Zawadi gani zilikushangaza wakati wa harusi au party yeyote

Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,739
744
Habari wanajamii,
Mimi nimefunga ndoa weekend iliyopita yaani jmosi ya November 26, 2011. Katika zawadi nilizopewa zote zilikuwa nzuri lakini zawadi mbili zilinishangaza jinsi zilivyokuwa zimeendaliwa.
Zawadi ya kwanza ilifungwa vizuri sana lakini ndani yake hakukuwa na kitu chochote. Yaani empty box.
Zawadi ya pili nilikuta vitu ambavyo sikuweza kujua nini lengo la mtoa zawadi, kwanza ilifungwa very rafu na used gift paper, baada ya kufungua nikakuta magazeti ya zamani machafu na yamechezewa sana, nikakuta karatasi za kitabu either ni cha darasa la pili au la tatu lakini kimechakaa na kimechezewa sana. Pia nilikuta nyanya moja iliyoiva, kitunguu kimoja, mhindi mbichi mmoja, machungwa mawili, sahani moja na kijiko kimoja. Na tayari vilikuwa vimeanza kupata uvundo. Zawadi zote watoaji waliandika majina hizi mbili sikuona majina yao. Na nilishindwa kuunganisha matukio. Mtaalam atafsiri nini maana yake. Lakini je wewe uliwahi kukutana na zawadi kama hizi au zilizokushangaza? Naomba kuwasilisha
 
Kuna bingwa aliwahi kuleta box la condom pale DDC Kariakoo, tena wazi bila ficho lolote!
Ile hata Ulaya hapana pata namna hii...
 
Hawakutaka kuwapa zawadi hao. . .
Ila huyo wa pili inawezekana ana kinyongo na mmoja wenu au nyote wawili.
 
Ktk birthday yangu Jamaa alinipa zawadi bahasha mbili,moja ikiwa na tsh 10000 na ya pili ilikuwa na kadi ya mchango wa harusi tsh 15000/- dah nilichoka balaa
 
Amani ya milele njooni twende kwake karibu diamond 4dec upate nia ya amani kupitia ujumbe ama wajumbe wa christ ambassador from kgl
 
Kwanza hongera kwa kufunga pingu za maisha.Huyo wa empty boz alifunga love and kissesHuyo wa pili aliona maybe mtaamka na njaa hivo akafunga chakula kidogo but kikaharibika. Basi, chukulia ni watu wanakupenda ila hawakua na hela maana ukianza kujiuliza mengi sana utaishia kuchukia watu bure na ndoa changa haianzi kwa kuwachukia watu.
 
Mpwa kama vipi kama una zo box kachungulie mkanda wa harusi utamwona live akija na manjonjo bila kujua kuna cctva unless acheze na jamaa wa kamera wachomoe hiyo part..m nilipoangalia kwenye zile box mojawapoalikuwa jirani yangu kabisa tena mtu na mkewe ...usiniulizee zaid.......nikawabariki amoja na hilo mke wangu aongei nao hata akienda kwa wakwe
 
Kabla hatujafungua tuliziombea zawadi zetu mimi ni mkatoliki tukasali na rozari pia. Tulipoiona hii zawadi mke wangu alichukua sahani na kijiko na baadaye akataka machungwa tuyale lakini nafsi yangu haikuwa na aman kabisa, nilichokifanya sikumwambia inauhusiano na ushirikina ila nikamwambia hebu ilete hiyo sahani nikarudisha kwenye box lake sikuwa home nilikuwa hotelini nikaenda kuitupa kwenye dustbin. Nashukuru kwa tafsiri na ushauri sasa nasubiri nione mkanda wa video ni nani aliyetoa zawadi hizi.
 
Back
Top Bottom