Ze comedi... Wanajenga, wanabomoa...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ze comedi... Wanajenga, wanabomoa...?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Dr. Chapa Kiuno, Sep 18, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wadau, jana hawa jamaa wa Ze comedi wameendeleza uhasama dhidi ya wasanii wenzao wa kutengeneza filamu baada ya kuponda kikao cha wasanii hao kilichofanyika juzi n huku wakijigamba kuwa wao hawatishiki n kwa jeuri zaidi hata wakamkaribisha Manji kwenye kipindi chao...

  Je, watakapo fulia kabisa MANJI ataendelea kuwatunza?


  USIMCHEKE MAMBA KABLA.........
   
 2. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wanajiharibia tu
   
 3. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wao wanajiona kuwa ni zaidi ya wasanii, lakini "Time will Tell"
   
 4. M

  Mary Eric New Member

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwakweli hawa jamaa sasa wamevuka mipaka, sababu wao saiv wanahela wanajiona wamefika? alafu wanaonekana bado wana utoto,wasingewajibu wenzao badala yake wangekaa kimya tu kwani wana makosa,wao wenyewe kiingereza kinawapiga chenga,na ifike muda wajue kiingereza sio lugha yetu. wakae wakijua kuwa siku hazigandi... " what goes around comes around"
   
 5. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  kwa kweli wasipojirekebisha wataangukia pabaya! wangekaa na wasanii wenzao waombane msamaha ila wao ndy kwanza wanamwagia petroli kwenye msitu.
   
 6. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wao ni wasanii, na hicho wanachokifanya ni usanii, mi naona kuzidi kuwasema ni kuwapa kichwa, bora watu wawanyamazie 2! Itafikia kipindi watajiona wajinga.
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,111
  Likes Received: 24,173
  Trophy Points: 280
  Waombe msamaha kwa kosa gani? Mi sioni kosa walilolifanya. Wamewaigiza watu mashuri kuliko huyo Kanumba hamjasema, kusemwa Kanumba imekuwa nongwa? Kanumba alifulia kama ze komedy wanavyoelekea kufulia, hilo halina ubishi.
   
 8. Johas

  Johas Senior Member

  #8
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli Nimehamini penye riziki hapakosi fitina, hayo sasa eti "wanahela" yanatoka wapi?? na wenye hela utawaweka wapi? Sawa hata kama "wanavisenti" mimi napenda kuita hivyo, si zao!!? Tuyaache hayo, narudi katika mada yenyewe.
  Jamani, wakati tulionao huu ni wa uwazi zaidi, hivi kwanini hatukubali ukweli kwamba mwezetu kalitia haibu taifa letu kule?.Sasa Ze-comedy wanapofikisha ujumbe kwa jamii ki-urahisi zaidi ili wasanii waliopo na wengine wajifunze, tunaaza kujenga na kuweka "informal gathering" vilizojaa lugha za kashfa, chuki, majungu na fitina dhidi yao, badala ya sisi wahusika kujipanga upya katika swala hili la lugha.
  Siku zote katika maisha hapa duniani ombea yule anayekukosoa maana anakuwa ana-KUJENGA na kukuimarisha sio KUBOMOA kama wengi wetu tunavyofikilia hapa.
   
 9. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nadhani hii mada haistahili kujadiliwa...

  Zekomedi ni comedians. Kumwalika Manji hakuhusiani kitu na suala la Wanafilamu(wanamaigizo) kutokuwa na uelewa wa lugha ya Malkia. Hawa wanafilamu walipewa changamoto kwamba hizo nguvu walizotumia kupinga zekomedi kumuigiza Kanumba wangezihamishia kwenye mambo endelevu kama kupinga piracy, dhuluma kwa kazi zao na kujiendeleza kama wasanii.

  Sioni kama Zekomedi wamefanya kosa lolote kwa mtizamo wangu.

  Sasa hao wanafilamus ndio mwaona wanafanya sawa? wanajenga nini kupoteza airtime ya television kupinga ujinga?? acheni kuwaonea zekomedi.
   
 10. M

  Matulanya Member

  #10
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa mtazamo wangu ze comedy kuna baadhi ya clips wanajenga kupitia kumkosoa mhusika na kufikisha ujumbe ila kuna baadhi ya sehemu wanabomboa au kuharibu.Ile tabia ya joti ya kujambisha binafsi siifagili kabisa....Na kile kipengele cha aliyeeefulia pale wanatakiwa waangalie mbele mana siku hazigandi , ipo siku nao yatakuja kuwafika...ni sawa na kuwatukana wakunga wakati uzazi bado upo.Vijana kwa 65% huwa wanafikisha ujumbe ambao ni kuburudisha watu(kwa vituko vyao) ndo maana wakaitwa hivyo ze comedy
   
 11. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Saaawa.
   
 12. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Waacheni Ze Comedy wafanye kazi yao bwana,yaani kisa cha thread zote hizi kumuiga Kanumba???,WTf!!!..Anaigwa Pinda na suti zake za rangi mbili,anaigwa JK,wanaigwa waytu wengi tu lakini hamjasema kitu,leo kaigwa Kanumba akiongea PUMBA zake mbele ya mamilioni ya watu duniani wewe unaanza kuwalalamikia Ze komedi,kazi kwelikweli...kuhusu kufulia mkuu,isikusumbue sana,usidhani daima watu watu watakuwa juu...Walikuwepo watu maarufu(angalia wacheza mpira) lakini dakika ya mwisho nao huishia na kuwa chini tu..Unamkumbuka Power Mabula lakini?,jamaa alikuwa na nguvu kama nini,alikuwa anaweza hata kubeba gari ama kuzuia gari lisitembee lakini ilifikia kipindi aliugua kisukari akaokoka,aliishiwa nguvu mpaka Biblia ilikuwa tabu kuibeba,anabebewa...So usiwatishie Ze komedi kuhusu kufulia mkuu,muda ni wao saa hizi waache wautumie ili wakifulia tupate cha kuwakumbukia............
   
 13. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kwamba Ukweli daima unauma saana.
   
 14. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #14
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ......halafu vile ni vichekesho bana,kama wengine mmechoka kucheka,basi IPOTEZEE tu kivyako,subiria FUTUHII!!!(hawa ndo hamna kitu kabisa),ZE.. kiwango bana huo ndo ukweli
   
 15. Sal

  Sal JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa Jonas, kutokujua kiingereza ni kutia aibu taifa kivipi? kiingereza sio lugha yetu ya taifa, watanzania tunaongea kiswahili sio kiingereza. sioni aibu kwa taifa iliyotiwa na kanumba, na sidhani mafanikio ya mtu yanategemea kiingereza. watanzania tuamke sasa na tupendane tuache majungu yasio ya maana. kosa lililofanyika hapa ni kanumba kwenda bila mkalimani, lakini hana sababu ya kujua kiingereza maana sio lugha yake. wajerumani, wafaransa, wa swedish, na wengine wengi hawaongei kiingereza lakini wao wakiburuza kiingereza mnaona sawa kwa vile ni mweupe, lakini kanumba kuwa mweusi, tayari keshatia aibu taifa. hao wenye kudhani kanumba kafanya kosa, ndio wenye kutia aibu taifa, kwa kuthamini lugha za watu wengine na kudharau yao ya asili. hao ze comedi, wala hawanipi tabu, elimu waliyo nayo inasababisha wafanye hayo wanayoyafanya. hata mseme vipi watajibu tu kwa akili zao finyu.
   
 16. t

  timbwili New Member

  #16
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 15, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa issue ya Kanumba kwamba alichemsha kwenye ngeli hilo halina ubishini ni kiasi cha kujifunza tu kwani lugha yoyote ukijifunza utaimasta.ILa hawa nao inelekea wameishiwa,kwa lugha yao wameanza kufuli.Habari ya kuanza kumuonyesha huyu dogo Mhindi fisadi mara Yanga sijui imefanyaje ni mwanzo wa kufulia.Watafute vitu vingine habari ya kutuonyesha ofisi za quality group na mmiliki wake sidhani kama watanzania tulio wengi tuna interest nayo.Kama anawafadhili watafute jinsi ya kumshukuru ila sio kumuonyesha kwenye Tv ya walipa kodi kimtindo hatummaindi wala nini?
   
 17. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  wafanyacho ze comedy ni kununua muda tu kwani creation zimeisha na wamejifungia ndani hawataki changamoto.

  JAMII IKILALAMIKA MJUE NI SAUTI YA MUNGU. hivyo akina JOTI ambao wanajidhania wamesimama basi waangalie wasianguke
   
 18. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Atlist mkuu wewe umeongea la maana maana wengine walikuwa wanawasuuport kwa kitendo chao cha kumsema mwenzao! Hao ndy wanao thamini lugha za nje ili hali wazungu wenyewe hawashobokei yao.
   
 19. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Dah,bradha...Mkalimani wa nini tena ndani ya jumba la Big bradha????,cha msingi KANUMBA hakuwa na sifa za kwenda ndani ya jumba lile,period..Labda kama ingekuwa inaruhusiwa kuongea Kiswahili na Kisukuma ndo angalau angekuwa na sifa ya kuingia,swali ni nani alimruhusu KANUMBA kwenda kule ilhali wanajua kabisa kwamba ni MAIMUNA na medium ya communication ya pale ni Kiingereza???????????????????
   
 20. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  mzee mbona hukuitwa wewe kwenba BB4 kuwakaribisha wawakilishi wa nchi mbalimbali, ameitwa Kanumba kwa sababu yeye ni Celebrity na ilitamkwa kwamba jamaa anatoka Tanzania, hivyo anapochemsha ni aibu kwa Taifa kwa maana hizo ndio product zetu, sasa Ze Comedy wana Tatizo gani kuigiza yaliyojili huko bondeni, mimi nadhani hii ni changamoto kubwa kwa bwana Kanumba kutafuta kozi ya ungenge kwa sababu yeye ni Celebrity na muda wowote anaweza itwa kwenda kwenye maoccasion makubwa kama hayo ili atoe keynote, sasa kwa broken kama ile sijuhi kama jamaa watamwita tena
   
Loading...