Z’bar ‘mikononi’ mwa Lowassa, Maalim Seif

Kwa akili za wa Tz usishangae CCM ikashinda kila kitu kwa njia yoyote ile then Ukawa wakabaki kulalamika....mfano Umea kinondon
 
jecha yuleyule tuliyemkataa mwanzo na kuyakataa maamuzi yake leo hii tena tunakubali kuingia kwenye uchaguzi yeye akiwa katika position ileile........najiuliza walichokikataa cuf na kutotaka kurudia uchaguzi ni kipi??
 
Elimu Elimu Elimu! Uchaguzi wa Ubunge ndio Uchaguzi pekee ambao haukufutwa Zanzibar! Ndiyo maana tunao Wabunge WA CUF Bunge la JMT! Aliyekuwa Mbunge WA Dimani alifariki na kuacha Jimbo wazi, hivyo uchaguzi huu Ni wa Ubunge na sii wa Wakilishi!

WILE Uchaguzi huu hausimamiwi na Jecha, unasimamiwa na NEC, sii ZEC! CUF walisusia chaguzi za ZEC! Naamini imekusaidia kuelewa!
Kama CUF wanagombea leo. Si bora wangegombania uliopita pia (2015). Bado sijaelewa strategy yao?
 
UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ukiongozwa na Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF na Edward Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema wanatarajiwa kuunguruma leo visiwani Zanzibar.

Viongozi hao watawasha moto katika Skuli ya Fuoni, Zanzibar katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani.

Lowassa ambaye alikuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 anashiriki uzinduzi wa kampeni hizo sambamba na Maalim ambaye pia alikuwa mgombea Urais Visiwani Zanizbar kupitia CUF.

Wakati Lowassa na Maalim Seif wakizindua kampeni hizo leo, vigogo wengine kutoka vyama washirika wa Ukawa wanatarajia kupanda jukwaa katika siku zingine za kampeni ikiwemo Januari 21 mwaka huu ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni.

Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampeni yake siku nne zilizopita ambapo Abdurahman Kinana, Katibu Mkuu wa chama hicho akiambatana na viongozi wengine wa chama hicho na jumuiya zake walihutubia.

Miongoni mwa waliohudhuria uzinduzi wa CCM ni Shaka Hamdu, Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM).

Kwa mujibu wa Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar viongozi mbalimbali wa Chadema taifa akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, watashiriki kampeni za Dimani kwa nyakati tofauti.

Salim Bimani, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa CUF amenukuliwa akisema “Patakuwa hapatoshi hapa Skuli ya Fuoni, Lowassa anakubalika sana hapa na pia atapata nafasi ya kuwashukuru Wazanzibar kwa kura nyingi walizompigia katika uchaguzi wa 2015.”

Mbali na viongozi wa Chadema kuwa katika ratiba ya kushiriki uchaguzi mdogo wa Dimani pia inatarajiwa kuwa James Mbatia, Mbunge wa Jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi anatarajiwa kutua Visiwani Zanzibar pia.

Itakumbukwa kuwa uchaguzi huo mdogo utafanyika tarehe 22 Januari, 2017 kufuatia kufariki dunia kwa Hafidh Ally Tahir aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kabla ya kufariki dunia 11 Novemba, 2016 mkoani Dodoma.
MBOWE TAABANI KABISA
 
jecha yuleyule tuliyemkataa mwanzo na kuyakataa maamuzi yake leo hii tena tunakubali kuingia kwenye uchaguzi yeye akiwa katika position ileile........najiuliza walichokikataa cuf na kutotaka kurudia uchaguzi ni kipi??
Hao ndo wapinzani wetu... Huwezi kujua wanataka nini wakati gani.. Wanabadirika kama vinyonga.
Wavumilieni hivyohivyo
 
Elimu Elimu Elimu! Uchaguzi wa Ubunge ndio Uchaguzi pekee ambao haukufutwa Zanzibar! Ndiyo maana tunao Wabunge WA CUF Bunge la JMT! Aliyekuwa Mbunge WA Dimani alifariki na kuacha Jimbo wazi, hivyo uchaguzi huu Ni wa Ubunge na sii wa Wakilishi!

WILE Uchaguzi huu hausimamiwi na Jecha, unasimamiwa na NEC, sii ZEC! CUF walisusia chaguzi za ZEC! Naamini imekusaidia kuelewa!
Sawa, Nilidhani walisusia chaguzi zote za Zanzibar. Naomba unitajie wabunge wa CUF waliopo kwenye bunge la JMT kupitia majimbo ya Zanzibar.
 
Wanaccm wengi waliosema lowasa mgonjwa na atakufa wamekufa wao. Mungu si mwanadamu:
Komba
Sitta
Mtikila
kombani
Na huyo wa juzi aliyekashifiwa sn
 
Back
Top Bottom