Zawadi ya Upasuaji wa Kurekebisha Matiti BURE kwa Manesi Wapya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zawadi ya Upasuaji wa Kurekebisha Matiti BURE kwa Manesi Wapya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 28, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Zawadi ya Upasuaji wa Kurekebisha Matiti BURE kwa Manesi Wapya

  [​IMG]
  Wednesday, May 27, 2009 4:56 AM

  Hospitali moja binafsi jijini Prague baada ya kukimbiwa na manesi wake, imeamua kutoa zawadi ya kuwafanyia bure upasuaji wa kurekebisha matiti na kuondoa mafuta kwa wenye matumbo makubwa, manesi wote watakaojiunga na hospitali hiyo.Hospitali moja binafsi jijini Prague katika jamhuri ya Cheki ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa manesi katika hospitali yake, imeamua kutoa zawadi ya kuwafanyia bure upasuaji wa kurekebisha matiti na kuondoa mafuta kwa wenye matumbo makubwa manesi wote wataojiunga na hospitali hiyo.

  Manesi wengi katika jamhuri ya Cheki wanakimbilia kufanya kazi katika nchi zingine za jumuiya ya ulaya kwa matumaini ya kulipwa mishahara mikubwa zaidi.

  Mkuu wa hospitali hiyo baada ya kuona kwamba uhaba wa manesi utaiua hospitali yake, aliamua kuja na mbinu hiyo ya aina yake.

  Mkuu huyo alisema kuwa mbinu hiyo imesaidia sana kuvuta manesi katika hospitali hiyo kwani kila tangazo la kutafuta manesi kwenye hospitali yake linapotolewa manesi wengi humiminika kugombea nafasi hizo.

  Uongozi wa hospitali hiyo unawafanyia bure manesi watakaoingia mkataba wa miaka mitatu upasuaji wa kurekebisha matiti yao au wale wenye matumbo makubwa huduma za kuondoa mafuta kwenye matumbo yao utafanyika bure wakitia sahihi mkataba huo.

  Hadi sasa manesi wanane wameishafaidika na zawadi hizo za kuingia mkataba.

  Hospitali hiyo hutoza euro 2800 kwa upasuaji wa kurekebisha matiti na euro 1880 kwa huduma za kuondoa mafuta mwilini wakati mshahara wa manesi wake haufiki hata euro 1,000.

  Manesi watakaovunja mkataba kabla ya miaka mitatu kutimia watalipishwa gharama zote za upasuaji waliofanyiwa.

  Zawadi hiyo pia inatolewa kwa madaktari wanaoingia mkataba wa kufanya kazi hospitalini hapo.
   
Loading...