Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,550
- 19,416
Maj. Gen Zawadi Madawili ni mwanamke ambaye binafsi nimekuwa namheshimu sana maisha yangu yote tangu nimfahamu wakati aliopongoza mbio za mwenge mwaka 1975 akiwa luteni wa jeshi la wananchi wa Tanzania. Baada ya mimi binafsi kupitia mafunzo ya kijeshi ndipo nilipozidi kumheshimu sana mama huyo.
Serikali ya Tanzania ingefanya jambo moja la maana sana kwa kumpa nafasi pekee Jenerali Madawili baada ya kustaafu kwake jeshini awe na jukumu kubwa sana katika nchi hii kuhusu haki za wanawake.
Wanawake wengi Tanzania wanaonewa sana kijinsia na waajiri wao ama kabla ya kupewa kazi au baada ya kupewa kazi. Ingawa mama Madawili siyo mwanasheria, ana jina kubwa sana ambalo angeweza kulitumia kwa kusaidiwa na wanasheria kuhakikisha kuwa wanawake wote wa Tanzania wanapewa haki na heshima kama binadamu wengine.