ZEC yafunga ndoa na JWTZ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ZEC yafunga ndoa na JWTZ!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Oct 4, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,504
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Je, ni sahihi kwa vifaa vya kupigia kura kusambazwa na JWTZ? Kama Lt. Gen. Shimbo ndio anatishia namna hii, hivyo vifaa vitakapofika kwenye vituo vya kupigia kura tutakuwa na imani navyo kweli?
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi hawa JWTZ wametokea wapi ktk shughuri hizi za uchaguzi? Mbona wanataka kuvuruga amani nchini? Mtasikia mwishoni, JWTZ ndio watakao hesabu kura. Hapa naona tayari Tanzania imeshachafuka.
   
 3. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 1,994
  Likes Received: 893
  Trophy Points: 280
  ..........please please please enyi viongozi huko mnakoelekea sio!!!! hivi nchi yetu ipo katika hali hiyo ya kuhitaji jeshi la ulinzi kusimamia uchaguzi? my godess!!! had it been in Congo DRC or Afighan or Somali, it would at least make sense lakini Tanzania!!?? no no no no!!!! it stinks!! something fishy is under way!!! my take: wanataka utakapofika muda wa kuchakachua, raia wema waogope kudai/kufuatilia ushindi wao at Poll Stations!!!!

  Shimbo huko ndio kuleta vurugu sasa!!!
   
 4. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,533
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Note: JWTZ, Police.....hawana chama! acheni wafanye kazi yao kama walivyoagizwa!
   
 5. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,015
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180


  usisemw hawana chama,always wanatumikia chama kilichopo madarakani coz ndo waajiri wao then from there the simple answer wanatumikia ccm in every way so hapo nadhani jibu umelipata mkuu
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,354
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Heeee!!!

  Ina maana NEC wameshindwa kufanya hii kazi?!!! Nchi hii sheria zinavujwa waziwazi tu, and no one cares! Wengine wananyimwa haki yako ya kupiga kura, kila mtu amekaa kimya!!! Jeshi kazi yake kulinda mipaka ya nchi, sasa wameingia kwenye ulinzi wa ndani, no one says anything!!!

  Haya mambo yataleta shida in future!!!
   
 7. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 3,847
  Likes Received: 815
  Trophy Points: 280
  Jeshi la Ulinzi na Usalama - JWTZ. Katiba inasemaje kuhusiana na JWTZ. Kwa nini lijihusishe na masuala ya kisiasa.

  Nadhani huyu Shimbo atakuwa ametumwa, na Jeshi likishaanza kujiingiza kwenye siasa, ndio hapo tamaa ya kushika dola inapoanza.
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,504
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Nani anawaagiza? je, malengo ya kuanzishwa kwa JWTZ kuna hata moja la kushirikiana na tume ya uchaguzi visiwani au bara kusambaza vifaa vya kupigia kura?
   
 9. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,383
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  NEC inahamasisha watu wajitokeze kupiga kura . Imetumia fedha nyingi sana, muda n.k Ni serikali hii hii imewazuia wanafunzi wasipige kura kwa kufanya calculated timing ili 31/10/2010 wasiwe vyuoni ambako walijiandikisha. Hii ni number kubwa ya wapiga kura ..elfu sitini 60,000. Kweli hii inawezekana tu Tanzania. Wenzetu hata wakiwa nje ya nchi zao wanapiga kura. Huu ni uvunjifu wa haki ya msingi ya hao wanafunzi ya kupiga kura. Mbaya kabisa . CCM kwendaaaaaaaaaaaaaaa.
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hivi hii ni kweli imetokea au inapangwa kufanyika hivyo?....Mkuu iweke vizuri tujue imetamkwa na nani au ni kwa maamuzi gani jambo hilo limefikiwa!...Vinginevyo sasa itaonekana wazi kuwa nia ni kutisha raia!
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,532
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kusikia kitu kama hicho, hivi hali ni mabaya kiasi hiki hadi JWTZ wasambaze hayo mabox? Shimbo naona ameamua kuja na yake. Halafu tangu nizaliwe sijawahi kusikia mnadhimu mkuu wa jeshi akicomment mambo ya siasa kama alivyofanya huyu Shimbo au hicho cheo hakikuwepo? Time will tell na msishangae baada ya Mwamunyange atakuja huyu kuchukua madaraka!
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,532
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Nani kakudanganya kuwa hawana chama? Fuatilia mkuu uone, kuna makada wa chama ambao ni ma JWTZ tena si wastaafu, wako kazini bado!
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,969
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbuka jinsi wanajeshi walivyokuwa wakihamishiwa Zanzibar chaguzi zilizopita kumdhibiti Maalim Seif.

  Upuuzi huo wanauleta tena bara mwaka huu, kwani miaka ya nyuma ni nani alikuwa anasambaza masanduku na makaratasi ya kura?
   
 14. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Abdallahaman shimbo asituletee udini ndani ya jeshiiii.Kamati yao ni;
  • MRISHO KIKWETE ,
  • YUSUF MAKAMBA,
  • ABDLAHAMNA KINANA,
  • RIDHIWANI KIWETE,
  • MIRAJI KIKWETE
  • SALAMA KIKWETE,
  • SAIDI MWEMA,
  • SOFIA SIMBA,
   
 15. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zanzibar wemeshazoea jeshi kusambaza visanduku vya kura. Hata wakati wa kuandikisha wapiga kura si mliwaona majeshi kule pemba na vifaru au hamuangali chanel ten nyinyi?

  Jamani eee pemba haopwi jeshi wala polisi kwanini huku tanganyika tunaogopa jeshi? Tukiwa wamoja na ukweli hata jeshi linasalim amri kwa raia.
   
 16. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,779
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kuwepo kwake yeye katika nafasi hiyo ndio udini? au kunajambo jengine! hicho unacho dai kukemea ndichi kinacho kusumbua.
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 180
  Ubabe tuu na udhalilishaji wa jeshi of all the things jeshi lasambaza mabox?
   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,752
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  sijamuelewa ila kama kunakitu anataka kusema hv
   
Loading...