
Kumbuka wakati tunaingia kwenye kapu la siasa na uchumi wa kimagharibi, CCM ilikuwa imeishaingiliwa na watu wa aina ya Mzee Chenge kwenye meza za maamuzi ya kitaifa.

Watu kama Mzee Chenge wasingeweza kujichimbia kaburi wenyewe wakati walikuwa wanaweza kutumia utaalamu wao wa mambo ya sheria katika kujinufaisha binafsi.

Kwa sababu hatukupata muda wa transition, ilikuwa ni vigumu kuiondoa au kupunguza nguvu ya Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama Taifa ili kuwepo na checks and balances katika uendeshaji wa nchi.
 
Tunapenda sana kukuza mambo na kukubali propaganda kutoka kwa wanasiasa wetu ambao ukiangalia kwa undani ni waongo au hawana exposure au sijui tuseme hawapo enlightened.

Ethiopia ipo nyuma sana kiviwanda katika bara la Africa. Ethiopia haijaifikia Tanzania kwenye viwanda (less industrialized according to UNCTAD data).

Na haya mawazo ya kihayawani kuwa treni ya umeme ndiyo maendeleo itabidi tuyaache. Hii miradi inakuwa financed na banks kama vile ADfB na ili mradi ufaulu ni lazima kuwe na faida, siyo kuwa tu na miradi hovyohovyo.

Thika road, Addis Railway na mabasi yaendayo kasi Dar, ni miradi ambayo ni ya mikopo.
Ni upuuzi kulitukana Taifa ambalo kwa kipindi hicho hicho limejemga gas pipeline ya $ 1.8bn, transit system ya 300m$ halfu usifie miradi ya 300 mil $ ya Thika na Addis kuwa mfano wa kuigwa.

Bwawa la mto Nile ni mradi ambao una faida na Ethiopia inahitaji, tusipende kuiga mambo bila mpangilio..
 
..hakuna mtu ametukana Tz.

..tunachosema ni kwamba yako mazuri ya kuiga toka kwa Meles Zenawi na moja wapo ni jinsi anavyowekeza ktk miundombinu.

..mradi wa reli ya Addis to Djibout una kadiriwa kuwa na thamani ya $ 5 billion. mradi wa kuzalisha umeme unakadiriwa kuwa na thamani ya $ 4.8 billion. Hapo bado hatujajumuisha mradi wa treni kwa jiji la Addis Ababa.

..pamoja na umasikini wa Ethiopia, na taarifa za Unctad kwamba tuna viwanda vingi kuwazidi, inaelekea wenzetu wanawekeza kwa kasi zaidi ktk miradi ambayo ni ya msingi ili kuweza ku-industrialize.

..Wenzetu wanatumia wa nguvu za maji kutosheleza mahitaji ya nchi nzima. Wakati huo huo Tz tuna gesi, makaa ya mawe, lakini bado hatuna umeme wa kututosheleza.

..Hata Raisi Magufuli naye anakerwa na huu umasikini wetu wakati tuna utajiri wa kila aina. There is nothing wrong kudadisi kama tunaweza kuiga toka kwa Ethiopia, Kenya, Rwanda, Angola, etc etc ktk harakati zetu za kujikwamua na umasikini unaotuandama.
 
Eeh bwana eh!! Huyu Zenawi alikuwa na Elimu ya kiwango gani, jamaa alikuwa kichwa kweli kweli! Amenikumbusha sana Jerry Rawlings, na Kambarage anajua jinsi ya ku tame na multioational Companies anajua jinsi ya kula nao lakini yeye akitumia kijiko chenye mkono mrefu the guy was gifted in every sense of the word - tuwe wakweli hapa jamaa huyu alikuwa anaona beyond his nose, wachangiaji wengine walikuwa a distant second kusema kweli.

Kinacho nifurahisha sana sana ni umahili wake kunyambua masuala kuhusu suala pana la infrastructure, kama ulijuhi vizuri hapo ndipo watawala na wawekezaji upiga pesa ndefu na kuwachia madeni ya kufa mtu, we angalia masuala ya ufisadi mkubwa katika Nchi nyingi za Kiafrika chanzo chake kimejikita katika sekta hii nyeti, kama kiongozi wa nchi hajui vizuri crets na crescent ya suala hili pana, ni rahisi sana Taifa likaingizwa mjini na wajanja bila ya kujitambua.

Nampa a Big up the late Zewani, pamoja na mapungufu yake kama binadamu wote tulivyo, lakini mazuri yake yana out weigh mapungufu, the guy knew this stuff like back of his hand.

Sasa Tanzania kama nchi tuna nini cha kujifunza kutoka kwa maono na misimamo yake? Binafsi napendekeza Dk.Magufuli atafute kanda/dvd/machapisho ya Zenawi ambazo kwa mawazo yangu naziona kama zitakuwa ni treasure trove kwa Dk.Magufuli - azitafute amsikilize kwa umakini sana the late Zenawi.

Nimalizie kwa kurudia kusema tena kwamba Tanzania as a Nation gotta lot to learn from Zenawi(RIP).
 
..nadhani UBINAFSI ndiyo tatizo letu kubwa.

..pia tumewekeza "mayai" yote kwa mtu mmoja--Raisi.

..tungekuwa na taasisi huru na imara, particularly bunge letu, tungeweza kuwa-mitigate wahuni kama Chenge.

Nimeisikiliza vyema tunachomiss watanzania ni UZALENDO,kama tungeweka UTAIFA kwanza haya yangekuwa historia.Haingii akilini kila kitu unampa mgeni,hivi imeshindikana kwa mwenyeji kupewa nafasi??

Hivi tumeshajiuliza hawa wageni wanapata wapi mitaji??Mitaji yao yote inapata hapa hapa Tanzania kutoka kwenye Bank zetu wenyewe na kudhaminiwa na Serikali,hivi kama serikali inaweza kuwadhamini wageni kwanini wasiwadhamini RAIA wake??

Kitu kingine UMIMI wa Watawala wetu,wamejiondoa kwenye UONGOZI wamejivika UKABURU na UDIKTETA,hakuna anayeona kwamba anafanya makosa,hakuna ruhusa kumkosoa maana kumkosa humtendei haki unamkufuru,unamdhalilisha sababu umemkosoa.

Kitu kingine kwa serikali kuown BUNGE,BUNGE letu haliko huru,limekuwa RUBBER stamp,limechaguliwa viongozi wake very weak candidates.Tumeona wala rushwa ndiyo viongozi wa bunge na wengine ni mawaziri.hakuna mtawala anayelisikiliza,na kwa sababu ya CHOYO na UBINSAFSI wabunge wa chama tawala wanashindwa hata kuiwajibisha serikali kwa sababu MAOVU yao yatatoka nje,watakosa Ubunge,watakosa UWAZIRI,watakosa mahitaji yao makuu kiuchumi.UCHOYO umeliharibu TAIFA,na wale wanaoikosoa serikali wamenyamazishwa kwa kupewa hongo ya ili kufungwa midomo.

Kama Rais anakashfa unadhani atalisaidia TAIFA.Tunatakiwa kweli kuliangalia tatizo la RUSHWA ya uongozi,wabunge wangapi wamepita kwa kutoa RUSHWA,TAKUKURU ilikuwa inajua hili imelifanyia kazi??Tume yetu ya UCHAGUZI inasemaje kuhusu RUSHWA kutumika kwenye CHAGUZI,nina uhakika ikisikia ni wa UPINZANI lazima atapewa adhabu kali na akiwa wa chama tawala watasema ni majungu au wanafanyia kazi.

Kama TAifa tunatakiwa kudai TUME HURU ya uchaguzi,yenye meno,inayoweza kumshataki mgombea anayetoa RUSHWA,inayomchunguza mgombea kabla hajachukua form.Tunahitaji tume ambayo kweli itakuwa HURU haitaingiliwa na Serikali au uwezekano wa kupewa RUSHWA.

Na kitu kingine kupunguza Wagombea kupelekana mahakamani kwani kuna sheria ambazo zikikiukwa ni rahisi kuwa solved within Tume ya Uchaguzi,mfano mzuri ni ule wa kumtangaza aliyeshindwa badala ya aliyeshindwa ambapo uamuzi unaweza kutolewa siku hiyo hiyo na kuondoa gharama zisizo za lazima.

Matumizi ya Polisi,kutumia nguvu kubwa kwa ajili ya kulinda Chama kimoja tu.Lugha za Matusi na ubaguzi,kutumia Lugha zetu badala ya lugha ya Taifa ,na mwisho Tume irudie kufanya Uandikaji wa kudumu wa daftari la wapiga kura kuanzia sasa kwa kutumia vifaa vya kisasa siyo vile used BVR.Tume ikubali haiko huru na zoezi la kuandikisha wapiga kura liwe la UHURU na HAKI,tusinyimwe nafasi,eti sababu ya MUDA.

Nategemea Serikali ikikubali weakness zake na kuacha mara moja kutumia nguvu kubwa kuuzima upinzani,kwani bila upinzani IMARA hakuna CHAMA TAWALA Imara tukubali hivyo.Na watawala wakubali kwamba wapinzani siyo Foreigners ni watanzania wenye haki sawa na wasio na vyama au wanachama wa chama Tawala.

Watanzania tuache kujadili mtu tuanze kujadili issues,tuweke UTAIFA mbele tusupport pale panapohitaji support,tukosoe panapohitaji kukosolewa,kukubaliana katika kutokubaliana.

Tuondoe Siasa kwenye maisha ya Mtanzania,sioni umuhimu wa wakuu wa wilaya au wakuu wa mikoa.Serikali iangalie namna yakutoa hawa wanaokuwa wakuu wa wilaya au wakuu wa mikoa ambao 98% wanasimamia SIASA kuliko UTAIFA.
 
Sikuwa namfuatilia Meles Zenawi mpaka pale Zitto Kabwe alipoandika makala ya kuomboleza kifo chake.

Baada ya kumfuatilia kwa kweli nimemkubali kwamba alikuwa ni kiongozi mwenye maono na misimamo ya kuisaidia nchi yake.
Msema kweli mpenzi wa Mungu. Ni kiasi cha miezi 2 au 3 nyuma ndipo nilianza ku-pay attention kuhusu Ethiopia lakini kabla ya hapo nilikuwa naichukulia poa sana hii nchi. Mwishoni mwa January 2016 nilikutana na mdada mmoja wa Kihabeshi. Kumbukumbu ambayo bado ilikuwa imetawala kichwani mwangu ni ya vita kati ya nchi mbili masikini kabisa Afrika ambazo mara kwa mara kwa mara ukumbwa na baa la njaa! Ni kumbukumbu ya vita kati ya Ethiopia na Eritrea!

Baada ya kuwa pamoja kwa siku chache na yule dada, maelezo yake yakawa yanakataana moja kwa moja na hisia zangu hasi dhidi ya Ethiopia kwamba ni linchi maskini lisilo na uwezo hata wa kujilisha. Awali, nilidhani yule dada anaipaisha tu nchi yao lakini baadae nilipokuja kufanya utafiti... thanks God, tangu nilipokutana nae nilikuwa nimehifadhi ulimi wangu vinginevyo ningejisikia aibu! Ndipo nikaja kugundua kwamba Ethiopia niliyokuwa nayo mimi kichwani ni Ethiopia ya zamani ambayo ilikuwa imebadilisshwa kwa kiasi kikubwa na Meles Zenawi.
 
Sasa kama Ethiopia wako juu...... ni kwa nini watu wake wanaikimbia nchi kwa umasikini?

..wapo na Wachina wamekimbilia maisha magumu kwao na kuja kubangaiza Tz!!

..hayo uliyoyaeleza ndiyo MAPUNGUFU ya ukuaji wa uchumi wa Ethiopia.

..tafiti mbalimbali zinasema kwamba Ethiopia is the fastest growing economy in the world.

..Tanzania ni namba 11 ktk baadhi ya tafiti zilizofanyika kuhusu ukuaji wa uchumi.

..hapa tunajaribu kuangalia ni mambo gani mazuri wenzetu wanafanya, ambayo tunaweza kuyaiga ili tuweze kupiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.
 
Tunapenda sana kukuza mambo na kukubali propaganda kutoka kwa wanasiasa wetu ambao ukiangalia kwa undani ni waongo au hawana exposure au sijui tuseme hawapo enlightened.

Ethiopia ipo nyuma sana kiviwanda katika bara la Africa. Ethiopia haijaifikia Tanzania kwenye viwanda (less industrialized according to UNCTAD data).

Na haya mawazo ya kihayawani kuwa treni ya umeme ndiyo maendeleo itabidi tuyaache. Hii miradi inakuwa financed na banks kama vile ADfB na ili mradi ufaulu ni lazima kuwe na faida, siyo kuwa tu na miradi hovyohovyo.

Thika road, Addis Railway na mabasi yaendayo kasi Dar, ni miradi ambayo ni ya mikopo.
Ni upuuzi kulitukana Taifa ambalo kwa kipindi hicho hicho limejemga gas pipeline ya $ 1.8bn, transit system ya 300m$ halfu usifie miradi ya 300 mil $ ya Thika na Addis kuwa mfano wa kuigwa.

Bwawa la mto Nile ni mradi ambao una faida na Ethiopia inahitaji, tusipende kuiga mambo bila mpangilio..
Hizo data ni zamwaka gani mkuu? Kama ni 1970's sawa tz tulikua na viwanda vingi kuliko Ethiopia lakini kama ni za currently ni big no wenzetu washatuacha mbaaali
 
Hizo data ni zamwaka gani mkuu? Kama ni 1970's sawa tz tulikua na viwanda vingi kuliko Ethiopia lakini kama ni za currently ni big no wenzetu washatuacha mbaaali
Kwa sababu umeshakuwa programmed, umeshaaminishwa hivyo. Siyo kwamba una data, Ila una imani kuwa Ethiopia is way industrialized.
Wewe tafuta za mwaka huu au za Jana halafu ndiyo ubishe.
 
Back
Top Bottom