Zanzibar 2020 ZEC yamfungia mgombea Urais wa ACT Wazalendo Maalim Seif kufanya kampeni kwa siku 5

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,867
2,000
Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemfungia mgombea Urais wa @ACTwazalendo, Seif Sharif Hamad kutofanya kampeni kwa siku tano hadi Oktoba 20, 2020.

Chama cha Demokrasia Makini kiliwasilisha malalamiko kuwa mgombea huyo ameshawishi watu wapige kura Oktoba 27.
========

Katibu wa Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khamis Issa Khamis amesema mbele ya waandishi wa habari kwamba Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Act-Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amefungiwa kufanya mikutano ya kampeni kuanzia tarehe 16 Oktoba hadi tarehe 20 Oktoba Mwaka huu kutokana na kukiuka maadili ya Uchaguzi baada ya kuwasilishwa malalamiko dhidi yake na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Demokrasia Makini, Bwana Ameir Hassan Ameir.

Madai yaliowasilishwa mbele ya Kamati hiyo ni kuwa Maalim Seif mnamo Oktoba 13 mwaka huu katika mkutano wake uliofanyika viwanja vya Jadida Wete Pemba alitoa kauli ya kuwahamasisha wanachama wake kwenda katika vituo kupiga kura siku ya October 27 kinyume na kifungu cha 82 ambacho kimewataja watu maalumu walioruhusiwa kwenda kupiga kura siku hiyo ya uchaguzi.
 
Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,232
2,000
Hili li kitu Tume ya Maadili naona uchaguzi huu lipo sebuleni na shetani kwa mikakati dhidi ya Wapinzani. Hutu tu vyama pinzani dhaifu tunatumika tu na chama tawala

Hutukuwahi liona kabla.

Lakini Yehova Mungu ana mbinu zake dhidi ya wakandamizaji.

Kasome Biblia yako ( in Mwl. Mwakasege voice)
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,858
2,000
Angefutwa kabisa

Kushawishi watu wakapige kura sambamba na Vikosi vya ulinzi tofauti na Utaratibu ni kunajisi zoezi zima la Uchaguzi, Anyimwe Urais kama alivyonyimwa 2015 kwa kimbelembele chake cha kujitangaza kabla ya muda
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
35,194
2,000
Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemfungia mgombea Urais wa @ACTwazalendo, Seif Sharif Hamad kutofanya kampeni kwa siku tano hadi Oktoba 20, 2020.

Chama cha Demokrasia Makini kiliwasilisha malalamiko kuwa mgombea huyo ameshawishi watu wapige kura Oktoba 27.
Zanzibar kampeni siku 1 tu inatosha!

Kessy alisema ukipiga filimbi nchi nzima inasikia.
 
mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
3,211
2,000
Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemfungia mgombea Urais wa @ACTwazalendo, Seif Sharif Hamad kutofanya kampeni kwa siku tano hadi Oktoba 20, 2020.

Chama cha Demokrasia Makini kiliwasilisha malalamiko kuwa mgombea huyo ameshawishi watu wapige kura Oktoba 27.
NEC hawana mamlaka hayo na wenyewe wanajua kuwa wanasumbuka, Mtu pekee mwenye mamlaka ya kumzuia maalimu asifanye kampeni ni Maalimu Seif pekee.
 
kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,205
2,000
Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemfungia mgombea Urais wa @ACTwazalendo, Seif Sharif Hamad kutofanya kampeni kwa siku tano hadi Oktoba 20, 2020.

Chama cha Demokrasia Makini kiliwasilisha malalamiko kuwa mgombea huyo ameshawishi watu wapige kura Oktoba 27.

Ukisikia vichekesho ndio hivi - Maalim alisha maliza kazi ya kampeni, sasa anapita tu maeneo mbali mbali kuwapa Wazanzibari burudani! Wamempa adhabu ambayo haitamuathiri kwa chochote kuelekea uchaguzi mkuu! Sana sana kumpa mapumziko ya lazima
 
ndammu

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
1,953
2,000
Angefutwa kabisa

Kushawishi watu wakapige kura sambamba nabVikosi vya ulinzi tofauti na Utaratibu ni kunajisi zoezi zima la Uchaguzi, Anyimwe Urais kama alivyonyimwa 2015 kwa kimbelembele chake cha kujitangaza kabla ya muda
Tutapiga kura tareh 27 msitusumbue
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
13,200
2,000
Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemfungia mgombea Urais wa @ACTwazalendo, Seif Sharif Hamad kutofanya kampeni kwa siku tano hadi Oktoba 20, 2020.

Chama cha Demokrasia Makini kiliwasilisha malalamiko kuwa mgombea huyo ameshawishi watu wapige kura Oktoba 27.
Zanzibar kampeni siku 1 tu inatosha!

Kessy alisema ukipiga filimbi nchi nzima inasikia.
Kwa haya maamuzi wanawapigia campaign bila wao kujua .
 
funza

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
7,470
2,000
Angefutwa kabisa

Kushawishi watu wakapige kura sambamba nabVikosi vya ulinzi tofauti na Utaratibu ni kunajisi zoezi zima la Uchaguzi, Anyimwe Urais kama alivyonyimwa 2015 kwa kimbelembele chake cha kujitangaza kabla ya muda
Huu upumbavu wa neno kimbelembele ndiyo imepelekea CCM kujiona kuwa wapo sahihi kwa kila ujinga wenu maana kila anayekataa upumbavu wenu mnaona ana kimbelembeke
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom