Ze Comedy Watinga Mahakamani

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Baada ya mvutano wa muda mrefu na kituo cha TV cha EATV baada ya mkataba wao kwisha na "Ze Comedy" wakasaini mkataba na TBC1 kisha wakapata pingamizi kuhusu matumizi ya jina "Ze Comedy" ndani ya Runinga ya TBC1 toka kwa msajili wa nembo za biashara kwamba hata majina kama "Masanja Mkandamizaji, Joti, Mpoki, nk." Kwamba yasitumike katika kituo cha TBC1, sasa nao Ze Comedy wameamua kwenda mahakamani kupinga amri ya EATV kuhusu matumizi ya jina Ze Comedy na majina yao. Pia watadai fidia ya milioni 200 kwa kufanyiwa mizengwe hiyo.

Mimi nawaunga mkono hawa jamaa maana tanguzamani nilikuwa nafahamu kuna Joti na Mpoki. Achilia mbali jina Ze Cmedy na Masanja na wengine. Hii ina maanisha kuwa hawa EATV watataka hata sura zao zisionekane katika TBC1 kitu ambacho hakiwezekani.

Tuchangie
 
wabongo atupendani hata kidogo ndio maana kuna mafisadi wengi mpaka kwenye makanisa!!!
 
Tuchangie[/QUOTE]

Tunachangiaje sasa??
Tuonyeshe mshikamano katika kutete haki za wasanii, especially wakiwa wanaonewa na huku talent ni God give.
 
Kweli kabisa kama wanawakataza wasitumie jina Joti,Mpoki n.k eti ni yao EATV si kweli.
Kwani haya majina toka zamani hawa walikuwepo na walikuwa wanatumia majina haya haya sasa hapo wanakuwa hawawatendei haki kabisa.
BAadae watasema hata sura zao ni haki yao,sijui hawa COSOTA vp? mm naomba sheria ichukue mkondo wake kama ndo hivyo na hao EATV wawalipe hao akina Joti,mpoki n.k kwa maana ni majina yao na ni haki yao wawalipe fidia kwani wametengeneza faida sana kwa kuwatumia hawa jamaa na sasa EATV imepoteza mwelekeo kabisa matangazo yaliyo kuwa yanawalipa kwa kupitia Ze comedy hayapo tena.Ukata unanukia EATV.
 
Tatizo ya EATV ni wivu tu huo unawasumbua kwani wanajua zile hela za matangazo walizokuwa wanazipata katika kipindi cha 'the commedy' ndo basi tena.

Kama walishindwa kuwahudumia vizuri walijua hakuna mtu mwingine atakayetaka kufanya nao kazi?

Last week niliona mwanasheria wa EATV amewapa TBC1 siku kumi na tano kuacha kutangaza matangazo ya ZEE COMEDI
 
Mimi namshauri Bwana Reginald Abraham Mengi afikirie mara mbili katika suala hili.Inawezekana kweli kisheria ana haki ya kuwazuia kina Mkandamizaji kufanya vionjo vyao pale TBC,lakini does that denial serve public interest? Umma wa watanzania interest yao ni kuwaona wale vijana wakiwapa raha ,kwao it does't matter ni katika channel ipi,kwa mtazamaji TV ni Tv tu.Hizi infights zake na kina Manji aangalie zisije zikampotezea mwelekeo kibiashara,Manji has got little to lose,he stands to lose a lot.
 
Ze Comedy walikurupuka. Cha kufanya, TBC1 wanunue hiyo nembo ya biashara na haki miliki kutoka EATV




.
 
Wapambanapo fahari wawili,ziumiazo ni Nyasi.
Huu ugomvi wa Manji na Mengi unawafanya hawa watoto wakose msosi na vitambi hata mng'ao utaondoka kabisa.Mahakamani huko nako kuna siasa tu,itawachukua mda mrefu kesi kuhukumiwa,na hukumu itakuwa ile ile ya siku zote ambayo ni ya kulinda hawa wafanyabiashara,kwa kuwa kodi za hawa watu ndo zinawalipa mahakimu,bongo dari salama kweli.
 
Naomba niwarejeshe zamni kidogo utagundua ni kwanini Mengi na timu nzima ya EATV wanataka kuwaangamiza Ze Comedy

Tatitizo siyo waao ila ni TBC
Kama utakumbuka wakati ule wa Kugombea kuonyesha World Cup,TBC walishindanishwa kibiashara na ITV na TV zingine huku wao wanpewa Ruzuku na serikali,Hivyo Mengi alipinga sana kwa chombop cha serikali kufanya biashara kwa kushinda na vyombo ambavyo vinajiendesha vyenyewe.

Utakumbuka Mengi alitoa hadi tamko,na hii ilikuwa baada ya Tido kuingia Pale,Hii ilimuuzi sana Mzee Mengi na Mpaka Leo anaendeleza Libeneke na siyo Rahisi kwa yeye kuwaruhusu Ze Comedy waendelee na Biashara na EATV,yaani ni bora wangeenda TV nyingine na Siyo TBC

Ushauri kwa Mengi na Wakurugenzi wake
Baada ya wao kuaha kabisa kushirikiana na TBC ,ningeomba kwanza wakae chini na kuondoa Tofauti zao hata kama ITV ilikuwapo toka zamani na washirikiane,

Pili awaruhusu vijana hawa waendelee na kipindi chao pale TBC,Najua kimapato imewaathiri sana hasa fungu lilikuwa likitolewa na Tigo kila mweiz ambalo sasa wamelikosa.
 
Wakuu nadhani ndiyo maana watanzania na waafrika hatuendelei kwa sababu tunapenda shortcut ya mambo! We always like looking at the things the way they ought to be and not the way they are.

Kama walivyosema wengine, hao Ze commedy wangekuwa na washauri wangeamua kuongea na kuinunua hiyo nembo au haki miliki kutoka EATV. Jamani tusiangalie mambo kwa kutumia hisia. Hapa ni sheria mtindo mmoja. Nani alikwambia kwamba unaweza kuishi kwa jasho la mwenzako?

Nani alimjua Masanja, Joti et al, walipokuwa hawajapewa jukwaa na mzee Mengi pale EATV? People be real! Hapa hakuna uonevu hata kidogo! watu inabidi wawe serious na wanachokifanya. Mzee Mengi siyo Red Cross kwamba anatoa msaada au anafanya kazi ya huruma!

Tatizo la hawa vijana walilewa na sifa na umaarufu wakajua kwamba they are on top of the world. Kifupi waongee na EATV waangalie ni namna gani wanaweza kusaidiwa.. Lakini siyo kutumia hisia...

Hizi arguments ohh..wasaidiwe, vijana wanajitafutia riziki, Mengi hana huruma..etc..its just crap..Mengi is a businessman..hayuko pale kuonea watu huruma! Labda wataalam wa intellectual property waje hapa watupe mwanga zaidi. But to me, in all fairness..EATV have all the rights on ZE COMMEDY and everything asscoaited with that name!
 
Mi nafikiri hapa ni kupigania hayo majina yao ya Joti, Mpoki, n.k, kuhusu ze comedy watafute jina lingine walisajili, hapo kinachopiganiwa na EATV ni kutaka walipwe na TBC1, au kuwalaza njaa hawa vijana.
 
Ze Comedy walikurupuka. Cha kufanya, TBC1 wanunue hiyo nembo ya biashara na haki miliki kutoka EATV




.

NO NO NO.
wanunue wakati ni majina yao halisi toka zamani tunamjua Joti,Mpoki sasa wanunue vp?Na jina si hilo wamebadili wanaitwa ZEE COMED.
 
Wapiganapo fahali wawili ziumiazo ni nyasi
EATV baada ya kusikia jamaa wanataka kuchomoka tena kwenda kwa mahasimu wao TBC
jamaa wakacheki mkataba na kuweka vizuri ili wasichomoke kirahisi
Tatizo la MANJI anakurupuka ndio maana hata Mengi alishinda ile kesi
Jamaa wangetafuta jinsi ya kuchomoka au kufanya masahihisho ya mkataba kwanza
 
I think EATV this time wameenda too far.Mpaka majina yao?kweli ze comedy na haki ichukue mkondo wake maana mimi nimemjua Mpoki na Joti kwa haya majina siku mingi tuu iweje leo waambie stop using those names?
 
EATv wana haki yao ya msingi juu ya hilo. Na hapa sisemi kwa ajili ya eatv bali ni kwa ajili ya hao akina Masanja. Suala la maisha kwao si shida kwani kama ni magari walishapewa na kama nyumba wamepangishiwa (Waangalie wasije wakatimuliwa baadae wakipoteza umaarfu ama biashara ya ufisadi ikitokomea). Cha msingi ni kwamba wao walikurupuka kwa kuingia katikati ya ugomvi wa Manji na Mengi (na hapo sioni kosa la Mengi). Vyombo vyake vya habari vimetufumbua macho watanzania tulio wengi kwani hatukujua kama huyo jamaa nii nyoka tunayeishi naye. Kwa hiyoo kama watanzania wa leo na hasa humu JF bado wanashabikia watu kama hao basi ni haki kabisa ya wapiga kura wa Chenge kumchinjia ng'ombe Chenge wao.

Leo hii Manji amekuwa rafiki wa walipa kodi (ama kweli kila sheitwan na mbuyu wake).
 
EATV aliingiza mtaji na kununua ubunifu, na kwamba kujenga jina ze commedy na majina ya uigizaji kulimgharmu, sasa kwa sababu TBC1 Kapenda Boga basi awe tayari kununua boga hilo na maua yake.

Kwa wastaarabu ukinunua duka la mtu na bidhaa ndani yake, katika mapatano ya bei - ingawa kwa TBC na EATV kinachofanyika ni tamaduni tofauti ya kuhujumiana - bidhaa na na hata jengo zinathamanishwa, lakini cha juu baada ya bei ni gharama ya kujenga jina la biashara ambayo kimsingi inaweza kuwa kubwa hata kuliko thamani ya jengo na bidhaa zenyewe.

Hapa TBC1, wasifikiri kizamani na kwamba vitu vinaweza kuja kuja tu kimkato, ni ufisadi pekee ndiyo unaweza kukata mbuga, mengine haiwezekani mchana, hata wachawi husubiri usiku.
 
kama kweli TBC wanafikiri wana haki na Ze Comedy si waanze kuwatumia kama Ze Comedy halafu waone kama hawatafilisiwa hadi senti ya mwisho?
 
EATV wanajiabisha... hii itawafanya wasanii wengi kuwa makini sana kufanya kazi nao... it is simply non-***** kugombana na watu wadogo kama wale ambao hata kampuni nadhani walikuwa hawana...

It is a shame... kwa maoni yangu... ingawa kisheria EATV wako sawa.
 
Back
Top Bottom