Zena wa TTCL Customer Service yake Hovyo - Soma haya majibu!

Mkuu wangu tafadhali.... Hivi kama hajui ulitegemea aseme nini zaidi?. bila shaka kisha kwambai ahajui wewe bado unataka akueleze approx. itachukua muda gani wakati hajui. Je ulitaka akudanganye?..au afanye guess work!

Do u know what you talking about??yeye kama customer services kazi yake ni nini??kupokea simu na kuwajibu watu uchafu au??yeye ilibidi atoe approx yake au aulize kwa hao ma engineer,sio aseme mimi sio engineer kwanza aliyepiga simu hajui kama yeye ni customer services??analipa hela kupata internet sasa why wamzingue??stupid Zena

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
(toa ushauri, hiyo campaign ifanyikaje? mi nashauri tuwe tunawaweka tu humu ndani, au tuwaanzishie web kabisa, kila tukikutana nao tunawaweka kwenye mtandao)

Hiyo inaweza kuwa sehemu ya campaign inabidi tuwaonyeshe kuwa tumechoka na huduma zao mbovu tunaweza kuwaweka humu ndani lakini je waajiri wao watajua?

Baadhi ya makampuni yanatumia pesa nyingi kujitangaza,yanalipa pesa nyingi kwenye vyombo vya habari ili habari yoyote mbaya inayowahusu isiandikwe nina uzoefu na kampuni ya airtel lakini pamoja na kuchukua hatua mpaka TCRA hili swala lilizimwa na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa bila kuwaonyesha hawajua mteja ni mfalme
 
Tatizo kubwa sanaaaa,hawa ma HR wanachukua ma customer services wa ovyo sana ndio maana,plus elimu hamna hata kidogo,yaani anikatie simu wakati hela ya mshahara namlipa mwenyewe,dharau sana

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
POLE MKUU....miongoni mwetu huwa tunataka unyumba pia kwa hawa warembo through customer care free calls..
 
Tatizo alilonalo Zena lipo karibu ofisi zote za serikali na huduma za jamii mbalimbali. Mimi nafikiri ni kwa sababu ya mishahara midogo, maana watendaji hao hao wakiajiriwa na ofisi za wageni toka nje wanakuwa na heshima nzuri sana. Hata ukiwakuta nje ya nchi wanakuwa na nidhamu nzuri sana. Hapa kwetu matatizo ni kama mawili hivi la kwanza pesa ndogo, la pili ni Uvivu unaosababishwa na pesa hiyohiyo kutokutosha hivyo unakuwa umekaa kutafakari namna ya kuongeza kipato kwa njia zisizo rasmi. Ndio maana wakenya wanatuzidi.
 
Hasa mashirika ya serikali kinyaa sana, sijui huwa hawana evaluation kwa watumishi???
 
Kama kunamtu analiyewahi kuwapigia TCU nadhani analijua balaa lake, kupokea simu tu ni utata.
 
(toa ushauri, hiyo campaign ifanyikaje? mi nashauri tuwe tunawaweka tu humu ndani, au tuwaanzishie web kabisa, kila tukikutana nao tunawaweka kwenye mtandao)

Hiyo inaweza kuwa sehemu ya campaign inabidi tuwaonyeshe kuwa tumechoka na huduma zao mbovu tunaweza kuwaweka humu ndani lakini je waajiri wao watajua?

Baadhi ya makampuni yanatumia pesa nyingi kujitangaza,yanalipa pesa nyingi kwenye vyombo vya habari ili habari yoyote mbaya inayowahusu isiandikwe nina uzoefu na kampuni ya airtel lakini pamoja na kuchukua hatua mpaka TCRA hili swala lilizimwa na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa bila kuwaonyesha hawajua mteja ni mfalme

basi tutaanzisha mtandao wa kuwachora tu watu wanaotuharibia nchi
 
Mkuu unamshangaa ZENA! kama kiongozi wa chombo cha juu kama BUNGE anamwambia mwenzake anawashwawashwa,itakuwa kwa ZENA?
 
POLE MKUU....miongoni mwetu huwa tunataka unyumba pia kwa hawa warembo through customer care free calls..

hahahaaa mi sikutafuta hiyo huduma mkuu, si unaona hata maongezi yangu hayaelekei kabisa huko?
 
afazali umeanzisha uzi huu....yupo na Irene wa tigopesa! Huyu nimemwambia nimemtumia mke wangu hela na meseji imekuja na ref namba ninayo kakataa. Nikamwambia basi angoje nimtajie hiyo ref no, akasema hayupo kubishana na mteja, akakata simu. Wanasema simu za malalamiko huea zinarekodiwa lakini sidhani kama kuna anayehangaika kuzisikiliza na ndio maana wahudumu wanajibu ovyo
 
Bold basi ilo jina, yes, simu huwa zinarekodiwa, inabidi tuwe tunaweka tu hapa, cha msingi tusimuonee mtu, wao kampuni za simu ziwajibike kupata ushahidi kutoka recorded voice
 
...Mimi yamenikuta kwa CC ya Vodacom. Kwa kuwa nina ushahidi wa kutosha wa incompetence waliyonifanyia staff wao kitengo hicho, nimemua kuwa nitakwenda nao sambamba ikibidi hata mpaka makao yao makuu, iwe Afrika Kusini ama Uingereza hata kwa email tu ilimradi wajue tu tunachofanyiwa huku. Ninakwenda ngazi kwa ngazi. Kwa kuanzia naomba msaada wa email za Vigogo hawa wa Vodacom: Mkurugenzi Mkuu Renne Meza, Rukia Mtingwa, Mwamvita Makamba na Afisa Uajiri Stella nani sijui...
 
Mkuu wangu tafadhali.... Hivi kama hajui ulitegemea aseme nini zaidi?. bila shaka kisha kwambai ahajui wewe bado unataka akueleze approx. itachukua muda gani wakati hajui. Je ulitaka akudanganye?..au afanye guess work!

..coming from you, that is really saddening comrade Mkandara!
 
Customer care courses wanafanya sana, ni usimamizi na kuwa na uniformity kwenye its application...nadhani angeomba tu namba yako na kukupigia akiwa na jibu,
 
Customer care courses wanafanya sana, ni usimamizi na kuwa na uniformity kwenye its application...nadhani angeomba tu namba yako na kukupigia akiwa na jibu,

Nilishakaa emergency desk ya TANESCO ilibaki nusu tu nimjibu ***** mtu, maana unapokea unaanziwa matusi mwanzo mwisho kisha mnaambiwa 'mkipenda rudisheni umeme,mkipenda tulazeni giza'
 
Mkuu wangu tafadhali.... Hivi kama hajui ulitegemea aseme nini zaidi?. bila shaka kisha kwambai ahajui wewe bado unataka akueleze approx. itachukua muda gani wakati hajui. Je ulitaka akudanganye?..au afanye guess work!
mkuu ila kuna ile lugha ya kuvutia kwa wateja,mtu anaweza akakueleza tu kwa kauli nzuri na ukaridhika.Mbona wenzetu wa nchi zingine wana maneno mazuri
 
na huduma za kitapeli katika mitandao yote hapa tanzania ni balaa.
Vodafone 555 blue na offer zisizotolewa ni wizi mtupu, ukidai haki unazostahili unaambiwa wewe ni mteja mkorofi, hiyo nilifanyiwa na mtu mmoja mutta vodashop mwanza ppf branch.
 
Back
Top Bottom