ZEC Yatangaza Tarehe ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ZEC Yatangaza Tarehe ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Junius, Apr 14, 2010.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na Mwantanga Ame

  TUME ya Uchaguzi ZEC, imetangaza kuwa uchaguzi Mkuu wa Zanzibar utafanyika Oktoba 31 mwaka huu baada ya kuvunjwa Baraza la Wawakilishi.

  Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Salum Kassim Ali, ametoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari walioshiriki semina kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

  Semina hiyo ambayo imeandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar, na kufadhiliwa na Shirika la Umoja waMataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa ajili ya Wawakilishi wa asasi zinazofanya kazi na Wanawake ikiwa ni hatua ya kujadili mahitaji ya Wanawake wakati wa Uchaguzi.

  Mkurugenzi huyo alisema sehemu kubwa ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu ujao wa Zanzibar yamekamilika na uchaguzi huo umepangwa kufanyika kuanzia Oktoba 31 mwaka huu.

  Katiba ya Zanzibar inaeleza kuwa Tume ya uchaguzi ndiyo yenye Mamlaka ya kuitisha uchaguzi ndani ya siku tano baada ya Baraza la Wawakilishi kuvunjwa.

  Alisema uteuzi wa wagombea kupitia Tume hiyo utaanza Agosti mwaka huu baada ya vyama kumaliza kufanya uteuzi wao.

  Kuhusu kampeni, Mkurugenzi huyo alisema zitanzia Oktoba 10, mwaka huu na kumalizika siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika.

  Alisema vifaa kwa ajili ya uchaguzi huo vimeanza kuagizwa na vinatarajiwa kufika nchini wakati wowote zikiwemo taa, Kompyuta na wino maalum wa kupigia kura.

  Hata hivyo, alisema katika uchaguzi huo, hakuna jimbo litakalokatwa na kubakia yale yale 50 na wadi 141.


  SOURCE: ZANZIBAR LEO & OMMYKISS WEB BLOG
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwa kawaida ninavyofahamu uchaguzi Mkuu wa Zanzibar unafanywa mwanzo na kufuatiwa na ule wa Muungano, kama tamko la ZEC ni sahihi hapo juu, nikiamini kuwa ni sahihi kwa kuwa limetolewa na afisa wake mwenye mamlaka, basi uchaguzi wa rais wa na wabunge wa jamhuri ya muungano utakuwa si Oktoba tena bali baada ya hapo, au labda mwaka huu wawe wamekusudia kuunganisha chaguzi zote kwa siku moja.
   
 3. C

  Calipso JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wache waendelee kuboronga,elimu yenyewe kama mimi, au mtu ana fani ya ubaharia anapewa tume,ndo nchi hii ilivo
   
Loading...