Zena wa TTCL Customer Service yake Hovyo - Soma haya majibu!

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Kumekua na malalamiko mengi kuhusu huduma mbaya kwa wateja hasa kutoka kwa mashirika ya Umma, na leo nimekutana na hili, ninafikiri kushare hizi experience na kama wahusika wanaona basi iwasadie kuchukua hatua.

Ninatumia huduma ya TTCL broadband kwa internet, ni huduma nzuri. leo mida ya saa 12 huduma ikakatika na mie nilikua na utitiri wa kazi, nikaamua kupiga simu huduma kwa wateja.


Nilipiga namba 100, haya yalikua maongezi yetu


Zena (Customer Service -TTCL): Hallow, nikusaidie nini
Mimi: Hallow, ninaitwa (nikataja jina), ninaongea na nani?

Zena (Customer Service -TTCL): Naitwa Zena, Nikusaidie nini?
Mimi: Asante Zena, ninaongea kutoka UmojaSwitch kijitonyama, toka nusu saa ilopita hatupati connection ya internet, kuna tatizo?

Zena (Customer Service -TTCL): Ndio, kuna shida kubwa kweli, hata sisi wenyewe hapa hatupati internet, lakini mafundi wanafanyia kazi
Mimi: Je, tuitegemee baada ya muda gani?

Zena (Customer Service -TTCL): hapana siwezi kusema, nimeshakwambia hata sisi wenyewe hatupati hiyo internet na mafundi wanafanyia kazi, unajua mimi sio injinia, kwa hiyo siwezi kusema itachukua muda gani
Mimi: sikia zena, sitegemei wewe uwe injinia, lakini nategemea wewe uwe taarifa, ndio maana nakuuliza, lakini asante.

zena akakata simu!.

Mytake:
Hapo kwenye red ndio tatizo.

Customer Service kazi yake (kwa kiasi kikubwa) ni kumpa mteja taarifa, nilitegemea kama kuna tatizo kubwa na wao wanajua nategemea zena awe angalau anajua itachukua muda gani kwa hilo tatizo kutatuliwa ili aweze kuwa-serve wateja.

sikua ninamuomba zena arudishe connection kwa wakati huo, ninaelewa kuna tatizo, ila ili niweze kujipanga ninaomba tu kujua the approximate time itayochukua kabla connection haijarejeshwa.
 
Pale bongo kinatakiwa chuo kikuu cha customer service tu.

Lakini hata hicho nina shaka kama kitashinda utamaduni wa nyodo. Customer Service inataka humility na kujishusha kwa hali ya juu, ambako wengi wetu hatukuwezi, tunataka kazi tu.

Nishagombana na air hostess wa ATC kwa poor customer service, kuja air marshall ananiambia "hawa kinadada wengine wana matatizo yao kuanzia kwao huko".

Nikachoka hata kuendeleza somo.
 
Mkuu ukianza kuwawazia hawa customer cares Wa tz utaumwa na kichwa na utakuwa unaharibu siku yako kila siku. Tz bado tuko nyuma sana kwa hilo.
 
Hii ndio Tanzania.
Zena aliona kama anakufanyia favor.
Hajui kwamba wewe ndio unampa mshahara.

Sio peke yeke, wako wengi sana kama yeye....
 
Mkuu wangu tafadhali.... Hivi kama hajui ulitegemea aseme nini zaidi?. bila shaka kisha kwambai ahajui wewe bado unataka akueleze approx. itachukua muda gani wakati hajui. Je ulitaka akudanganye?..au afanye guess work!

Ondoa yoooooote.

Customer Service Rep hamkatii simu mteja hata siku moja.

Mie hata rafiki yangu tu - ambaye yupo karibu nami zaidi ya CS Rep- hawezi kunikatia simu hata kwa kughafilika, seuze CS Rep ninayemlipia mshahara kwa ada zangu?
 
Mkuu wangu tafadhali.... Hivi kama hajui ulitegemea aseme nini zaidi?. bila shaka kisha kwambai ahajui wewe bado unataka akueleze approx. itachukua muda gani wakati hajui. Je ulitaka akudanganye?..au afanye guess work!

hapo ndio kwenye tatizo, anatakiwa ajue
 
Mimi pia nilishapata majibu ya kusitaajabisha nikipiga Startimes kule kunako king'amuzi nilijibiwa utasema nimetongoza na ndo sitakiwi na mwanamke yule nilijuta hadi lisilobudi nikaenda ofisini

hili ni tatizo kubwa sana TZ, inabidi ukikutana nayo uwe unatujulisha ili tuwajue, nashukuru kwamba umesema ni startimes lakini nasikitika hujaweka na details kabisa, i mean ukiongea na mtu get his/her name, hapa picha ya startimes inachafuka na kumbe ni mtu mmoja tu
 
Tatizo kubwa ni hawa HR wetu maana wao waajiri kupitia Facebook na akishapewa hongo ya nyuchi. Fanya utafiti utakuta ni mbovu sana na kasomea vyuo vya Yombo huko. Even the Law of how to treate the customer she don't i.e(Treat the Customer the way you want to be treated). Unaleta jeuri kazini kwa kuwa aliyekuleta hakutaki tena yaani KISIMA PUMBAFUU weeeeeee!
 
ni kweli tuna tatizo la watu wa customer care lakini wakiajrliwa watu kutoka kenya au nchi nyingine tunakuwa wa kwanza kulalamika oh wageni wanachukua ajira zetu matatizo hayo yapo kuanzia bar,benki,ofisi za serikali,Nssf na hasa ukifikiria wewe ndie unayefanya waajiriwe.Nafikiri inabidi tufanye kampeni za waziwazi kupambana na tatizo hili kuna watu wengi wako mitaani wanatafuta ajira
 
Akitimliwa apewe Mhindi au mchina kesho anaanza majungu mtaani ooh wazawa hatupewi fursa!!! sisi tuna matatizo sana mtu akipewa nafasi anajiona ameshika mbingu..badala ya kutia bidii uende mbele wanakalia majungu na majivuno...watz shid sana
 
.......Nafikiri inabidi tufanye kampeni za waziwazi kupambana na tatizo hili kuna watu wengi wako mitaani wanatafuta ajira

toa ushauri, hiyo campaign ifanyikaje? mi nashauri tuwe tunawaweka tu humu ndani, au tuwaanzishie web kabisa, kila tukikutana nao tunawaweka kwenye mtandao
 
Nilipata experience isiyotofautiana na hii Airtel nikifuatilia BB Services.Nililipia huduma hii na nikawa siipati nikapiga simu Customer care nadhani mara sita ni kila nikipiga napewa sijui ticket namba next time nikipiga ni porojo tu.
Hii iliendelea for 2 weeks nikatuma hata mails kwenda CC but hata Courtesy ya kujibu haikuwepo mpaka nilipoamua kuachana nao wakiwa wameniibia 35000 na kwenda kupata huduma hiyo kwa provider mwingine.
 
ajira za maungoni sio za kichwani unategemea nini? ili upate kazi inategemea unamjua nani sio unajua nini?
 
Mitanzania bwana huyo atakuwa aliombewa kazi akapata kwa kujuana si kawaida hii
 
Back
Top Bottom