Zembwela amponda Sugu

Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,831
1,164
Ni wakati anaielezea Antivirus mixtape. Amejiuliza inakuwaje mbunge anapata muda wa kutunga matusi kwa ajili ya kuwatukana watu. Je jimbo lake la Mbeya limekamilika kwa mahitaji yake hadi anapata muda wa ziada kama huo.
 
Zembwela, najua uko eastafricaradio, una mchango mzuri kwa jamii ya kibongo, unapinga maovu mengi e.g. umeme, maji, ufisadi n.k. Sasa hapa unapoenda kwa sugu utapoteza umaarufu wako, sugu bado anakubalika ktk jamii ya kibongo.
 
akili za zembwela kama zako tu mwita..hamna hata tofauti..mkikutana wewe zambwela na mkeo FF sijui inakuaje
 
Zembwela, najua uko eastafricaradio, una mchango mzuri kwa jamii ya kibongo, unapinga maovu mengi e.g. umeme, maji, ufisadi n.k. Sasa hapa unapoenda kwa sugu utapoteza umaarufu wako, sugu bado anakubalika ktk jamii ya kibongo.
Hata JK mwanzo alikuwa anakubalika na jamii........ na akapata kura nyingi sana za uraisi lakini 2010 kura zilipungua sana
 
Eti kisa mtu anajua kuigiza basi anapewa radio presenter,uandishi wa habari,u-MC...wakubali tu ya kwamba sugu yuko juu,mbona easy?
 
Ni wakati anaielezea Antivirus mixtape. Amejiuliza inakuwaje mbunge anapata muda wa kutunga matusi kwa ajili ya kuwatukana watu. Je jimbo lake la Mbeya limekamilika kwa mahitaji yake hadi anapata muda wa ziada kama huo.

mbona title na ujumbe haviendani..imo!
 
<br />
<br />
Antivirus vol. 2 imetoka last week wewe
kwanza hukua specific kwenye heading yako, and to answer that one, album haiandaliwi kama we we unavyoandaa posts za jf

Artists anaweza akatoa nyimbo leo aliyoandika 10-20 years ago
beats anaandaa producer na kukutana na artists studio tu
a combination makes a song/album

nijuavyo mimi kama walishaandika lyrics sugu hakuhitaji hata siku tatu kuingiza vocal na baadae kuwaacha maprodyuza wakichanganya na kuedit au kureview

lets say 5 days

sasa jiulize mawaziri wako tunaowakuta club 84 tena wakiwa na wake za watu hadi asubuhi na kutwa mnadani, chako ni chako tena kipindi cha bunge wanatoa wapi muda wa kusoma hata makabrasha ya bunge??? ndio mwisho wake wanaishia kulala kama pono bungeni na ushahidi wa picha upo

Just try to be smarter when building hoja or something.... Kuhusu zembwela, sidhani kama amemchana sugu, bali ameuliza huyu jamaa anapata wapi muda? which is a genuine question to anyone

Pia ukiwa kama mtanzania ni lazima uelwe kwamba mbunge kazi yake ya kwanza ni uwakilishi na sio kuzibua mitaro na kuchimba vyoo... yeye kazi yake ni kuwakilisha wananchi kwa watunga sheria na wapanga mipango ya maendeleo

Ningekua wewe ningejiuliza hivi RAS, DED, DC, regional/district management team wanfanya nini? kwani hata mapato na matumizi yanakua mikononi mwao?? wabunge na madiwani ni wasimizi zaidi na si watendaji?? na ukihoji anasiamamia nini sasa kama hakuna maendeleo ntakujibu serikali iliyo madarakani ni ya chama kipi hadi watu wanabaki hovyo?

NOW, HIVI RAIS WETU ANAPATA WAPI MUDA WA KUSAFIRI VILE WAKATI NCHI IMECHOKA HIVI??

WAKATABAHU
 
Back
Top Bottom