Ze Utamu Blog: Ni aibu kubwa mno kwa taifa!

Status
Not open for further replies.

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Kwanza kabisa naomba kutoa pongezi kwa wanaJF wote kwa michango yao ya kila aina katika kuibua maswala yanayoigusa jamii ya kitanzania kwa ujumla.Jukwaa hili kwa kiasi kikubwa limekuwa na mshiko ( impact) kuanzia mtu binafsi kwa maana ya kubadili fikra, mitizamo na hata tabia kwa baadhi.

Kijamii, jukwaa limekuwa ni kioo cha kupima muonekanao wa watanzania kwao wenyewe na hata kwa wenzao wasio watanzania.

Baada ya kusema haya machache kama utangulizi, nimeona nije hapa jukwaani na mada yenye kulenga kujitizama kama jamii inayoishi kwenye ulimwengu wenye kiu ya maisha yenye maana na manufaa.Mtashangaa kwamba ninazunguka badala ya kumwaga hoja jamvini izungumzwe na kukatiwa shauri.Mtanisamehe sana kwa hili maana inahitaji busara kuiweka bayana ili ieleweke na isilete maana mbaya na kupelekea kutupiliwa mbali kama kitu kisicho na maana.

Suala ninaloomba mliangalie kwa busara ili kulipatia ufumbuzi ni hili la wanawake kutupiana maneno, shutuma, kejeli na matusi manene maana kusema mazito ni understatement. Blogs zimefunguliwa za kila aina siku hizi zenye kulenga kuchafuana kusiko na tija wala manufaa kwamtu yeyote yule.

Chukulia mifano ya blogs kama theutamu, wakereketwa n.k haya yamekuwa ni majukwaa ya wanawake kutwezana, sisemi kuwa wanaume hawayatembelei na kutoa maoni, la hasha! Wanawake ndo wamezidi kupakazana na hata kuwadhalilisha wanaume ambao ni wapenzi wao au wamewahi kuhusiana kimapenzi.Wanawake hawa wamediriki hata kuwachambua hao wanaume wapenzi wao kwa kuwasasambua vilivyo ikiwa ni pamoja na kuwa describe sehemu zao za siri kwa namna ya kuwatweza. Ni aibu sana kuona wanawake wasomi, warembo na wenye bahati ya pekee kuliko wenzao kutumia fursa hii ya teknolojia kujidhalilisha kwa kutoa matusi bila haya wala soni.

Ukichambua kwa undani zaidi utaona kisa ch akufanya vitendo hivi vya aibu ni wivu, chuki, ujinga kama siyo upumbavu ndio vinawasumbua! Je kweli watanzania tutafika?Kama hawa ndiyo wasomi walioenda kutafuta elimu ughaibuni wanakuwa na mwelekeo kama huu, wakirudi wataweza kuwa na michango ya maana kwa jamii – mwanamke ambaye matusi yamemkaa kuliko hata jina lake atakuwa mama au mke wa namna gain? Ataweza kutoa malezi bora? Na je ataweza kuwa kioo /role model wa kuigwa ili alete sifa na manufaa kwa jamii? Mwanamke wa aina hii ni aibu kwa taifa jamani.

Na nyie wakina baba, nawaomba muwasusie wanawake kama hawa, msibabaishwe na urembo wao.Wanawatieni aibu tupu na kuwaweka kwenye mashaka makubwa. Ni aibu kaka/ baba/ uliye na maadili mema kuhusiana na wanawake kama hawa. Watengeni kuanzia leo ili wajirekebishe.Na hili linawezekana maana hao wanawake wanajulikana.Jifikirie wewe mwanaume unayeheshimika ni kwa jinsi gani unajiweka kwenye nafasi ya kudhalilika unapoanikwa na hawa wanawake waziiiiiiii... ni watu wangapi wanasoma blogs hizi? Fikiria ni aibu gani unayompa dadako, mamako, mkeo, mchumba ( ndiyo wake na wachumba zenu wanasoma na wanahuzunika sana!) bintiyo!

Poleni wale wote mliokwisha twezwa na hawa wajinga wasiokuwa na maadili!

Naomba kutoa hoja.
 
Ungeanza na MACHANGUDOA anaopambana nao Mzee Kova. Hayo ya kwenye blogs ni sinema tayari.
 
...just Ignore them WOS, hudhani ulivyoziweka hizo link humu ndio ume zi publicize zaidi?, maana kuna 'wataoshawishika kuchungulia'...!
 
Wawe machangudoa au hawa wa kwenye blogs, nafikiri issue ni kuwa uwezo wao wa kufikiri unawasisi, kwa sababu wanasema that which goes round must come round, just imagine leo unajiona kuwa wewe ndie mbabe wa kuwachambua watu na kuweka picha aidha zako za utupu au za wenzako. kuna siku utakuwa umetulia labda na familia yako basi hiyo picha au vipande vyako vinafukuliwa. That which should not be done in the broad daylight, should not be done at all!
 
...just Ignore them WOS, hudhani ulivyoziweka hizo link humu ndio ume zi publicize zaidi?, maana kuna 'wataoshawishika kuchungulia'...!

Unajua Mchongoma... si kusudi kupublicize..lakini pia si vibaya kujua kinachoendelea ili kukemea kwa nguvu zote..na hasa akina kaka na baba wanaochamnbuliwa humo..najua wakiona wenyewe watawasusa hao wanawake wenye midomo michafu..waliokosa ustaarabu...
 
...just Ignore them WOS, hudhani ulivyoziweka hizo link humu ndio ume zi publicize zaidi?, maana kuna 'wataoshawishika kuchungulia'...!

Mchongoma,

Nafikiri, idea hapa haikuwa ku-publicize, kuna vitu ukiandika lazima utoe ushaidi la sivyo vinakuwa udaku, na nafikiri WOS alikuwa anajaribu kufanya hivyo.
 
Mh. naona hapa umeniwahi, hata mimi nilikuwa nataka kuweka jambo hili hapa jamvini.
Yaani ni aibu tele unapokwenda kusoma kilichomo mle ndani. Hali hii itahatarisha AMANI katika jamii ya Watanzania. Nasema hivyo kwa sababu nina ushahidi kamili kuwa mzazi wa mmoja wa mabinti ambaye picha yake imefanyiwa usanii (Photoshop) alipoteza FAHAMU pale alipoonyeshwa one of those blogs. Na huyu mama ni mtu mzito kwenye idara moja ya usalama Tanzania.
Na wengine wamediriki kutamka na kuahidi kuwa wataanza kuchomeana USCIS (United States Citizenship and Immigration Services). Sasa hapa tunakwenda mbele, piga maktaim au tunatudi nyuma.

Naamini kila mtanzania au grupu fulani linakuwa na interests zao. Lakini jamani siamini kwa utamaduni wa kitanzania interests zetu zipo katika divisions. Ukijaribu kuangalia kwa undani zaidi hakuna ukweli wowote zaidi ya CHUKI, WIVU and more.

Humo wanatukana hata watu wazima ambao ni mama zetu. Na hii ndio inazidisha chuki maana mtu kama mimi nitakubali unifanyie lolote lakini si kumtukana Mama yangu. My mother means everything in this world. Mie binafsi au familia yangu haijaandikwa lakini kuona Mzazi wa Mtanzania mwenzako anatusiwa na binti ni FEDHEHA.

Sasa mama aliyezirahi kwa kuona photoshoped pic ya mwanae kaahidi kulifuatilia suala hilo kwenye vyombo vya sheria (Sijui sheria ya nchi gani - anajua yeye mwenyewe) ila mie binafsi sitapendelea kuona blog hii inajenga chuki katika jamii ya kitanzania. Watu tunatakiwa kupendana, kusaidiana na kuheshimiana.
Nitatumia akili, busara, utaalamu, influence pamoja na negotiation kuhakikisha hii blog haijengi mtafaruku katika jamii yetu ya kitanzania.
Nikikamilisha kazi nitakujulisheni kilichojiri.
UTAMU and WAKEREKETWA STOP THESE NONSENSE.
 

...waswahili ndivyo tulivyo, mambo yetu ya kiswahili swahili tu hata ughaibuni, nchini kwa watu, aibu aibu tuuu...

Ninachoshukuru Jamii forums ni umakini wa Moderators wake, ingawa kwa sababu za 'kiubinadamu' mara nyingine wanawakwaza baadhi, lakini ukiyataka 'ya nguoni' unaomba leseni mwenyewe kwenda 'mambo ya kikubwa'.

Kuwataja hao kina Utamu, wakereketwa etc hapa ni kuwapa ujiko tu, anyway, point noted and taken. Shukran.
 
The gift and curse of economic development and technology; one day they will be strip clubs and red light districts in Tanzania just like in the USA, Holland and UK... you cant have your cake and eat it too... there will be some undesirable repercussions of globalisation. Cant fight it just dont visit the website (even if ur picture is up there), just like how Chenge and his buddies cant do anything about JF(although JF is doing it for the good of TZ), it will be impossible to deal with imbiciles like this.
 
Picha unazoziona kwenye hizi blogs nyingi zinatokana na machangudoa hawa walioko barabarani.

Barabara zipi hizo unazozingumzia wewe mkuu?
Nadhani hapa tunaongelea suala zima la watu kuchafua wenzao na siyo uchangudoa...... una habari kuwa kuna watu wanadhalilishwa kwa kutukanwa kwenye hizo blogs na hawahusiani na uchangudoa wala kusimama barabarani? rejea posts za wengine uelewe tunachokizungumzia hapa MKUU!
 
Utotot tu unawasumbua wakizeeka watajutia. Shame upon them

But twende mbele na kurudi nyuma....
Hizi picha za utupu hawa wenye blogs wanazipata wapi?.... Mimi nasema katu usimwamini yeyote hata mumeo au mkeo akupige picha ya utupu kwa tiketi ya mapenzi... you never know what s/he can do nazo ukiachana naye... Inasikitisha
 
Barabara zipi hizo unazozingumzia wewe mkuu?
Nadhani hapa tunaongelea suala zima la watu kuchafua wenzao na siyo uchangudoa...... una habari kuwa kuna watu wanadhalilishwa kwa kutukanwa kwenye hizo blogs na hawahusiani na uchangudoa wala kusimama barabarani? rejea posts za wengine uelewe tunachokizungumzia hapa MKUU!

Kama hivyo ndivyo; PICHA ya UTUPU yangu (au yako!) wataipataje hadi wanidhalilishe kiasi hiki?
 
I need air, air! that was horrible. May God have mercy on them, nilichogundua ni kwamba kama mtu ana chuki na wewe na akapata picha yako hata kama ni ya kawaida ataipeleka na kusema wewe ni malaya. kama picha ya wema pale wamefanyia tu utundu kiwiliwili sio chake. Pia Joyce omindo, oh God i was so shocked but naye mtu tu kamwonea dada wa watu kapeleka picha yake tu na kumsemea mbovu sijui alimkataa. Du dunia hii tunakoelekea siko jamani, unaweza kupatwa na presha ukijikuta huko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom