Z'bar, Vunja Sheria Uende Zako! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Z'bar, Vunja Sheria Uende Zako!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Frankie_ngoka, Nov 11, 2009.

 1. F

  Frankie_ngoka Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Salim Said Salim

  WIMBO maarufu wa dansi wa watoto wa mji kasoro bahari, Morogoro, umetokea kupendwa kwa mantiki yake juu ya hali halisi ya maisha. Kilichopendwa hasa ni ile tahadhari iliyotolewa inayosema, "Tenda wema wende zako…usingoje shukurani."
  Lakini, uzoefu mpya wa maisha hapa Zanzibar sasa unatuonyesha kile unachoweza kukieleza kama "Fanya uzembe na vunja sheria uende zako…usingojee kuwajibishwa."
  Kwa maana nyingine huoni watu kuwajibishwa kwa maovu wanayofanya wao moja kwa moja au kwenda sambamba na kuwajibika kwa kosa liliofanywa na taasisi anayoiongoza.
  Inapotokea idara ya serikali kuwa na zaidi ya asilimia 10 ya wafanyakazi hewa kwa miaka, maelfu ya watu kujiandikisha kupiga kura zaidi ya mara moja kama ilivyofanyika, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar katika uchaguzi wa mwaka 2005; huoni mtu kuwajibishwa kisheria na boti, majahazi na meli zinapozama na watu kupoteza maisha huoni kuwapo uwajibikaji wa kweli.
  Kutokana na maafa ya meli ya mv Fatih kupinduka katika Bandari ya Zanzibar na watu kupoteza maisha yao huku waliopo ufukweni wakiangalia, Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, alitoa wito kwa wenye vyombo vya usafiri wa baharini kuchukua tahadhari kuepusha kutokea ajali mbaya kama hii. Ni wito mzuri na unaoonyesha kujali kwake na serikali yake juu ya maafa kama haya.
  Lakini suala ni je, hii inatosha? Wapo wanaohisi na wanazo sababu zao, zenye mantiki ya aina fulani, wanaoona wito huu hautofautiani na kile kinachoitwa stara cha kuchukua kawa ukafunika chakula ili watu wasione chakula gani kimo ndani ya sahani.
  Tume ya Uchunguzi imeundwa na kinachongojewa ni ripoti yake. Pamekuwepo na lawama kwamba nahodha wa mv Fatih alidanganya juu ya idadi kamili ya abiria aliopakia.
  Lakini tujiulize, kama alidanganya alipata wapi mwanya wa kufanya hivi kama si uzembe uliopo katika bandari zetu kwa chombo kuweza kufanya safari bila ya kuwa na uhakika kimebeba abiria wangapi na majina yao kujulikana?
  Zipo habari zinazosema nahodha amedai alipoona hali ni mbaya akiwa njiani alitaka kuipeleka meli kwenye mchanga kabla ya kuingia katika Bandari ya Zanzibar ili anusuru maisha ya watu na akakataliwa. Hili lazima ukweli wake upatikane.
  Kama kweli alikataliwa ni nani aliyetoa amri hiyo? Alipata wapi maelekezo na kwa nini alifanya hivyo? Jingine ambalo jawabu lake nalo inaonekana limefunikwa kawa na halionekani kwa macho ya kawaida, labda tutumie darubini, ni kwa vile meli iliingia bandarini ikijulikana imejaa maji, hatua gani za dharura zilichukuliwa kuokoa maisha ya watu mara tu meli ilipofika?
  Haya ni masuala magumu, lakini si vizuri kukataa kuyatafutia ukweli wake kutokana na ugumu wake na kufunika mwamvuli wa "ajali haikwepeki…imeandikwa".
  Unapojaribu kupekua kwa undani utaona anayepaswa hasa kuhakikisha panachukuliwa tahadhari za kila aina, kama sheria zinavyoeleza juu ya usafiri wa baharini, ni mamlaka ya bandari na vyombo vingine vilivyopewa jukumu hilo.
  Hawa wanapaswa kutekeleza na si kukaa kimya, kwa nini chombo huondoka bandarini bila ya kukaguliwa kimebeba abiria wangapi na bidhaa za aina gani na kama ni kizima kuweza kuhimili safari ya bahari ambayo kwa kawaida huwa haitabiriki kutokana na hali ya hewa kubadilka mara kwa mara, hasa nyakati hizi ambapo upepo wa kusi huwa unapiga hodi kuufukuza ule wa kaskazi.
  Inawezekana mv Fatih ilikaguliwa na palikuwepo orodha ya abiria. Kama ni hivyo, cheti cha ukaguzi tuonyeshwe na huyo aliyekagua atueleze alifanya hivyo ndani ya chombo au ufukweni?
  Hii tabia ya kuwaachia wanaofanya madhambi na wale ambao madhambi hayo yanafanyika katika taasisi wanazoziongoza wasiwajibike kwa njia moja au nyingine inalea na kupalilia uzembe ambao unahatarisha maisha. Tubadilike ili wale wanaoamini na kuimba: "Fanya uzembe na vunja sheria uende zako…usingoje kuwajibishwa," waelewe zama hizo zimekwisha na tumefungua ukurasa mpya wa uwajibikaji.
  SOURCE: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=10273
   
 2. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2009
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Mawazo mgando haya, sisi twajua wenyewe jinsi ya kwenda.
   
 3. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Namshangaa Salim na vitu anavyoandika. Hivi naye habadiliki-jamani? Uandishi gani huu anaonesha?
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  ana andika mambo ya kwao ya Pwani
   
 5. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Amechanganyikiwa huyo mtu. -Lakini professionally- ni Mwandishi mzuri tu.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Nov 11, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mbona unajadili kuhusu mtoa taarifa badala ya taarifa yenyewe? Hayo mambo aliyoyataja hayapo Z'bar au vipi? Kaazi kweli kweli!
   
 7. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu Buchanan!kwani hujasikiapo ule msemo usemao mpenda chongo huita kengeza?
   
Loading...