Hii ni zawadi kwa waungwana kuhusu ukweli kuhusu moyo.Kwa wale tunao amini uwepo wa Mola muumba ukweli huu tunapaswa kuujua na kuufanyia kazi.Wale wasio amini uwepo wa Mola wanaweza kuchagua moja.
Malengo ya Moyo kwa binadamu
Hakika hali wa shani kila kiungo cha mwanadamu kimeumbwa kwa lengo maalumu,na laiti kama kiungo hicho kikitumiwa kinyume na malengo kwayo kimeumbwa bila shaka mwenye nacho atakuwa anakosea pakubwa sana.Hii kama ilivyo macho kwa mwanadamu amepewa kwa ajili ya kutazama na kuona,masikio kwa ajili ya kusikiliza,miguu kwa ajili ya kutembea,ulimi kwa ajili ladha na kuongea sambamba na mdomo,pua kwa ajili ya kunusa,ngozi kwa ajili ya kuhisi mguzo na mfano wake,mikono kwa ajili ya kushika na mfano wake,viungo hivi ukivitumia kinyume na malengo tunasema umeidhulumu nafsi yako na unaingia katika makosa,ndivyo ilivyo katika moyo.
Mtume wetu amani ya Allah iwe juu yake anasema "Katika mwili wa binadamu kuna kipande cha nyama,kikitengemaa kipande hicho bila shaka mwili waote umetengemaa na kikifisidika kipande hicho cha nyama basi mwili wote umefisidika,na hakika kipande hicho cha nyama ni MOYO".
Huo ndio moyo jamaa,yaani mama wa viungo vyote vya mwili ni moyo.Na tumepewa moyo wanadamu ili tutambue mambo kama yalivyo.
.......inaendelea
Sehemu inayofata tutaangazia kuhusu kazi za MOYO