Ze comedy wa eatv kuwafunika original comedy wa tbc?

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,592
1,599
Kwa wapenzi wa wa tasnia ya vichekesho, kuna komedi ya TBC na ile ambayo imeanza pale EATV, kwa mtazamo wangu akina Joti wa TBC wameshaanz kupwaya ukilinganisha na hawa jamaa ambao wamekuja kwa kasipale EATV, akina Mtanga na Bambo. Hawa jamaa wa EATV wanachapa kazi si mchezo. WanaJF mnaonaje?
 
Kweli bana hakuna mashabiki wengi wavichekesho kama zamani,waliboa walivyo ondoka eatv,alafu hawakuwa na jipya
 
Nakubali eatv ni waanzilishi lakini hawa jamaa watadumu hapo au manji atawahamisha tena?????
 
Lakini hata wakihama bado naona eatv wamejipanga sana na wanaweza ibua makomedia wengine,ila tbc mmmh hawana ujanja wao na clouds sawa sawa
 
kweliii eeh?

Kwangu wote hovyo tu. Kuchekesha sio mpaka uvae hovyo hovyo au kubadili lafudhi.

Wote hovyo tu. Akina Masanja ubunifu zero. Kumchekesha mtu si lazima utumie nguvu za mwili na kuongea maneno mengi yasiyokuwa na msingi. Akina Mtanga vichekesho vyao ni kubana pua na kuongea sauti za ajabu ajabu. Unakuta tozi kanyoa timberland (mfano Ujio wa Kaole, Labadina etc) halafu anaongea kwa sauti ya kubana pua, hata haviendani. Tozi anataka kuigiza vichekesho vya "kibongo" halafu anataka aendelee kuonekana tozi mtaani. Angalau Masele mlevi, huyu safi ameweza kujitengenezea identity yake. Wengi hujaribu kuigiza ulevi (kama Pendapenda, Dr Kenny etc) lakini hawafikii uwezo wa Masele ambaye anaweza kuyumba, kutetemeka na kufinyafinya macho kilevi. Majuto naye vichekesho vya kitoto. Lakini watu bado wanakimbilia TV kutazama. Mi nashangaa.

Hakuna comedy bongo. Tunaweza kuwa na waigizaji (somehow) lakini ni wazi kuwa hatuna watunzi.
 
Lakini hata wakihama bado naona eatv wamejipanga sana na wanaweza ibua makomedia wengine,ila tbc mmmh hawana ujanja wao na clouds sawa sawa

Ni kweli kuwa TBC hawajajipanga na comedy kwa kuwa suala la akina Masanja kwenda TBC lilikuwa kishabiki zaidi. Hata hivyo TBC wana mawazo mengi ya kibiashara na kimaboresho. Ukiangalia kutoka TVT hadi TBC kumekuwa na mabadiliko makubwa sana. Angalia vipindi vyao na Graphics zimeboreshwa. Ila suala la comedy mbadala unakuwa mgumu sana. EATV pia watakuwa na shida kupata mbadala. Hata akina Bambo si mbadala muafaka. Walichoangalia actually si kufanya comedy ila ni kuwa na tukio litakaloaminika kutazamwa na wengi na kisha kuvuta matangazo (biashara).

Clouds ni namba nyingine Mkuu. Nakerwa na tabia yao ya ki-CCM CCM. Naichukia CCM. Ila Clouds wana uwezo mkubwa kuibua vipaji. Angalia watu waliopitia Clouds Jide, Fina, Masoud, Amina, etc. Angalia ambao bado wapo. Angalia matamasha. Angalia clouds TV, vipindi na graphics. Angalia talents na bidii za viongozi Ruge na Kusaga. Angalia investments na initiatives zao zingine. Nauchukia u-CCM wao, napenda bidii zao.
 
Aise...kumbe mambo ndio yako namna hiyo. Sasa akitokea mtu akawanyakua akina masanja pale tbc, basi no comedy at all maana tbc hawana ubunifu, kazi yao ni kuiba waliokwisha pikwa na steshen zingine...
 
Ile IPP ni Academy, inaibua vipaji ili wavitumie wao pamoja na wengine,ndo maana utakuta kuna watangazaji wengi wazuri wamejifunza kazi pale na sasa wanafanya vizuri kwingineko.
 
Wote ni feki! Jaribu kucheki The comedy show ya CNN,I think by john stewart kama sikosei,aidia ya kina joti bila shaka ilitoka hapa.jamaa hawavai vibaya au kike kike,
tatizo letu bado hatujatumia academic institutions kufanikisha mambo yetu.kila kitu 'Kipaji'
 
Kwa wapenzi wa wa tasnia ya vichekesho, kuna komedi ya TBC na ile ambayo imeanza pale EATV, kwa mtazamo wangu akina Joti wa TBC wameshaanz kupwaya ukilinganisha na hawa jamaa ambao wamekuja kwa kasipale EATV, akina Mtanga na Bambo. Hawa jamaa wa EATV wanachapa kazi si mchezo. WanaJF mnaonaje?
hapo sikubaliani kabisa.nimekuwa mfuatiliaji wa hivi vipindi viwili lakini kamwe hawa wa eatv hawataweza kuwafunika wa tbc
 
unapoigiza jinsia nyingine, kweli ni kichekesho lkn sio ndo iwe forever, imefika stage watu wanakuona ur too much better in the other side na kwa kipindi hiki chenyewe ni sodoma season two, usishangae kusumbuliwa,
 
Ni kweli kuwa TBC hawajajipanga na comedy kwa kuwa suala la akina Masanja kwenda TBC lilikuwa kishabiki zaidi. Hata hivyo TBC wana mawazo mengi ya kibiashara na kimaboresho. Ukiangalia kutoka TVT hadi TBC kumekuwa na mabadiliko makubwa sana. Angalia vipindi vyao na Graphics zimeboreshwa. Ila suala la comedy mbadala unakuwa mgumu sana. EATV pia watakuwa na shida kupata mbadala. Hata akina Bambo si mbadala muafaka. Walichoangalia actually si kufanya comedy ila ni kuwa na tukio litakaloaminika kutazamwa na wengi na kisha kuvuta matangazo (biashara).

Clouds ni namba nyingine Mkuu. Nakerwa na tabia yao ya ki-CCM CCM. Naichukia CCM. Ila Clouds wana uwezo mkubwa kuibua vipaji. Angalia watu waliopitia Clouds Jide, Fina, Masoud, Amina, etc. Angalia ambao bado wapo. Angalia matamasha. Angalia clouds TV, vipindi na graphics. Angalia talents na bidii za viongozi Ruge na Kusaga. Angalia investments na initiatives zao zingine. Nauchukia u-CCM wao, napenda bidii zao.

Mkubwa kama utakumbuku kuna wakati fulani aliyekuwa Waziri Mkuu wetu akijulikana kwa aka ya Ziro, wakati fulani kule moshi aliwaambia wafanyabiashara kuwa iwapo wanataka biashara zao zinawiri na kushamiri pasipo bughudha basi hawana budi kujiunga na SISIEM. Ni kwa msingi huo ndo maana hapo kwenye nyekundu kunakuwepo. Aidha Kipanya alipata umaarufu kabla ya kujiunga na Claudis FM.

Nikirejea kwenye wachekeshaji, binafsi namzimia yule jamaa anayejiita Maringo Saba wa Mizegwe.
 
Kuna mapungufu makubwa katika ubunifu unaoendana na mahitaji ya wateja. Walipoanza original comedy pale eat kidogo walikonga nyoyo za mashabiki. Walipoingia TBC kwa msukumo wa kisiasa na vita binafsi za vigogo wameendelea kushuka na hawa ze comedy wa eat hawana jipya. Wote hawanizuwii kuangalia vipindi vingine wangali bado hewani
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom