Zawadi Mwanangu alizompelekea Mama yake (My -X) zimezua utata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zawadi Mwanangu alizompelekea Mama yake (My -X) zimezua utata

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Shark, Feb 25, 2012.

 1. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,312
  Trophy Points: 280
  Heshima kwenu Wadau,
  Nina mtoto ambae nlimpata Kitambo tu nkiwa Form 5 Mwaka 2000 but sikubahatika kuendelea na Mama yake kwani sikua tayari kuanza Maisha ya kujitegemea wakati huo.
  Sasa yule Dada akaolewa na Jama m wengine na wakapata watoto wengine wawili akiwamo aliezaliwa last month.
  Kwakua Mwanangu ana mawasiliano Na Mama yake habari zikamfikia na kuniomba nimnunulie zawadi za Baby Starter Kitampelekee Mdogo wake aliezaliwa (kwa mama yake).
  Tatizo limekuja sasa Mume wa huyo X wangu amemsusa huyo mtoto mpya akidai ni wangu, eti na ndio maana nimempelekea Zawadi.
  Namuonea Huruma mkewe anaingia matatizoni wakati ukweli sija-do nae toka mwaka 2000 aliponizalia mtoto. Sasa hasaidiwi kwa chochote Na mumewe kiasi ananiomba kama nina hela kidogo nimsaidie.
  Nimetumiwa Wazee waje waniulize/wanishawishi niseme ukweli but kila nachowaambia hawakubali.
  Vipimo vya DNA ndio kabisaa hawaviamini eti baada ya hivi laribuni kutoa matokeo kua zaidi ya nusu waliopimwa walikutwa wamesingiziwa.
  Nifanyaje wadau????
   
 2. YNNAH

  YNNAH JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,663
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Huyo bint alikuwa andiko lako....nakushauri endelea kumsaidia hadi mambo yatakapo kuwa sawa kwani atapata shida na mtoto.
   
 3. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Huyo jamaa ****, hayo ndio matatizo ya wanaume wa kiafrica. Yaani mtu na X wake hawawezi ongea especially mna mtoto nyie, wanataka muwe kama maadui. Tatizo ni hiyo zawadi, mwambie nimempa dogo pesa awanunulie nduguze anachotaka sasa kuna kosa gani.

  Huyo alikuwa anataka kutupa majukumu yake.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Mueleze huyo baba aanze kumhudumia mkewe. Itamsaidia kumuongezea confidence kama mume! Kinachomtia kimuyemuye ni hicho tu, hamtunzi mkewe na wanae na ana wasiwasi na kila anayeonekana kama angeweza kumtunza! Nyambaff, anageoa mluo amtandike kabisa!
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hehehe huyo jamaa ni mshamba mshamba, si alijua toka long time kwamba wewe mzazi mwenzake sasa analia lia nini??
   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,312
  Trophy Points: 280
  Anadai mimi ni kama nani mpaka nipeleke hiyo Baby Starter Kit??
  Nimejaribu kua ni mwanangu ndio alioniomba nimnunulie kwa ajili ya mdogo wake haelewi. Eti anadai ni mimi ndio nliotoa ila natumia kigezo cha mtoto kuzuga.
  Cha ajabu haamini hata vipimo vya DNA, nachoogopa nikiendelea kumsaidia zaidi mkewe ndio madai yake yatakua Na nguvu, Na nikiacha kumsaidia pia naona Imani kwa mwanangu kwamba ndio chanzo.
  Kweli nimekamatika wadau.
   
 7. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,312
  Trophy Points: 280
  Nkiendelea kumsaidia si ndio itathibitisha madai ya mumewe kua mimi ndio baba wa huyo mtoto mpya hivyo napeleka hela ya matumizi kijanja????
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  miafrika ndivyo yalivyo yaani mi naona alikuwa anatafuta gia ya kumsusa tu huyu mke wake hana lolote huyo jamaa au kauawa nini hana kitu ndio anatafuta visababu..

  pole sana mkuu..
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Kusema "wanaume wa kiafrika" wako hivyo hakuwatendei haki wanaume wa kiafrika wengi sana waliooa wanawake wenye watoto na wanaoheshimu uhusiano wa baba, mama na mtoto.

  Sema labda wanaume wa kiafrika unaowajua wewe ndio wako valuvalu hivyo, lakini mambo ya kulundikana "wanaume wa kiafrika" wako hivi noma.

  Halafu hata hao "wasio waafrika", ambao presumably wanakuwa hawana matatizo kwa sababu wao si waafrika kuna "Jerry Springer types" kibao.

  Tusitake kuambizana kwamba uAfrika ndio tatizo hapa wakati kuna mambo lukuki kama elimu, kujielewa, kujiamini, kuheshimu wenzako, mapenzi ya dhati etc ambayo hayajali uafrika.

  The grass is always greener on the other side.
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  duh, una kazi.

  Kwani, wewe unamzidi kipato huyo mumewe??
  Kama unamzidi, EGO inahusu. Na kama upeo mdogo ndo bomu kubwa zaidi.

  Kaa nae mbali, kama unamsaidia iwe kwa siri sana. Inabidi na mwanao apumzike kidogo kwenda kwa mama yake which is not fair kwa mtoto.

  Lakini upande wa pili, ni bora kuwa naye mbali angalau aweze rekebisha ndoa yake kwanza.
   
 11. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  ukiangalia kwa haraka unaweza kumlaumu huyo jamaa lakini upande mwingine jamaa uliyepeleka hiyo zawadi si ustaarabu, na jamaa ana haki ya kuhoji uhalali wa wewe kupeleka zawadi kwa mkewe kwa vile wewe ulikuwa ni hawala hata kama mmeachana kumbuka mna mtoto ambaye yawezekana mlikuwa mnawekwa karibu kimawasiliano ..

  kaa chini ufikiria kiustarabu nini ulitakiwa kufanya ..
   
 12. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  tOA HIYO HELA NA AKIGAIN PATA KITU KUTOKA KWAKE
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Hakuna "jamaa" aliyepeleka zawadi hapo, zawadi imepelekwa kutoka kwa mtoto kwenda kwa mdogo wake kwa mujibu wa maelezo (ambayo kamwe hayawezi kutupa picha kamili kwa sababu ni ya upande mmoja).

  Wewe ni mmoja kati ya wale wanaotetea wivu wa kipumbavu?
   
 14. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  pole kama una muda mchunguze huyo mbaba sijui mkaka utakuta ana yake uko nje. mara nyingi ni tabu sana wanaume kuamini wanawake waliozaa kabla hawajaolewa nao. ila saidia kumchunguza utakuta labda na yeye ana katoto huko nje etc

  Sali Mungu akuongoze.

  Kwani amehama toka nyumba wanayoishi na mkewe?
   
 15. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  labda nikuulize swali ulikuwa na mawasiliano na X-wf wako before? alafu mumewahuyo jamaa anauwezogani sasa kimaisha mana unaweza ukakuta uwezo wake wa kimaisha ni mbaya na wewe upo pazuri hivyo jamaa anatafuta msaada wanamna hiyo. lingine huyo X-wf je anakupenda wewe kumbuka ni mke wa mtu sasa hivyo hata kama anakupenda baadae anaweza kukuingiza kwenye matatzo so angalia hayo sawa best ila pole kwa hilo ila pia usiachekumsaidia
   
 16. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  mkuu usitumie lugha kali kiasi hicho .. tujaribu tuangalie pande zote usahihi na nini si sahihi .. tusiunge mkono upande mmoja , hebu jaribu kuvaa hivyo viatu na uone nin ambacho ni sawa na si sawa
   
 17. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Pole sana mdau!Umewashirikisha wazee wako na wazee wa pande nyingine zote mbili katika kutafuta suluhu?Hebu jaribu kufanya hivyo na nashauri kama hali ikitulia mkataze mwanao kwenda kwa mama yake kwa muda flani hii itasaidia kurudisha amani kwa mwanaume mwenzio inawezekana hata kwenda kwa mwanao pale kwake ni tatizo sana kwake!!
   
 18. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #18
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,312
  Trophy Points: 280
  Ki uwezo niko vizuri mara hata ishirini kuliko huyo jamaa (sijisifu)
  Mimi nakaa Kijitonyama na yeye anakaa Tandika ambapo isingewezekana mtoto aende kwa daladala wakati baba yake nina Zaidi ya Gari 3 zakutembelea ukiacha za Biashara so ilibidi nimpeleke mwenyewe.
  Hata Zawadi nimempeleka mwenyewe Mtoto madukani kutafuta maana kwa Miaka yake 12 sidhani Kama angeweza kununua mwenyewe hizo zawadi.
  Wala isingefaa eti nimfikishe karibu Na Nyumba nimuache aingie mwenyewe Na zawadi zake kwani nayo pia isingependeza kama wangejua mtoto kaletwa Na mimi nikaishia njiani.
   
 19. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #19
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  haitakuwa busara kumzui mtoto lakini lazima kuwe na mipaka katika wazazi na si kupitia kwa mtoto kuonyesha hisia au umuhimu fulani
   
 20. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #20
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,312
  Trophy Points: 280
  Wazee walioshirikishwa hapa ni wa upande wa pili, but tatizo la wazee hawa ni kua tayari wana " Marking Scheme" zao kichwani, eti wananiambia nikubali kua mtoto ni wangu ili yaishe
   
Loading...